Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Nikiibiwa kura nitawaingiza Wananchi barabarani

Asante mkuu
 
Mwenzio mboe aliambiwa SIJARIBIWI akaufyata na hakupeleka watu barabarani , wewe unajiaminishaje?
 
Usisahau kuitanguliza mbele familia take,sio kuamasisha watoto wa wenzake waandamame huku wa kwake kawaficha hotelin
Kuna watu lazima watolewe sadaka
 
Hili ndilo tatizo kubwa la Tundu Lissu. Yeye siku zote huita kushindwa kutotendewa haki. Lissu ni lazima akubali kuwa kuna kushinda kihalali au kushinda kwa mbinu chafu. Pia kuna kushindwa na kushindwa kwa mbinu chafu. Ni vizuri mgombea kuweka yote bayana na siyo kufikiria kuwa kushindwa koote ni kwa mbinu cha au kushia koote ni kwa kutumia mbinu chafu.

Pamoja na Tundu Lissu kuwa mwanasiasa ambaye anakuwa na hoja kali lakini hpja zake huchafuliwa na lugha chafu, lugha yenye matusi machafu, lugha ya majigambo yanoyokosa "humility". Juzi nimemsikia akiongea juu ya sekondari za kata. Badala ya yeye kuangalia jinsi ya kuziimarisha na kuwezesha watoto wa vijijini kuingia sekondari na kupata elimu nzuri yeye ni kuzikashifu na kusema mtoto wake hawezi kwenda shule hizo. Anawasomesha watoto wake shule binafsi. Yeye akisomesha watoto wake binafsi ataona vipi adha ya shule za kata. Je yeye ana tofauti gani na viongozi wa sasa, wa nyuma, na wenyenavyo? Yaani yeye anatuambiya ni daraja la juu huku anatuomba wa daraja la chini tuwe naye, tumpe kura atitawale, watoto wake waliyosoma shule nzuri wapate urahisi kupitia kwake na watoto wa maskini wakulima na wapika gongo waendelee kusomea shule za kata ambazo hajasema atazifanyia nini! Shule za kata hata kama duni bado kila mwaka zinashindisha watoto watano au sita kwenda high school na hao si haba. Maana zingikuwepo hao wasingepatikana. Mwanasiasa mahiri ni yule atayeongelea namna ya kuziborosha na siyo kutumia udhaifu wa hizo shule kujinyakulia kura!
 
Na atapigika kweli. Watanzania wenzangu nawaomba msijaribu kuingia barabarani kitakachowakuta hamtasahau maisha yenu. Najua JF ni wabishi ila subirini tu
Kuna askari wangapi vs waathirika wa CCM negligence wangapi? Lazima askari wapige magoti!
 
Kura hazitaibiwa, figisu na dhulma wakati wake ulishapita,watanzania wenye mawazo mbadala ninyi ni ndugu zetu, mpo kisheria, mnafanya majukumu yenu kwa mujibu wa sheria, kuwa wapinzani haimaanishi mliletwa na shetani,hapana.
Utendaji kazi wetu kwa kiasi kikubwa umekuwa ukiathiriwa na wanasiasa (Chama Dola) kutokana na mfumo wa uundwaji wa taasisi yetu, rejea Sheria ya jeshi la polisi na wasaidizi wake na pia Police General Orders(PGO).

Tunashuhudia kwa kiasi kikubwa sasa idadi ya askari, wakaguzi na maafisa wakiwa wameuchoka mfumo wa kikoloni, amini nawaambia watanzania wenzetu tupo pamoja nanyi, matatizo yenu ni ya kwetu,tupo kuwalinda na kuhakikisha usalama wenu, tutazilinda kura zenu, timizeni wajibu wenu.

Tunawapenda sana watanzania.

Afande Tanzania,
Muumini wa utawala wa Sheria.
 

Labda nami nimkumbushe kuhusu mgombea mwenza wake kuwa aliwahi kugombea ubunge wa Jimbo la Kinondoni, je, anastahili nafasi hiyo kulingana na Katiba ya JMT, Ibara ya 47(3)?
 
Mapema hivyo! Hizo ni hisia tu! Wananchi wanaojitambua hawawezi kuingia barabarani.
 
Kama nimesoma vizuri kichwa cha habari ni kuwa kasema "Kama nitaibiwa kura..." na sio "Kama nikishindwa..." sasa hapa sijui nani mchochezi, Lissu au mnaotafsiri maneno yake mnavyotaka nyinyi.
Sishangai kuona Lissu ana shida kesi zote.
 
Huyu ndio anafaa kulingana na nyakati tulizonazo leo hii.
Jidanganye tu kama ulivyojidanganya kwa Lowasa. Waulizeni wapemba, Lissu kaona kawa chibanda soni peke ake anataka wawe viwete na vilema wengi. Mtapigwa virungu na hakuna wa kuwasaidia Lissu atakimbia asubuhi na mapema kwenda Ubelgiji.
 
Kuibiwa inategemea na kiasi, kuibiwa kura moja,mbili mpaka 100 kweli nikuibiwa,lakini kuibiwa kura zaidi ya milioni moja huko sikuibiwa ni kushindwa,mm naimani uchaguzi ukiwa haki na huru Lisu atashinwa kwa 80%,,Sasa huko kutakuwa kuibiwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…