Tundu Lissu: Niliwahi kufanya kazi katika kampuni iliyokamata ndege ya Tanzania Uholanzi. Kauli hii inakupa hisia gani?

Kwa hiyo umeshindwa kutofautisha wakati wa sasa na wakati uliopita?

Ameeleza wazi kuwa aliwahi, siyo kuwa anafanya kwa sasa.

Hata hivyo, Tundu Lissu ndiye aliyeshurutisha mikataba ivunjwe kwa nguvu?

Shida ya tundu ni kuwa anaonekana kuburudishwa na namna anbavyo nchi yetu inavyopewa kibano. Halafu hata siku moja haoneshi kushauri kama kuna remedy yoyote, licha ya kuwa kuna makosa yalifanyika. Sasa sisi wazalendo wa kweli na wafia nchi tunaumia. Nchi inauma bro wee acha tu.

Halafu yee lisu anashangilia, ndiyo maana machungu yanatupanda.
 
Kwenye bilioni 380 ana mgao wake kama wa bilioni kumi, anategeshea tu serikali ilipe achukue chake mapema
 



..tatizo la baadhi ya wazalendo ni kushindwa kutofautisha watawala na nchi, au serikali na nchi.

..Lissu alitahadharisha kuhusu uvunjaji mikataba kiholela. Kwamba tutaburuzwa mahakamani na kushindwa na kuingia hasara kubwa.

..Baadhi ya mawaziri kama Dr.Mwakyembe, na Dr.Kabudi, wakawa wanamkejeli kwamba Tz haiigopi kushtakiwa.

..Tunapaswa kuilaumu serikali. At least tuwalaani mawaziri na wanasheria wakuu ambao uongozi, maamuzi, na ushauri wao, imeiiingiza nchi katika hasara kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…