Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Mahojiano yake na mwanahabari katika kituo kimoja maarufu cha television nchini yamethibitisha uoga na unyonge wa huyu muungwana katika kupambana na kudhibiti rushwa ndani ya chama chake mwenyewe, lakini pia imethibitika pasina shaka huyu muungwana hana uwezo wala mipango mikakati ya makusudi kudhibiti rushwa kama kiongozi muandamizi wa chama cha siasa.
Sasa ndani ya chama chake wazi wazi kaishindwa, sasa nje ya chama ndio atafanya nini?
Ndani ya chama chake aliogopa hata kuwataja tu wala rushwa aliokua akiwatuhumu kwa vitendo hivyo, na kukwepa kabisa kuzungumzia jambo hilo ndani ya vikao vya chama chake, badala yake akaamua kukimbilia kuilalamikia kwa wananchi sasa sijui ni ili tu apate umaarufu au huruma, haijulikani mpaka wa leo
Lakini pia na nje ya chama chake vile vile anaishia kujiuma uma tu na kutishia kuwataja wala rushwa kitu ambacho ni dhahiri ni uongo na ndio maana anagwaya kuwataja anao watuhumu kwamba ni wala rushwa.
Na anakwenda mbali zaidi na kudai kwamba eti aliempelekea rushwa ya mamilioni akaikataa, na hataki kuwataja walio mpelekea hiyo rushwa.
Sasa ukiangalia mtu kama huyu ambae kabisa ni kiongozi, tena muandamizi katika chama ana nia kweli kupambana na rushwa, kama anawaonea aibu na kuwaogopa wala rushwa kiasi hiki?
Ndrugu zango, huyu mtu ana nia kweli ya kupambana na rushwa? tusidanganywe tahadhali alaaaa!
Na kwa kuzingati hulka yake ya kuomba omba kuchangiwa, hivi anaweza kukataa pesa huyu kweli hata ukimtazama tu?
Nachelea kuhitimisha kwamba huyu muungwana, si tu ni muongo bali pia ni mwanamaigizo ya ukali lakini kiuhalisia ni muoga zaidi ya Hamas licha yakua ni mbishi na muongeaji kichizi.
Na hii inadhirisha tu kwamba huyu muungwana hana meno wala ubavu wa kupambana na rushwa lakini zaidi sana, hana mipango kikakati nayo na anaogopa rushwa kama ukoma.
Ni mtu asie na uthubutu kabisa wala maono ya kijasiri kwenye rushwa, ni bla blaa tu. na kwahivyo hafai kabisa kua kiongozi wa kitaifa wa chama chochote cha siasa.
Na kwasababu hiyo sidhani kama wanaChadema katika uchaguzi wao wa ndani unaokuja watakubali tena kuongozwa na kiongozi mzigo, muoga na dhaifu kama huyu kwenye mambo ya msingi kitaifa.🐒
Mungu Ibariki Tanzania