Ligaba
JF-Expert Member
- Oct 12, 2018
- 1,063
- 2,874
Kwa kweli namuonea huruma sana Rais wangu mpendwa mtetezi wa wanyonge John Joseph Magufuli. Namuonea huruma kwa usumbufu unaompata kwa tatizo ambalo angeweza kulidhibiti mapema. Tundu Lissu ni tatizo kubwa sana kwa Rais wetu. Bisha, pinga na tukana ukweli ndio huo.
KWA NINI LISSU NI TATIZO?
Kiasili watu aina ya Lissu ni SUPEREGO mbaya zaidi Mungu kamuongezea very smart brain. Watu wa sampuli hii huwa hawaamini waliowazunguka ni bora zaidi yao hivyo hukuchukulia kama underdog tu. Ukosoaji wote wa Lissu kwa Magufuli ni vile Lissu haamini kama Magufuli ni bora zaidi yake basi humuona tu kama underdog.
1. Usumbufu wa Lissu muulize mama Anna Makinda, atakupa feedback
2. Kikwete alimuelewa Lissu ni aina ya MTU gani na aliwahi kusema ni bora achaguliwe Slaa kuwa Rais lakini Lissu asiwe mbunge, kwa nini?
3. Hata waliompiga risasi ni dhahiri walimuelewa Lissu sema hawakujua njia sahihi ya kupambana nae.
4. Hata NEC sasa inamfuata
5. Angalia mahakama ana kesi sita zote zinamfuata.
6. Angalia hata CHADEMA Leo yote inamfuata anachopanga, bila Lissu unafikiri CHADEMA kingemwekea Magufuli pingamizi?
KOSA ALILOLIFANYA MAGUFULI.
Mpaka ninapoandika 7000hrs Magufuli ameshafanya kosa la kuruhusu usumbufu. Hebu niambie unafikiri majina ambayo yanamyima usingizi linaloongoza ni jina la nani?. Kuepuka huu usumbufu alipaswa kuhakikisha Lissu atoboi kwa tume, au zile mahakama zenye makesi yake yangetumika kumdhibiti. Amini maandishi yangu, kumuacha Lissu agombee kunainufaisha CHADEMA kwa kiwango kikubwa sana. Hata akinyimwa urais Lissu ataongeza idadi kubwa ya wabunge, Lissu ni kama mganga aliyeletwa kufufua wafu, wapiga kura wengi walikuwa sawa na wafu sasa wanapata hamasa ya uhai kutoka kwa Lissu.
OMBI KWA CHADEMA.
Kwa aina ya siasa ya uhuni zinazofanyika sasa hivi, Lissu alipaswa kuwa mwenyekiti, MBOWE ukitaka CHADEMA ikabiliane na siasa za uharamia baada ya uchaguzi mkabidhi uenyekiti Lissu wewe bakia mlezi wa chama.
Bado nina imani tume na Rais, CCM mna nafasi ya kumdhibiti kupitia kampeni.