Tundu Lissu: Ni ufisadi na ufujaji wa fedha za umma kwa Bunge kuwalipa watu ambao hawana sifa za kuwa wabunge

Tundu Lissu: Ni ufisadi na ufujaji wa fedha za umma kwa Bunge kuwalipa watu ambao hawana sifa za kuwa wabunge

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Ameandika hivi katika akaunti yake ya Twitter:

Ni ufisadi na ufujaji wa fedha za umma kwa Bunge kulipa mishahara na posho kwa watu ambao dunia nzima inafahamu hawana sifa ya kuwa wabunge kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania. Ipo siku wahusika wa ufisadi huu na wale wanaouwezesha watawajibishwa. Tuendelee kukusanya ushahidi.

Capture.PNG
 
Hongereni sana Covid19 kupata fursa.Dunia hii na siasa zetu waweza kuta hata taifa halina kiongozi, ukitumia kigezo cha HAKI.
 
Hapa lisu anatamini angekuwa bungeni mana job alimwaga na kumnyima mapension yake .lisu watanzania walishampuuza bora akae kimya

Ukipewa ubwabwa kichwa chako ni sawa na mfuko wa kubebea meno. Unawezaje kutaka mchago wakati CAG kakwambia Trillion 1.5 watu wamepiga na umekaa kimya. Kwa hili bima akili yako kama ipo sawa
 
Ameandika hivi katika akaunti yake ya twitter:

Ni ufisadi na ufujaji wa fedha za umma kwa Bunge kulipa mishahara na posho kwa watu ambao dunia nzima inafahamu hawana sifa ya kuwa wabunge kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania. Ipo siku wahusika wa ufisadi huu na wale wanaouwezesha watawajibishwa. Tuendelee kukusanya ushahidi.
Tundu Lissu ana matatizo ya akili
Angehoji kwanza chama chake kwa nini kinakula ruzuku itokanayo na uchaguzi haramu
 
Nadhani ni hasara zaidi kugoma kupeleka wabunge kwenye Bunge la Nchi na kuacha zile nafasi wazi. Kama wale 19 sio halali, kwanini Chama hakichagui na kupeleka wengine kureplace wale ambao hawana baraka za chama?

Hoja kwamba kupeleka wabunge ni "kushiriki haramu" haina mashiko sana in my honest opinion maana Aida yupo bungeni kihalali akiwa na baraka za chama wakati na yeye alipatikana kwa uchaguzi uleule.
 
Lissu akae afanye maisha yake tu aachane na mambo ya siasa daa. Ashukuru mungu alimwokoa ajifanyie mambo mengne uweezo was kusumbua serikali Hana atapata msongo wa mawazo bure
 
Mbowe, Mnyika kimyaaaaaa!!! Wanapiga zaidi ya mil. 100 kila mwezi Kama hawajui kinachoendelea vile, huku nyie mmekomaa na tweet za Lissu.
 
Back
Top Bottom