"Anayosema kihusu uchaguzi huru na haki iwe kweli vinginevyo dunia itashangazwa na Tanzania itaandika historia mpya!"Kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu kumepatikana mwamko na amsha amsha za aina yake!
Kupitia Safu hii napenda nijadili haiba ya wagombea urais aina ya Lissu!
Kwa waliopita ktk system ya kusolve migogoro ya power corridors ndani na nje ya nchi mtakubaliana nami hiki ninachokwenda kuandika hapa.
Duniani kote wanaotumika kuleta mapinduzi au kuongoza mageuzi huwa ni watu ambao hawana cha kupoteza ktk maisha (lumpen)
Lissu amepitia Kitu tunaita’Near Death Experience’ Duniani kote wanasiasa au wanaharakati waliopitia the Near death Experience huwa majasiri na hatari sana! Wanaopanga njama dhidi yao huchagua kufa au kupona.
Spirit Yao huwa ni kali sana na hubadilisha upepo wa mambo kwa kasi sana!
Wanaomsikiliza Lissu wanaweza kuona anatania au anatishia but psychologically anachoongea Lissu kinatoka moyoni na anadhamiria.
Miaka mingi tumekuwa tukisema upinzani umepoa na hamna wa kukinukisha ni kwa sababu hapajawai tokea Mtu wa kuongoza aina ya Lissu ambaye kwa hatua aliyopo ni Kama hana tena cha kupoteza ktk maisha.
Hivyo kupitia safu hii nasema tena Lissu asipuuzwe!
Anayosema kihusu uchaguzi huru na haki iwe kweli vinginevyo dunia itashangazwa na Tanzania itaandika historia mpya!
Nashauri tuwe na uchaguzi huru na haki kweli kweli!
"Nashauri tuwe na uchaguzi huru na haki kweli kweli!"
Kwa mujibu wa sentensi hizo mbili labda niulize tu kwamba mtu hatari ni yule anae kubaliana na sentensi hizo, ama ni yule anae zikataa?