Pre GE2025 Tundu Lissu: Nimewasilisha kusudio la kugombea nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA

Pre GE2025 Tundu Lissu: Nimewasilisha kusudio la kugombea nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hilo la fedha ya chama kupelekwa ngazi za chini safi sana.na huko chini ndiko kwenye kazi sio huko juu kwenye matamko tu
 
Baada ya Miaka 20, Lissu Atangaza Nia ya Kumng'oa Mbowe

Katika kile kinachoonekana kama hatua ya kihistoria ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu leo, Alhamisi, Disemba 12, 2024, ametangaza rasmi azma yake ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho, nafasi ambayo imekuwa ikishikiliwa na Freeman Mbowe kwa zaidi ya miongo miwili.

Lissu, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), alitoa tamko hilo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Mlimani City, jijini Dar es Salaam. Alisema kuwa muda wa mabadiliko umefika na kwamba chama kinahitaji uongozi mpya wenye maono mapya ili kukabiliana na changamoto za kisiasa nchini.

"Mbowe amekuwa Mwenyekiti wa Chadema kwa miaka 20, na wakati wa uongozi wake tumepata mafanikio mengi. Hata hivyo, sasa ni wakati wa damu mpya kuleta mwelekeo mpya. Nafasi hii si miliki ya mtu mmoja, bali ni jukumu la kila mwanachama mwenye uwezo na nia ya dhati ya kukitumikia chama," alisema Lissu kwa msisitizo.

Akifafanua zaidi, Lissu alisema kuwa chama kimepoteza baadhi ya fursa muhimu kwa sababu ya kile alichokiita "mtindo wa uongozi wa mtu mmoja." Alisema kuwa mabadiliko ya uongozi ni sehemu ya demokrasia na yanahitajika ili kuimarisha umoja na mshikamano wa wanachama.

Freeman Mbowe, ambaye amekuwa kwenye uongozi wa Chadema tangu mwaka 2004, bado hajatoa tamko rasmi kuhusu hatua ya Lissu. Hata hivyo, wachambuzi wa siasa wanaona kuwa uamuzi huu wa Lissu unaweza kugawanya wanachama wa Chadema kati ya wale wanaomuunga mkono Mbowe na wale wanaotaka mabadiliko.

Huku uchaguzi wa ndani wa Chadema ukitarajiwa kufanyika mapema mwaka ujao, hatua hii ya Lissu imezua mjadala mpana kuhusu mustakabali wa chama hicho kikuu cha upinzani, hasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Je, Lissu ataweza kumng'oa Mbowe na kuleta mabadiliko anayoahidi? Wanachama na wafuasi wa Chadema wanasubiri kwa hamu kuona matokeo ya kinyang'anyiro hiki cha uongozi.
 
Attachments

  • IMG-20241212-WA0060.jpg
    IMG-20241212-WA0060.jpg
    127.7 KB · Views: 1
He is dong worse in politics coz there is a saying that if you do good in class, you are likely to do good also in all aspects. The fact that Lisu did bad in class, there is no miracle for him to do good in politics. These things are sequencial and simultaneous
Resistance to change
 
Sasa ndio kifo cha chadema kinakuja

Because, utawala hauwezi kukubali lissu awe mwenyekiti

Na lisu akikosa hiyo nafasi lazima ataondoka chadema kwenda kuanzisha Chama kingine au ataenda Kwa Zitto
Au ataanzisha chama chake: Chama cha Catiba na Maendeleo (CCM).
 
CCM wanajaribu kila namna kuokoteza matukio ili mradi tu Chadema kionekane kina vurumai,Mbowe aliwajibu juzi kuwa mambo ya ndani ya CHADEMA yanawahusu nini?
 
Nawashukuruni wote kwa kuitikia wito wangu wa kuwa pamoja nami katika siku hii ya leo.

Tundu A.M. Lissu MTIA NIA
He is the ONE for CHADEMA and for Tanzania at this time.

Muda ni mfupi sana kurekebisha yote haya na kumkabiri Bi. Chura Kiziwi.
 
He is dong worse in politics coz there is a saying that if you do good in class, you are likely to do good also in all aspects. The fact that Lisu did bad in class, there is no miracle for him to do good in politics. These things are sequencial and simultaneous
As if you know anything about what you're writing about; which is totally nonsense!
 
Mimi na Wewe anayeteseka ni nani? 😂

Nimekumbusha tu hata Mchungaji Msigwa alianzaga na vipress hivi hivi
Sijui kwa nini unahangaika sana namna hii siku hizi, hata aibu huna!
Kama kawaida yako, badala ya kuchambua yaliyo semwa na Tundu Lissu, ujuzi wako unaishia kwenye kuingiza vihabari ambavyo ni nje kabisa ya mjadala husika.

Hii ndiyo sifa pekee inayo kupambanua humu JF kwa muda mrefu.

Umesikiliza au umesoma hayo aliyo wasilisha Tundu Lissu hapo juu? Kwa nini usichukue muda kuyachambua hayo tujue uelewa wako ni upi juu yake?
 
Sijui kwa nini unahangaika sana namna hii siku hizi, hata aibu huna!
Kama kawaida yako, badala ya kuchambua yaliyo semwa na Tundu Lissu, ujuzi wako unaishia kwenye kuingiza vihabari ambavyo ni nje kabisa ya mjadala husika.

Hii ndiyo sifa pekee inayo kupambanua humu JF kwa muda mrefu.
We pimbi kweli hii comment ni Baada ya Mwenyekit Lisu kuongea Mlimani City?

Bure kabisa wewe
 
To be honest....... namuheshimu sana Tundu Lissu lakini binafsi Lissu anafaa zaidi kwenye nafasi ya utendaji na si kuwa kiongozi top........ issues kama decision making naona ni mtu ambaye hana utulivu sana kuongoza taasisi kama chama kwasababu hana breki.Mimi Tundu huwa namaanisha na JPM kwenye baadhi ya mambo (naweza kukosolewa pia).Kuwa mbeba maoni wa taasisi si jambo dogo,na wengi huwa wanamlaumu lakini namna Freeman anavyotumia busara kuifikisha chadema hapa,anapaswa kutoonekana mjinga, binafsi namuona Lissu akiwa chini ya mtu anakuwa mtu bora zaidi.. Ningekuwa mshauri wa Mbowe ningemuomba apumzike asigombee kabisa kwasababu legacy yake ni kubwa
 
Okay, sijaona komenti baada..., ipo wapi?
Mimi nimeongea na Nyalusi Boss wa Chadema Iringa mjini kwa Simu na nimempa Pongezi zangu aziwasilishe kwa Mwenyekiti Mpya mh Tundu Lisu

Hapa JF Uzi ulivyofunguliwa wa Press mubashara sijaondoka hadi Press ilivyoisha 😂😂😂
 
Mkuu 'John' tutakwenda taratibu hivyo hivyo, mradi tu tufike salama na Tanzania yetu hii. Hili ndilo la muhimu kuliko yote.
CCM ni chama tu, sote kwa nyakati tofauti tuli kipenda chama hicho..., lakini haturuhusu hilo ndilo liwe mzigo wa Tanzania nzima na wananchi wake daima.
 
DAA LKN yote na yote Mbowe anastaili sifa na Kueshimiwa na LiSU pamoja na yote Pamoja na LiSU kusema anatembea na chuma mgongoni kweli LiSU kapitia Mengi ka88ima Binadam nikijivalisha ULisu apana jamaaa ni mwamba sio Wakitoto Lkn Tukuoombuke pia MBOWE alijitolea kumpambania LISU kishujaaa kias cha kuatarisha maisha yake MBOWE wengi awajui vuzuli au awataki kusema Ukweli huu ile ndege iliom'beba ndugu LiSU ilik
 
To be honest....... namuheshimu sana Tundu Lissu lakini binafsi Lissu anafaa zaidi kwenye nafasi ya utendaji na si kuwa kiongozi top........ issues kama decision making naona ni mtu ambaye hana utulivu sana kuongoza taasisi kama chama kwasababu hana breki.Mimi Tundu huwa namaanisha na JPM kwenye baadhi ya mambo (naweza kukosolewa pia).Kuwa mbeba maoni wa taasisi si jambo dogo,na wengi huwa wanamlaumu lakini namna Freeman anavyotumia busara kuifikisha chadema hapa,anapaswa kutoonekana mjinga, binafsi namuona Lissu akiwa chini ya mtu anakuwa mtu bora zaidi.. Ningekuwa mshauri wa Mbowe ningemuomba apumzike asigombee kabisa kwasababu legacy yake ni kubwa
Nipe maono mawili tu ya Samia Suluhu Hassan.
Kwa nini umfananishe Tundu Lissu na Magufuli; hata 'intellectually' watu wasio fanana kwa lolote? "Busara"?

Ushauri wako kwa Mbowe ni mzuri. Hiyo "Busara" kwa CCM ya Samia haina lolote la maana.
 
Back
Top Bottom