Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais Magufuli asitufanye wote wajinga, jipya ni kujenga uwanja na mbuga Chato

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais Magufuli asitufanye wote wajinga, jipya ni kujenga uwanja na mbuga Chato

Tundu Lissu akihutubia mamia ya wafuasi wa Chadema na wananchi wasio na itikadi ya chama chochote mkoani Dodoma ametoa hoja kali ambazo CCM hawana uwezo wa kuzijibu zaidi ya kupanic na kukimbilia kwenye vyombo vya habari viwahurumie wasirushe mikutano ya Tundu Lissu.

Mosi, amezungumza kuwa jipya na la ajabu kwenye utawala huu ni Rais kujenga uwanja mkubwa Chato wakati marais waliopita hawakufanya maajabu haya, amesisitiza Tundu Lissu.

Pili, ni kitendo cha Rais kupeleka mbuga Chato. Hili ni ajabu kuu ambalo halijawahi kufanyika amesisitiza Tundu Lissu.

Tatu, Lissu amesisitiza kuwa watu wamedhalilishwa, hasa viongozi wa serikali na akina Mama kwa kauli chafu zinazotolewa.

Lissu amesisitiza hii nchi sio kila mtu ni mjinga na unaweza kuwadanganya kirahisi. Kuna watu werevu na wanakwenda kuwaambia wananchi kwa miaka mitano madudu yaliyofanyika.

Je, haya maajabu ni kweli yamefanyika huko Chato?

Je, wakazi wa Lindi, Dodoma, Mbeya, Ruvuma, Arusha, Mtwara, Kilimanjaro mnafahamu maajabu haya ya huko Chato?

Kwa hoja hizi ambazo hata mimi sikuzijua kwa miaka mitano, sasa nimeamshwa usingizini.

Hoja haipigwi rungu, bali hujibiwa kwa hoja. Hii ni kauli ya Dkt Jakaya Kikwete

CCM oyeee oyeeee oyeeee, jibuni hoja hizo!
MKUU, CHATO MJI KIPENZI SASA TUNA KIWANJA CHA NDEGE, BANDARI NA MELI MPYA MV CHATO, MBUGA YA WANYAMA HADI TEMBO WANALETWA,IFADHI YETU RUBONDO IMEKUWA YA KISASA, TAA ZA KUONGOZA MAGARI JAPO MJI WETU UMEJAA PIKIPIKI NA BAISIKELI,HOTELI ZA KISASA JAPO WATEJA NI SHIDA, N.K, SASA TUNAUZA VIWANJA. KARIBU CHATO JARIBU MJI KIPENZI 2016/ 2020

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
Kwani chato ni wapi jameni, si ni Tz, sasa asahau kupata kura za chato na maeneo hayo
 
Kama una nia ya Lissu awe Rais wa Serikali ya awamu ya Sita, wewe na washambiki/wafuasi wake, mpeni/mfikisheni ushauri ufuatao:-
1) Arekebishe lugha anayotumia kuwasilisha hoja zake, kutoka ya matusi na kimahakamahakama na kuwa ya kisiasa.
2) Aheshimu mamlaka, kwa kauli na matendo yake, ili akiingia madarakani naye aheshimiwe.
3) Rais Magufuli amesimamia vizuri utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa chama chake. Yawezekana kuna mapungufu. Haya yabainishwe ni ya Sera (zilivyoainishwa kwenye Ilani) au ya utendaji wake. Kumlawaumu Magufuli, kwa ujumla, ni upofu wa uhalisia ambao unaweza kumgharimu Lissu na kundi lake. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe
4) Serikali ya awamu ya tano imefanya mambo mengi ya maendeleo, katika kipindi kifupi, ikilinganishwa na awamu zilizotangulia. Marais wastaafu na viongozi wengi Afrika na duniani kote, wanakiri hivyo hadharani. Ni kiongozi "mpumbavu" na "lofa" tu ndiye anaweza kusimama hadharani na kukebehi. Lissu akiendekeza lawama na kejeli dhidi ya Magufuli, hakuna shaka wananchi hawatasita kumwajibisha kwa kura.
5) Amekaa nje ya Tanzania kwa kipindi kirefu wakati mengi yamefanyika, hivyo afanye tathmini kabla ya kukurupuka kwa lawama na ahadi ambazo anaamini ni mpya, zitampa kukubalika na wapiga kura wakati hana jinsi ya kuthibitisha utekelezaji wake.
6) Akumbuke M/Kiti wa chama chake anatuhumiwa kufisadi fedha ya chama, ikiwa ni pamoja na ruzuku, kiasi cha kushindwa kujenga ofisi na kuwalipa wafanyakazi haki zao. Je, atawezaje kukabili na kubadili ufisadi huo wa "Boss" wake akiingia Ikulu?
7) Anaamini anapambana na CCM tu, je, amejiandaaje kwa ushindani wa wagombea Urais wa vyama vingine? Hadi sasa hajaonesha nia thabiti ya ushirikiano ikizingatiwa kuwa Uchaguzi Mkuu, 2015 CHADEMA ilivuna ushindi kupitia UKAWA na baadaye kuwatosa washirika wake. USALITI kamwe siyo mtaji katika maisha.
mbali na dar,chato na dodoma wapi kwingine nchni wanacho cha kujivunia yamefanyika mambo.Pili hayo yamesaidia nini kuboressha maisha ya wengi mbona bado ni fukara dhoofu hali kuliko awamu zote toka mkoloni
 
haoni reli? haoni madini? haioni dodoma? haoni ndege? haoni vituo vya afya? haoni meli? haoni elimu bite, haioni ubungo? haoni majizi kushughulikiwa? haoni makusanyo yakodi kuongezeka? haoni ccm safi? Nk. Nk. Haoni?

akatafute shughuli nyingine ya kufanya, akaombe hko ulaya ama ajiajiri mahali
We endelea kuidanganya familia yako tu,werevu wanakuchora tu kama katuni za kingo
 
Sawa ila kikubwa nchi iwe na maendleo
Sasa shida hapa ni tafsiri ya maendeleo, kama wafanyakazi na wakulima huwajali sasa hapo unazungumzia maendeleo gani, maana mimi kama mshahara wangu haupand na maisha yalivyopanda hv unatugemea hzo ndege ntapandaje au hzo lami, maana sisi wafanyakazi tunategewa na watu wengi huku chini.
 
haoni reli? haoni madini? haioni dodoma? haoni ndege? haoni vituo vya afya? haoni meli? haoni elimu bite, haioni ubungo? haoni majizi kushughulikiwa? haoni makusanyo yakodi kuongezeka? haoni ccm safi? Nk. Nk. Haoni?

akatafute shughuli nyingine ya kufanya, akaombe hko ulaya ama ajiajiri mahali

naona ndege hadi sasa inaendeshwa kwa hasara tupu, naona reli inajengwa kwa mkopo hadi deni la taifa limepaaa maradufu, madini yamefanya nini? kwamba yameongezeka ardhini ama wasemea ulivyo danganywa kwamba sasa mkataba uko 50/50 makusanyo ya kodi umesomewa mara ya mwisho lini na yalikuwa kiasi gani? yaani miaka mi 5 nyimbo zenu zilezile

kwamba elimu imekuwaje imekuwa bora ama
 
Tunatakiwa tujiulize kwa nini kwa miaka 59 ya uhuru bado hatuna shule za kutosha, vituo vya afya karibu na wananchi, maji safi, umeme nk. Watanzania tuna tatizo gani?
Population nayo inaongezeka,huyo lissu ataleta maajabu gani
 
so kila ajae apendelee kwao hata kwa visivo na tija je itakuwa nchi hio
Kwa iyo airport na mbuga ya wanyama havina tija, dah, hivi ushafika chato ukaona havina tija? Upinzani mnafeli sana. Unadhani atapata kura kutoka kwa wana chato?
Mbona Dom pamependelewa zaidi.
Lisu hafai kabisa.
 
Kuwa na subira kampeni bado hazijaanza, unataka aanze kunadi sera zake ili mkamuwekee pingamizi kuwa kaanza kampeni mapema?
Hawekewi mtu pingamizi msitafute sababu ya kushindwa
Ushindi utapatikana na mtapoteana humu
 
Kwa iyo airport na mbuga ya wanyama havina tija, dah, hivi ushafika chato ukaona havina tija? Upinzani mnafeli sana. Unadhani atapata kura kutoka kwa wana chato?
Mbona Dom pamependelewa zaidi.
Lisu hafai kabisa.
zile bendera zilizoshushwa chato ni za chama gani kama hakuna kura huko
 
Unataka kutuambia Marais wote walio pita hawakuwahi kununua ndege? Wakati kuna walio nunua tukala majani?

Kwamba shule hazikuwepo? Mimi nilisoma Uarabuni?

Kwamba hosipitali hazikuwepo tulitibiwa wapi? Hebu tuache utani kwenye mambobya msingi jamani.
Kumbe maendeleo ni nini basi mkuu, Kwa hiyo ulidhani afanye nini ambalo halipo hapo?

Akuletee ugali mezani kwako siyo?
 
zile bendera zilizoshushwa chato ni za chama gani kama hakuna kura huko
Za watu wa kuja tu, hakuna mwana chato mzawa aloshuhudia changes na faida ziloletwa na magufuli kupitia utalii na logistics, atamchagua lisu
 
Mh Tundu Lissu tangu ameingia Nchini hakuna hoja yoyote yenye mashiko ambayo ameitoa zaidi ya personal attack kww Magufuli.

Ila hotuba ya jana baada ya kukosa kick ya maandamano ilikuwa inachekesha sana.

Et Magufuli anawaita wazungu ambao wamekuwa wakitusaidia mabeberu anasahau, anasahau kwambq wazungu kutusaidia ni lazima na siyo omboli kwa sababu umasikini tulionao umechangiwa na wao.
 
haoni reli? haoni madini? haioni dodoma? haoni ndege? haoni vituo vya afya? haoni meli? haoni elimu bite, haioni ubungo? haoni majizi kushughulikiwa? haoni makusanyo yakodi kuongezeka? haoni ccm safi? Nk. Nk. Haoni?

akatafute shughuli nyingine ya kufanya, akaombe hko ulaya ama ajiajiri mahali
Wewe hayo unayaonaa ? au unayasikia kwenye matangazo?. Kumbuka hayo si mapya yalikuwepo miaka nenda rudi. Utekelezaji ndio umepitia hatua tofauti tofauti na kwa maraisi wote na yeye kukuta hapo na kuendeleza. Ni kweli jipya na la ajabu ambalo halikuwepo ni Uwanja mkubwa wa ndege kijijini Chato na mbuga ya chato, Burigi ilikuwepo toka zamani
 
Back
Top Bottom