Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa

Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa

Hivi unataka majibu au una lako jambo? Lissu hakuwa Wakili wa Barrick. Kwanza alikuwa akitaka kumwakilisha yule Mwanyika wa Acacia aliyewekwa ndani kwa uhujumu uchumi na madai ya acacia kukwepa kodi na kwamba ni kampuni ambayo haikusajiliwa.
Unajielewa kweli ama umeamua kuandika tu. Kwa nini atake kuwakalisha wahujumu uchumi wakati yeye alikuwa muwakilishi wa wananchi tayari? Aliacha kazi za kibunge na kufanya za kilaghai?
 
Hili swali ni gumu mno kwa cdm. Utaambulia matusi na kejeli lakini wa kukujibu hakuna.
Lissu alikua anatumiwa na mabeberu na pale alikua kazini kuwatetea mabeberu harafu leo anautaka urais. Nitapiga kampeni chumba kwa chumba kumtetea Magufuli.
Hadi sasa sioni jibu. Wakishindwa wakamulize waniletee.
 
La muhimu gani magufuli alilofanya wewe uvccm, yaani kuzuia makapi ya makinikia huku wazungu wakiendelea kujibebea dhahabu pure ndo ushujaa?
Huwa napenda jibu la moja kwa moja.

Magufuli kafanya mengi sana katika taifa hili. Baada ya 2025 utamkumbuka.
 
Naomba majibu ya hili swali Hadi leo sijapata.

Kwa nini Lissu alikiwa anawetetea Sana Barick na kutishia kwamba tutashitakiwa? Alikuwa na nia ya dhati kweli ama alikiwa anatetea ulaji wake tu? Ama ilikuwa sehemu ya Siasa kwamba ukiwa upinzani lazima upinge kila Jambo?

Nikijibiwa nikaelewa basi kura yangu kwake.

Hujapata jibu kwasababu hakuna ushahidi wala record ya Lissu kutetea Barricks na ndiyo maana hujibiwi.

Lissu kabla hata ya kuwa mbunge alikuwa wakili wa kutetea haki za wananchi wanaokaa kwenye machimbo miaka ya Uraia wa Mkapa kaulize watu kule Musoma na Mwanza. Hivyo sio tu alikuwa hawa tetei Barricks lakini alikuwa anawatetea wananchi kiasi kwamba alifunguliwa kesi wakati wa Mkapa! Sasa sijui wewe unatumia nini mpaka kichwa chako kiwe kizito hivyo
 
Yale makontena aliyozuia pale bandarini atayaachia na mbaya zaidi atalipia fidia kwa fedha za walipa kodi ambao wana lundo la makodi. Tutaacha kusonga mbele na kujikuta tunarudi nyuma kulipia nothing. Huu ni ukweli japo ni mchungu sana! Uzalendo wa kweli kamwe hauambatani na faraja ya muda mfupi inayozaa msiba baadaye.

Nasisitiza kuwa tunaibiwa kwenye mikataba yetu tuliyosainiwa na miccm. Huko kwingine Magufuli anapiga tu maneno.
Sijui kama bado unasoma huu utopolo wako.
 
Hujapata jibu kwasababu hakuna ushahidi wala record ya Lissu kutetea Barricks na ndiyo maana hujibiwi.

Lissu kabla hata ya kuwa mbunge alikuwa wakili wa kutetea haki za wananchi wanaokaa kwenye machimbo miaka ya Uraia wa Mkapa kaulize watu kule Musoma na Mwanza. Hivyo sio tu alikuwa hawa tetei Barricks lakini alikuwa anawatetea wananchi kiasi kwamba alifunguliwa kesi wakati wa Mkapa! Sasa sijui wewe unatumia nini mpaka kichwa chako kiwe kizito hivyo
Umekuwa mwepesi wa kusahau sana. Tutakukumbusha kama utataka.
 
La muhimu gani magufuli alilofanya wewe uvccm, yaani kuzuia makapi ya makinikia huku wazungu wakiendelea kujibebea dhahabu pure ndo ushujaa?
Sasa ulitaka wabebe dhahabu bandia! Wamewekeza ili wasibebe chochote?
 
Leo Magufuli anajifanya mzalendo na anahoji uzalendo we yeyote anayepingana nae.
Ni muongo. Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata. Kwa siku chache tu. Mark my words: ataumbuka na mtaumbuka.

#NIYEYE #LISSURAIS2020. ✌🏽✌🏽
 
Leo Magufuli anajifanya mzalendo na anahoji uzalendo we yeyote anayepingana nae.
Ni muongo. Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata. Kwa siku chache tu. Mark my words: ataumbuka na mtaumbuka.

#NIYEYE #LISSURAIS2020. [emoji1422][emoji1422]
Uzalendo wa mtu ni yule anayeweza kuwapenda hata maadui zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukitukana haisaidii
Kusema mtu anawaza kama "nyumbu" ni tusi na sio fact kwamba haijawahi kuwa mwanasheria wao? Kwani alichokuwa anaongea hadharani kuwatete alikuwa anafanya hivyo kama Mwanasheria wao au mwanasiasa, naomba unieleweshe inawezekana in this instance Mimi nimefikiria au kuandika kama "nyumbu"
 
Anaandika Lissu:

Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii: Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya tangu mwaka '99.

Wakati huo tulikuwa na mgodi mmoja tu wa dhahabu, Resolute Golden Pride Nzega. Bulyanhulu ilikuwa haijajengwa. Geita ndio kwanza walikuwa wanafukuza wanakijiji wa Mtakuja.

Nadhani nilikuwa wa kwanza katika nchi hii kupiga yowe kwamba tutaibiwa sana kwenye sekta ya madini.

Wewe sijui ulikuwa wapi wakati huo. Najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa MaCCM na wawekezaji hawa.

Nimepigana na wawekezaji hawa mahakamani, kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 15. Nimetetea wananchi completely free of charge Bulyanhulu, Tarime, Nzega, Geita, n.k.

Sijui wewe ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa upande wa nani: wa MaCCM na wanyonyaji hawa.

Soma Rai ya tarehe 17 Julai, 2001, uone tulimwambia nini Mkapa siku anaenda kuzindua Mgodi wa Bulyanhulu.

Sijui ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa wapi: alikuwa anatetea tumbo lake na matumbo ya wanyonyaji hawa.

Nilikamatwa na kushtakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya Bulyanhulu. Hiyo ilikuwa December 2002. Nilikaa na kesi hiyo mahakamani Kisutu kwa miaka sita.

Sijui ulikuwa wapi ila najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa watesi wa wananchi na wanyonyaji wa rasilmali zetu.

Leo Magufuli anajifanya mzalendo na anahoji uzalendo we yeyote anayepingana nae.

Ni muongo. Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata. Kwa siku chache tu. Mark my words: ataumbuka na mtaumbuka.

Mimi ninampinga hadharani. Sio mnafiki, na sijahongwa. Ninampinga kwa sababu atatusababishia matatizo makubwa zaidi kuliko tuliyonayo sasa.

Huo mchanga atauachia upelekwe ambako umepelekwa kwa miaka 16 iliyopita. Kama sheria ndiyo hiyo na mikataba ndiyo hiyo hana pakwenda.

Tatizo ninaloliona ni kwamba by the time anawarudishia mchanga wao, Tanzania itakuwa imekuwa a basket case kama Zimbabwe.

Na tutakuwa tumelipishwa mapesa mengi kama fidia na arbitral tribunals za kimataifa kwa kuvunja mikataba na wawekezaji hawa.

Kama kuna anayefikiri uzalendo ni kufumbia macho masuala haya basi huyo na amuunge mkono Magufuli kwenye upofu wake wa kujitakia.

Ripoti ya Prof. Mruma haitamaliza hata nusu saa under serious scrutiny. Zaidi ya majina ya maprofesa walioiandaa, ripoti hii haina credibility yoyote. Ni kazi ya kisiasa iliyopakwa rangi ya usomi.

Kama umefuatilia taarifa za kitaalamu za Bulyanhulu hata kabla ya Barrick Gold kuingia mwaka '99 utajua ninasema nini.

Sutton Resources, Outukumpu Oy na hata STAMICO walishafanya utafiti mkubwa juu ya utajiri wa Bulyanhulu. Taarifa zipo na zimekuwepo kwa hata mbumbumbu wa jiolojia ya madini kama mimi.

Hiki alichoambiwa Magufuli ni rubbish, hata kama ni ya kiprofesa. Rubbish. Hatuibiwi kwenye mchanga, that's the rubbish fed on the unlettered.

Tunaibiwa kwenye sheria. Kama hamuoni hilo then God have mercy on us.
Hivi siku hizi tumekuwa kama Zimbabwe?? Alitabiri mwanaharakati Moja
 
Mbona mambo ya Lisu yamekua sana mbele kuliko ya Magufuli yani mi hadi natamani ni vunje cm nyie mataga si mlisema Magu aliwin over Barric sa mbona mnatia tia huruma tena mbona mna tia aibu yaani ukifungua jf kila mda ni Lisu hivi mara Lisu vile hebu na nyie jiongezeni bhana.
Lisu ni nyoka na nyoka hana rafiki, ni mwendo wa kumbonda kichwa tu mpaka achakae
Yeye anajiona bi bora kuzidi watu wengine?
Anataka muungano na zito sasa yeye ajishushe amsapoti membe basi, kwani ni.lazima awe yeye?
 
Sasa ulitaka wabebe dhahabu bandia! Wamewekeza ili wasibebe chochote?
Ndo naonyesha upumbavu wa babu yenu hayo makapi aliyozuia pale bandarini alisema yana dhahabu nyingi wanatorosha hao BARICK, ndo sasa nasema kama lengo lilkuwa kuzuia dhahabu babu yenu kachemka make dhahabu zinaijiwa na ndege palepale mgodini, umeelewa sasa uvccm?
 
Duuh, asante kwa kuufukunyua uzi huu...

Unatukumbusha mbali sana na habari mbaya kumhusu kamanda wa mapambano haya, Tundu Lissu...

Hili andiko aliliandika miezi mitatu kabla hawajamgaragaza kwa bunduki za kivita za SMG na AK47 kama wanapiga tembo vile....

Duuh, Magufuli is a beast and a murderer. He doesn't deserve any respect until he repents his all atrocities he commited....
 
Back
Top Bottom