Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Yericko Nyerere ametoa tuhuma kuwa Dola na CCM wanaingilia uchaguzi na wanamtaka Lissu kwa nguvu.
Wamejificha weeee hatimaye wamejitokeza hadharani!
Halafu mwanachama halisi anainuka anasema Lissu anafaa kuwa mwenyekiti bila kujua nyuma yake kuna agenda gani? Wajumbe wa Mkutano Mkuu msifanye makosa yatakayokigharimu Chama chetu!
Dola na CCM yake wanaingilia uchaguzi wanamtaka Lissu kwa nguvu kubwa wametoa pesa na wanafanya kampeni za Wazi kabisa, Malengo yao ni kuwa Lissu ni mropokaji tu asiyeweza kuongoza taasisi ya Kisiasa inayohitaji hekima, busara na USIRI mkubwa, Kwamba Lissu hana uwezo wa kutafuta pesa ya kuendeshea chama, Kwamba Lissu akiwa Mwenyekiti hakuna Taasisi wala Watu wa Heshima nchini na nje ya Nchi watakaoshirikiana na Chadema kwakuwa Mwenyekiti wake Lissu HANA SIRI, ni Mropokaji kwa chochote watakachoshirikiana nae! Na hivyo Chama kitamfia ndani ya miezi michache tu baada ya kuchaguliwa na CCM itabaki salama dhidi ya Chadema ya Lissu.
CCM inaamini akina Lema ni wahuni tu wasioweza hata kujitafutia pesa ya kulisha familia zao badala yake wao na Familia zao wanalishwa na Serikali za Canada na Ubelgiji kama wakimbizi wa Kisiasa. Kwavyovyote vile, hawawezi kuongoza chama cha siasa Tanzania ambacho kukiongoza unatakiwa kuwa na Maarifa, misuli ya uchumi, busara na hekima.
Wajumbe epukeni mihemko, Lindeni Chama chenu, Mchagueni Mh Freeman Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti. Freeman Mbowe ana hekima, ana busara, msikivu, ana uthubutu na anaeleweka kwa kila mtu!