Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Nitalipa malimbikizo ya wafanyakazi yote kuanzia 2015 - 2020

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Nitalipa malimbikizo ya wafanyakazi yote kuanzia 2015 - 2020

Mtu alie ajiliwa mwisho wa mwezi anakinga mikono tu. Hivi vitu hawezi kuvielewa. Ila wanakuja kuona tofauti ya maisha yao na yetu.. na wanaishia kusema tunatoa watu kafara
Ndiyo hapo na unakuta kipato Cha mtu aliyejiajiri ni kikubwa kuliko Cha mwajiriwa ,, Wengi wanasubiri wastaff ndiyo wafanye maendeleo ila saizi watakuambia salary ndogo mara makato Mara sijui nn Yani balaa tupu
 
Pole sana kamanda naelewa kama mzaliwa wa family ya biashara, mhanga wa VAT ya Mkapa usipime, tulivuka kwa neema ya Mungu tu
Acha kabisa, ndugu yangu. VAT si rafiki hata kidogo, bado witholding tax, wanayo kata juu kwa juu unakuta wanalala mbele na zaidi ya 23%... bado na taka taka zingine.. kodi zimekuwa nyingi sana kwetu wafanya biashara hadi tunabuni mbinu za kuwa tunazikwepa, maana ukienda nao fair hutokaa utoke
 
Kwa hiyo hata waliofanya kosa la jinai kufoji vyeti atawalipa fidia! Ina maana anahamasisha watu kufoji vyeti! Huyu anastahili uraisi?

Wapi aliposema atalipa waliofoji vyeti? Na hata akiwalipa kuna kosa gani? Kwa maana mtu hulipwa kwa kazi alioifanya na sio vyeti. Kutokumlipa mtu stahili yake kwa kazi alioifanya ni wizi. Anaefanya kazi ni MTU na sio cheti.
 
Mungu akubariki TL..hoja nzito sana hizi.

Mtu kafanya kazi miaka 30...ananyimwa mafao na mshahara ulikuwa wakatwa kodi..
Hivi kweli!?
Tundu Lissu anasema atalipa malimbikizo yote ya mishahara na kupandisha vyeo vyote vilivyosimama toka mwaka 2015 mpaka leo 2020.

Anasema lazima wafanyakazi walipwe fidia na Serikali yake.

Anasema atawalipa pia fidia wote waliofukuzwa kazi na Serikali ya CCM ndani ya hii miaka 5.

Anasema atarudisha makato ya loan board kutoka 15% na kuwa 3%

Na yatakuwa kwa wale tu watakao kuwa na kazi za kueleweka ndani ya serikali yake.

Anasema atafumua mfumo wa elimu ili utoke kwenye kujibu mithihani na kuwa elimu ya maarifa na kujitegemea na kuajirika kirahisi.

Anasema ataifumua TRA na kuanzisha mfumo wa Kodi moja ili nchi zote zilizo tuzunguka zije kununua bidhaa bandarini na kwenye maduka yetu ya ndani.

View attachment 1552154View attachment 1552155
 
CHADEMA hawakua tayari kwa kampeni. Natabiri yaliyotokea 2015 kwa Lowasa yatokea 2020 tofauti itakua tu kwamba 2015 Lowasa hakuna nguvu ila 2020 Lissu pesa zitakata

Sasa nadhani ni kweli Lisu anahujumiwa kwa kunyimwa hela za campaign ni aibu chama kikubwa kama CHADEMA kutembeza bakuri wakati wa kampeni bora hata wangefanya kabla sijui hela za michango toka kwa wabunge, hela za michango ya wanachama na hela ya ruzuku na hela za misaada toka kwa wahisani zinaendaga wapi. Wangeanza kuwekeza kidogo kidogo kila mwezi leo wangekua hawaangaiki Na serikali kama ilishtuka vile wakapiga pini accounts za kituo cha haki za binadamu maana huko ndio zingepitia.
Kwa ushauri wangu tu CHADEMA bora waanze jiandaa kwa uchaguzi wa 2025 mapema waanze jenga ofisi zao nzuri tu kubwa ambazo wanaweza pangisha watu kama wafanyavyo ccm wanavopata hela toka kwenye majengo yao. Pia CHADEMA ina wafuasi wengi na very royal kiais kwamba CHADEMA inaweza wekeza kwenye miradi mbalimbalia na wakapata wateja mfano kilimo ufugaji etc imagine mnaanzisha hata kiwanda cha maji cheye sticker za CHADEMa au maziwa yenye label ya CHADEMA watu watanunua na mtapata hela nzuri tu.

Kwa mwendo wa sahivi Raia watawadharau sababu kama mnashindwa manage funds zenu ndani ya chama na kuomba michango wakati nyie ndio chama kikuu cha siasa mkipewa nchi si kodi ya kichwa itarudi
Dah......CHADEMA walikuwa na wabunge zaidi ya 30 bunge lililopita.......na kila mmoja kalipa Zaidi ya milioni 200 za kitanzania kama kiinua mgongo..ambayo kwa wote ni kama 6.8 billioni....na kila mwezi walivuna Zaidi ya milioni 12 shilingi za kitanzania ambayo inafanya jumla ya 24 billion za kibongo......ukiongeza na ruzuku ya 329m kwa mwezi ambayo inakwenda kuwa shillingi 20b....hivyo jumla ya pesa waliyoingiza Chadema na wafaidika wake ni shilling za kitanzania Bilioni 52 .... halafu leo mnakuja kusema chama hakina pesa.. eti tuwachangie...mburaaaaa...tuwachangie sisi wakati Bilioni 52 zimeliwa na watu wasiozidi 100 ... ndiyo mpewe hazina kweli? ...Dah 😳
 
Ahadi hewa kwa wajinga,ni furaha na vigeregere
Tundu Lissu anasema atalipa malimbikizo yote ya mishahara na kupandisha vyeo vyote vilivyosimama toka mwaka 2015 mpaka leo 2020.

Anasema lazima wafanyakazi walipwe fidia na Serikali yake.

Anasema atawalipa pia fidia wote waliofukuzwa kazi na Serikali ya CCM ndani ya hii miaka 5.

Anasema atarudisha makato ya loan board kutoka 15% na kuwa 3%

Na yatakuwa kwa wale tu watakao kuwa na kazi za kueleweka ndani ya serikali yake.

Anasema atafumua mfumo wa elimu ili utoke kwenye kujibu mithihani na kuwa elimu ya maarifa na kujitegemea na kuajirika kirahisi.

Anasema ataifumua TRA na kuanzisha mfumo wa Kodi moja ili nchi zote zilizo tuzunguka zije kununua bidhaa bandarini na kwenye maduka yetu ya ndani.

View attachment 1552154View attachment 1552155
 
Kama hela ya kampeni tu una pitisha bakuli kwenye mikutano sasa hela ya kuwa lipa wafanyakazi utaitoa wapi? Au ndio mipango yako mibaya ya kuja kutumia hela aliyo kusanya Magufuli???

Wewe kibaraka wa JOE TRIPPI huko unapo taka kutupeleka tumepashtukia
 
Atatumia hela za walipa kodi saivi hakusanyi kodi!!

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
Hahahaaa malimbikizo gani wakati rais amesema ameshalipa hayo madeni kwa wafanyakazi?
Au anadhani hii ni 2015?
Wewe "umesikia" amelipa malimbikizo yote, lakini tulio ndani ya kibuyu tunajua kiasi gani tunanyanyaswa na kudhulumiwa kwa miaka yote mitano!
 
Wewe "umesikia" amelipa malimbikizo yote, lakini tulio ndani ya kibuyu tunajua kiasi gani tunanyanyaswa na kudhulumiwa kwa miaka yote mitano!
Mlizoea kupiga pesa za serikali mamfikili ninyi ndo wajanja sana?
Sisi tunatozwa kodi kwa ajili ya maendeleo lakini nyie binafsi ndo mnaendelea wananchi tunabaki na shida.
Jengeni nchi kwanza
 
Uza nchi yako, Chagua Lissu
Nchi ilishauzwa chato kwani wamechukua pesa zote Hazina wamepeleka Chato na kwenye kampeni, SGR mwezi wa nne hawajalipwa ujenzi unasuasua mda wowote wafanyakazi watagoma
 
Nchi ilishauzwa chato kwani wamechukua pesa zote Hazina wamepeleka Chato na kwenye kampeni, SGR mwezi wa nne hawajalipwa ujenzi unasuasua mda wowote wafanyakazi watagoma
Tuliza kichwa, Chato ni tanzania.
Unaweza kutembea bila bughudha huko chato na sio kwa mabeberu
 
Back
Top Bottom