Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ni Jeshi la Mtu mmoja, ni Kama Batalioni nzima

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ni Jeshi la Mtu mmoja, ni Kama Batalioni nzima

KalamuTena

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2018
Posts
13,187
Reaction score
17,167
Tundu Lissu anavyoshambulia utadhani ni jeshi lenye askari wengi kiasi cha kuunda batalioni nzima. Ndiyo, inaeleweka chama chake kimempa nyenzo za watu na rasilimali chini ya kampeni yake; lakini ukitizama upande wa jeshi analopambana nalo ni dhahiri kwamba jemedari huyu anaongoza vyema kundi lake katika vita hii.

Jukwaa la Tundu Lissu, anasimama mwenyewe, hategemei Mwenyekiti wa Chama au Katibu Mkuu awashe msisimko ndani ya mioyo ya wananchi wanaokusanyika kwenye mikutano yake.

Hakuna mabango barabarani, wala wapambe kila sehemu wakipigana waziwazi upande wake kama ilivyo kwa jeshi zoefu la CCM.

Jemedari huyu sasa ndio anasuka jeshi la wananchi chini yake, jeshi ambalo hakuna IGP au amiri jeshi mkuu anaweza kulikabili na akabaki salama.

Wakati televisheni zote na vyombo vingine vya habari vinalazimika kulinda maslahi yao binafsi kwa kutoonyesha mikutano yake, mwanajeshi huyu anavyokusanya watu kwenye mikutano yake ni alama kwamba vyombo hivyo havina nguvu tena za kupasha habari. Kuna njia bora zaidi wanazotumia wananchi kupashana habari kwenye kampeni hizi.

Sasa ni dhahiri kwamba, hata zile njia za wizi wa kura walizotegemea CCM ziwabebe hawana uhakika nazo tena kama zitafanya kazi kama walivyozoea kuzitumia.

Jambo kubwa linalojitokeza katika vita hili ni hili: miaka mitano ilitumika sana kutugawa waTanzania katika makundi mbalimbali kiasi cha kuhatarisha umoja wetu.

Jeshi la wananchi analojenga Tundu Lissu linadhihirisha kwamba juhudi hizi za kutugawa katika mafungu ya kikabila, kidini, n.k., zimeshindwa vibaya sana. Jeshi la Tundu Lissu sio la wasukuma, wala wachaga au waislam au wakristo. Ni jeshi la waTanzania. Full Stop.

Tuendelee kutafuta HAKI, AMANI YA KWELI na UHURU wa Kweli.

Watanzania hawawezi kuwa mali ya mtu binafsi.
 
CCM walijidanganya mno ndani ya hi miaka mitamo...wakajiaminisha na wakawa wanaigawana nchi as if ni yao peke yao

Lissu MUNGU akulinde wewe umetuokoa katika haya makucha ya watu wachache.

Tunaona mwanga mbele yetu...finally !!
 
Watu wanashangaa Mbowe kutokuwepo kampeni za Lissu, sio kitu cha ajabu ile ni strategy. Ukweli ni kua watu wengi wanapata picha mbaya wakimuona Mbowe sababu kuna maneno ya chinichini mara anataka kua mwenyekiti wa milele, mara anapiga sana tungi na wanawake. Lissu kujionyesha kama kajitenga ni strategy nzuri sana.
 
Huyu mtu hata Mimi nimeogopa aisee ..

Jamaa anatembea mwenyewe ila anakusanya Kijiji

Imagine msafara wa Lissu ana magari 2 au 3 hivi lakini jamaa ni mwiba sana.
Huyu jamaa ana malaika kama buku hivi. Kwa macho ya nyama tunamuona peke yake lakini kumbe anasindikizwa na malaika kibao.

Hawa malaika ndiyo hupita majumbani mwa watu kuwapa taarifa juu ya ujio wake
 
Jamaa hana hata bango wala kipeperushi chochote mtaani lakini anatikisa mpaka vijijini.

...Lakini yule jamaa ana mabango mpaka klabu za pombe za kienyeji kwa walevi wenzie na mengine vijijini huko wasiokua na vyoo wameshukuru kuyapata maana wanayatawazia na kutupa vichakani... Yanachafua mazingira sana..
 
Back
Top Bottom