Hiyo ndio Kauli ya Mh Tundu Lissu iwapo ikitokea ameshindwa kwenye uchaguzi mkuu mwezi October 2020. Ataingiza watanzania barabarani ikiwa ataibiwa kura zake.
View attachment 1526711
My take: Ni mapema Sana kwa mgombea urais kutoa kauli Kama hii si kiashiria kizuri. Anataka kutuaminisha kuwa hata ikitokea ameshindwa kihalali tuamini kuwa kaibiwa kura ili atimize azima yake.
Uongozi wa CHADEMA umshauri huyu mgombea kauli hizi hazifai kwa usalama wa nchi yetu.
Anasema akiibiwa. Atashindwa ki halali kabisa. Ni mgombea mzuri, lkn timing yake ndo ina shida. Angesubiri magufuri amalize muda wake ili aje apambane na atakaye kuja. Kwa nini magufuri?
1. Amebana wizi kwenye madini, tumeibiwa sana kapunguza. Bado kwenye dhahabu, bado ndege zinabeba na kupeleka ulaya
2. Miradi ya maji, sasa angalau anafanya. Kuna watu wako ziwani lkn hawana maji miaka 60 ya uhuru, yeye anaendelea kuyasogeza.
3. Umeme wa stiglers gorge, itakuwa historia mpya. Lissu na akina zitto wanakubaliana kuwa tunaharibu mazingira. Magufuri miaka mitano ataitumia kumaliza mradi huo.
4. Sgr ni mradi wa magufuri, pia kufufua reli na bandari zilizokufa siku nyingi. Hii ndo heshima ambayo Kenya wanajiharishia sasa
5. Kuongeza mapato ya serikali hadi trillions of money. Ndiyo maana tumeingia nchi ya kipato cha kati.
6. Seriousness katika kutatua kero halimashauri. Magufuri hana mfano
7. Kufufua shirika la ndege
8. Taasisi za kifedha kukusanya ukwasi hadi kutamani kuwekeza nchi za kibepari kama kenya ni juhudi za magufuri.
9. Daraja la kigongo Lissu anaweza likata maana atakuja na vipaumbele vyake.
10. Upinzani wote waliingia kwenye mtego wa skendo za covid, kama siyo magufuri hata mimi nilimchukia lkn ameniprove wrong. Zito na akina mbowe wangekuwa wameifunga nchi kwa hekaya za corona. Magufuri ni visionary leader maana wote waliofunga wanalazimika kufuata njia za Tanzania.
Hayo machache na mengine ni sababu za Magufuri kupewa muda zaidi ayamalizie na atunyoshee hawa wakenya.
Anayo mabaya machache lkn hayapiti mazuri aliyoyafanya kwa miaka mitano. Tumpe muda magufuri