Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Nitalipa malimbikizo ya wafanyakazi yote kuanzia 2015 - 2020

Mlizoea kupiga pesa za serikali mamfikili ninyi ndo wajanja sana?
Sisi tunatozwa kodi kwa ajili ya maendeleo lakini nyie binafsi ndo mnaendelea wananchi tunabaki na shida.
Jengeni nchi kwanza
Tazama ulivyo na wivu wa kike, sasa sheria zilitungwa kwanini?
Hapa tunazungumza stahiki za kisheria, zilizoidhinishwa na kutekelezwa kwa miaka yote isipokuwa awamu hii

Hapo unajijuta kufurahia wenzako kukomolewa, wakulima wa korosho nao walizoea kupiga nini?
 
Kama mnajua ni za lazima mbona hamjaenda mahakamani?
 
Hayo yote ni kutaka kuonekana kwamba amesema kitu. Wote tunafahamu kabla ya 2015 wafanyakazi wa serikali walikuwa wanakaa miezi bila kulipwa mshahara. Siyo kwamba mshahara umecheleweshwa bali hulipwi kabisa kwa miezi kadhaa. Waalimu walikuwa kati ya waathirika wakuu. JPM alipoingia madarakani alikomesha hilo, akalipa malimbikizo yote ya wafanyakazi waliokuwa hawajalipwa, na hivi sasa mfanyakazi wa UMMA analipwa siku husika bila kucheleweshwa. Ni wazi hii ilikuwa kazi nzito na mtu mwenye akili timamu hatashindwa kuelewa kusuasua kwa upandaji wa vyeo. Si hivyo tu; elimu imekuwa bure mpaka Kidato cha Nne. Hilo nalo ni gharama kwa serikali. Kuzungumzia kupanda cheo baada ya kuona yaliyofanyika kuhusu watumishi wa Umma ni ubinafsi.

Kuhusu kulipa fidia kwa waliofukuzwa kazi, haiingii maanani. Unafukuzwa kazi kwa kuwa ni mhalifu na kuna sheria zinazo elekeza jinsi ya kufanya hilo.. Sasa unataka kiki kwa wahalifu? Kama kuna aliyeonewa kwa kufukuzwa isivyo kihalali, hilo ni jambo jingine ambalo mhusika anapaswa kwenda kwenye Mahakama ya Kazi. Tusitafute kiki kwa wahalifu.
 
CCM wamepiga pesa za SGR mpaka ujenzi unanda kusimama huku CAG hajawahi kukagua mahesabu ya CCM maana yamejaa wizi mwingi itokee siku apite huko wataenda kukanatwa mpaka wastaafu akina kinana makamba Nape na wenzao.
 
Tuliza kichwa, Chato ni tanzania.
Unaweza kutembea bila bughudha huko chato na sio kwa mabeberu
CCM wakienda ulaya kuomba omba misaada huwaita wazungu wafadhili wahisani lakini hao hao wazungu wakikataa Upumbavu wa CCM hugeuka na kuwaita wanaume wenzenu mabeberu
 
Story ndefu isiyo na point hata moja inaelekea wewe ni mnufaika wa mfumo kandamizi ndiyo maana umejitoa fahamu kutetea udhalimu wa Serikali yako ya kishetani kidikteta na uonevu.
 
Na wewe unajiona umeongea point hatari?
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]

Kabla ya 2015 hakuna mtu alikuwa halipwi mshahara wake, hakuna!
Mzee JK pamoja na madhaifu yake machache, lakini HAKUWAHI kuwa katili kwa viwango vya baada ya 2015!

Mzee wangu amestaafu tangu mwaka Jana August 2, mpaka leo bado hajapewa pesa zake, afu unakuja kuropoka ropoka hapa!
 
Shituka Kataa Kudanganywa!
Your browser is not able to display this video.
 
Sasa Takukuru Uhamiaji wameungana na Polisi kuwabambikia kesi wapinzani ili wagombea wa CCM wapate njia za kujitangaza kuwa wamepita bila kupingwa , ni style mpya ya kishetani na haramu, CCM ni ile ile
 
Tatizo la CCM wamempa Tenda cyprian Musiba na Le mutuz kuandaa watetezi wao Mitandaoni ambao kwa 99% wanakaririshwa ufala wa cyprian Musiba ndiyo maana utetezi wa CCM mitandaoni hufanana.
 
Shituka Kataa Kudanganywa
View attachment 1554022
a!
Maendeleo siyo Hisani za CCM maendeleo siyo pesa binafsi tokea mfukoni wa mtukufu malaika tokea chato, maendeleo ni pesa za watanzania wasio na vyama na watanzania wasio wapenzi wa CCM, pesa ya walipa kodi inafujwa na CCM kupitia ufisadi mwingi kwenye miradi wakati CCM wengi siyo walipa kodi.
 
Wewe acha uongo malimbikizo gani Magufuli alikuta hayajalipwa na yeye kuyalipa?

Mnafawafanya watu wote ni wapumbavu?
 
Sasa hapa ndio tusikie sera ambazo zinamgusa mwananchi na uchumi wake

Lissu amefanya vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…