Tundu Lissu: Niliwahi kufanya kazi katika kampuni iliyokamata ndege ya Tanzania Uholanzi. Kauli hii inakupa hisia gani?

Tundu Lissu: Niliwahi kufanya kazi katika kampuni iliyokamata ndege ya Tanzania Uholanzi. Kauli hii inakupa hisia gani?

Kwa hiyo umeshindwa kutofautisha wakati wa sasa na wakati uliopita?

Ameeleza wazi kuwa aliwahi, siyo kuwa anafanya kwa sasa.

Hata hivyo, Tundu Lissu ndiye aliyeshurutisha mikataba ivunjwe kwa nguvu?

Shida ya tundu ni kuwa anaonekana kuburudishwa na namna anbavyo nchi yetu inavyopewa kibano. Halafu hata siku moja haoneshi kushauri kama kuna remedy yoyote, licha ya kuwa kuna makosa yalifanyika. Sasa sisi wazalendo wa kweli na wafia nchi tunaumia. Nchi inauma bro wee acha tu.

Halafu yee lisu anashangilia, ndiyo maana machungu yanatupanda.
 
..Lissu amefunguliwa makesi mengi sana hapa Tanzania.

..Wameanza kumfungulia makesi tangu miaka ya 90.

..Kama angekuwa msaliti, au ana fanana na tuhuma hizo, watawala [ mkapa, kikwete,magufuli ] wangemfungulia kesi hiyo, au inayokaribiana na hiyo.

..Hii habari ya kumuita msaliti bila ya kumfikisha mahakamani ni jitihada za kumchafua na kumbomoa Lissu ili asiaminike na wananchi. Hiyo ni mbinu ambayo imetumika dhidi ya wanasiasa wengi waliokuwa mwiba kwa serikali.
Kwenye bilioni 380 ana mgao wake kama wa bilioni kumi, anategeshea tu serikali ilipe achukue chake mapema
 
Shida ya tundu ni kuwa anaonekana kuburudishwa na namna anbavyo nchi yetu inavyopewa kibano. Halafu hata siku moja haoneshi kushauri kama kuna remedy yoyote, licha ya kuwa kuna makosa yalifanyika. Sasa sisi wazalendo wa kweli na wafia nchi tunaumia. Nchi inauma bro wee acha tu.

Halafu yee lisu anashangilia, ndiyo maana machungu yanatupanda.

..tatizo la baadhi ya wazalendo ni kushindwa kutofautisha watawala na nchi, au serikali na nchi.

..Lissu alitahadharisha kuhusu uvunjaji mikataba kiholela. Kwamba tutaburuzwa mahakamani na kushindwa na kuingia hasara kubwa.

..Baadhi ya mawaziri kama Dr.Mwakyembe, na Dr.Kabudi, wakawa wanamkejeli kwamba Tz haiigopi kushtakiwa.

..Tunapaswa kuilaumu serikali. At least tuwalaani mawaziri na wanasheria wakuu ambao uongozi, maamuzi, na ushauri wao, imeiiingiza nchi katika hasara kubwa.
 
Back
Top Bottom