Tundu Lissu ni vyema na busara kama huna uhakika Waliokushambulia ni akina nani basi Unyamaze tu

Tundu Lissu ni vyema na busara kama huna uhakika Waliokushambulia ni akina nani basi Unyamaze tu

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Huko nyuma ulianza kwa Kuwatuhumu Watu wa TISS ukatuchanganya.

Katikati tena ukaja kusema Ulishambuliwa na Askari wa Kukodi wa Rwanda.

Hukuchelewa miaka kadhaa nyuma ukiwa Ulaya ulikokaribishwa ukawatuhumu Police Tanzania.

Haya jana sijui leo nimeona Umewatuhumu Wanajeshi kwa lililokutokea.

Naanza sasa kupatwa na Wasiwasi kuwa ipo Siku utawasingizia Chama cha CCM.

Ushauri wangu Kwako kama huna uhakika au huwajui Waliokushambulia basi nyamaza tu au fanya Utafiti wako wa Kina na ukishawajua ndipo uje Kutuambia Watanzania kwani kwa sasa si tu Unatuchanganya lakini unaanza Kutuboa hata Sisi tunaokupenda na kukuunga mkono.

Sijui na Siku mfano ukija kujua kuwa Wahusika wa Shambulio lako wanatoka CHADEMA utasemaje kwani Wahenga wanasema Kikulacho Ki Nguoni mwako.
 
Serikali ya Tz yenye jukumu la kutulinda WaTz na mali zetu inasemaje?
 
Magufuli ndio alitoa maelekezo ya kumuua Tundu Lissu lakini Mungu ni wetu sote limekufa lenyewee.
 
Huko nyuma ulianza kwa Kuwatuhumu Watu wa TISS ukatuchanganya.

Katikati tena ukaja kusema Ulishambuliwa na Askari wa Kukodi wa Rwanda.

Hukuchelewa miaka kadhaa nyuma ukiwa Ulaya ulikokaribishwa ukawatuhumu Police Tanzania.

Haya jana sijui leo nimeona Umewatuhumu Wanajeshi kwa lililokutokea.

Naanza sasa kupatwa na Wasiwasi kuwa ipo Siku utawasingizia Chama cha CCM.

Ushauri wangu Kwako kama huna uhakika au huwajui Waliokushambulia basi nyamaza tu au fanya Utafiti wako wa Kina na ukishawajua ndipo uje Kutuambia Watanzania kwani kwa sasa si tu Unatuchanganya lakini unaanza Kutuboa hata Sisi tunaokupenda na kukuunga mkono.

Sijui na Siku mfano ukija kujua kuwa Wahusika wa Shambulio lako wanatoka CHADEMA utasemaje kwani Wahenga wanasema Kikulacho Ki Nguoni mwako.
Akinyamaza mawe yatasema,aliyeamuru shambulizi haramu yuko kuzimu.
 
Huko nyuma ulianza kwa Kuwatuhumu Watu wa TISS ukatuchanganya.

Katikati tena ukaja kusema Ulishambuliwa na Askari wa Kukodi wa Rwanda...
Wewe ulishashambuliwa hata risasi moja kuujua uchungu wake ndugu kiasi cha kumshauri mhanga kunyamaza?

Kwani hawakuwepo waliopaswa kuhakikisha usalama au hata kufuatilia baada ya tukio?

Kwani wamefanya nini hata Leo hii?

Au kwako ni mkuki Kwa nguruwe tu?
 
Kwa hadhi kama ya tundu lissu kushambuliwa ina maana washambuliaji hawafahamiki? Je kama lissu angekuwa kiongozi mkuu wa serikali halafu ashambuliwe vile, hiyo operesheni kamatakamata ingezoa wengi, tena wengine kwa nyadhifa zao kwa ulinzi na usalama wangekamatwa kwa uzembe tu.

Ikumbukwe wale jamaa waliopanga jaribio la mapinduzi liloshindwa wengi walikamatwa hata kwa kuhusishwa tu na mapinduzi yale ya enzi za mwalimu.

Ishu ya lissu anawajua watesi wake, ni suala la muda tu ipo siku atawataja, kama hatawataja yeye wengine watawataja kwa namna itakavyowezekana. Hakuna unyama usiofunuliwa hata ipite miaka miaka mingi itasemwa tu
 
Back
Top Bottom