Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais Magufuli asitufanye wote wajinga, jipya ni kujenga uwanja na mbuga Chato

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais Magufuli asitufanye wote wajinga, jipya ni kujenga uwanja na mbuga Chato

Zaidi ya hapo ni mkabila na hana aibu ktk hilo
Kama mpaka hapo hujagundua tatizo liko wapi basi wewe jitafakari tena. Kwanini Nyerere,Mwinyi,Mkapa na Kikwete hawakujilimbikizia mali za umma makwao? Kama Nyerere angetaka kufanya hivyo asingeshindwa lakini alijua bado sehemu nyingi za nchi yetu zina uhitaji muhimu kama maji safi, huduma za afya, barabara n.k.

Hayo anayoyasema Lissu sio mageni masikioni mwetu sanasana analenga kupata majibu kwa njia ya hoja kutoka kwa mhusika na sio vitisho.

Alichokifanya Mh. Rais ni kitendo kisichokuwa na mashiko kwa taifa akiwa kama mkuu wa nchi.
 
Hivi unajua tangu Magufuli achukue fomu hajaongea lolote zaidi ya "Mabeberu"?
Mzee kikwete ndie alie mmalizia hoja mzee mwenzake kwa kutoboa siri ambayo ndio ilikuwa turufu yakujimwambafay nayo.
Hoja kuu ilikuwa kuingia uchumi wa kati kabla ya muda, yaani 2025. Lakini mzee kikwete alipotoboa siri kwamba mipango yote ilipangwa na mzee mkapa, na lengo ni kwamba ifikapo 2025 TZ iwe katika GNI per capita $3000. Baadhi wakataka kucheza mchezo mchafu wakudai kwamba hakuna mahali panapo zungumzia $3000 ifikapo 2025, lakini walipogundua kwamba $3000 haifutiki ghafla hoja zimekwisha.
Na hata hiyo hoja ya "mabeberu" nayo imeshakwisha. Tuliaminishwa kwamba miradi yote tokea 2015 tunajisimamia kwa fedha za ndani, lakini jana kuna maelezo yanadai kwamba tumekopa zaidi ya trilion 40 ndani ya muda mfupi wa awamu hii.
Hoja kuu iliyobaki ni kuingalia dodoma tu jinsi ilivyo jaa magorofa.
 
haoni reli? haoni madini? haioni dodoma? haoni ndege? haoni vituo vya afya? haoni meli? haoni elimu bite, haioni ubungo? haoni majizi kushughulikiwa? haoni makusanyo yakodi kuongezeka? haoni ccm safi? Nk. Nk. Haoni?

akatafute shughuli nyingine ya kufanya, akaombe hko ulaya ama ajiajiri mahali
Mkuu hivi zamani kama ulikua na gari mmoja ukaliuza na badae ukanunua kingine basi inaonyesha umepiga hatua kubwa?
 
siasa zinamfanya lissu kuwa na akili ndogoo Sana (zinamdumaza ubongo). Angeendelea na uwakili angesaidia wengi sana huku anakwaza kwakukosa misimamo na kupotosha jamii labda uwakili wake pia ulisheheni uongo na dharau
Lissu ndo kaja sasa. Mlishindwa kumzuia kwa risasi, njozi zako zitakukondesha tu.
 
Tundu Lissu akihutubia mamia ya wafuasi wa Chadema na wananchi wasio na itikadi ya chama chochote mkoani Dodoma ametoa hoja kali ambazo CCM hawana uwezo wa kuzijibu zaidi ya kupanic na kukimbilia kwenye vyombo vya habari viwahurumie wasirushe mikutano ya Tundu Lissu.

Mosi, amezungumza kuwa jipya na la ajabu kwenye utawala huu ni Rais kujenga uwanja mkubwa Chato wakati marais waliopita hawakufanya maajabu haya, amesisitiza Tundu Lissu.

Pili, ni kitendo cha Rais kupeleka mbuga Chato. Hili ni ajabu kuu ambalo halijawahi kufanyika amesisitiza Tundu Lissu.

Tatu, Lissu amesisitiza kuwa watu wamedhalilishwa, hasa viongozi wa serikali na akina Mama kwa kauli chafu zinazotolewa.

Lissu amesisitiza hii nchi sio kila mtu ni mjinga na unaweza kuwadanganya kirahisi. Kuna watu werevu na wanakwenda kuwaambia wananchi kwa miaka mitano madudu yaliyofanyika.

Je, haya maajabu ni kweli yamefanyika huko Chato?

Je, wakazi wa Lindi, Dodoma, Mbeya, Ruvuma, Arusha, Mtwara, Kilimanjaro mnafahamu maajabu haya ya huko Chato?

Kwa hoja hizi ambazo hata mimi sikuzijua kwa miaka mitano, sasa nimeamshwa usingizini.

Hoja haipigwi rungu, bali hujibiwa kwa hoja. Hii ni kauli ya Dkt Jakaya Kikwete

CCM oyeee oyeeee oyeeee, jibuni hoja hizo!
Hiyo nayo ni hoja hata imuumize kichwa mwana ccm!?, Trust me kwa hoja hizi ambazo hazina mashiko Chadema mnaendelea kujichimbia kaburi lenu wenyewe Tena mapema sana because hicho alicho kiongea TL hakuna mtanzania yoyote atakayekuwa twisted kwenye box la kura eti amchague dead Lissu.
 
Kosa kingine kwa Tundu lissu
Lissu hatakiwi kumshambulia Magufuli
Lissu anatakiwa atuambie atafanya Nini,kukomaa na Magufuli ni sawa na kuzidi kujipunguzia kura tu
Hivi kujenga hospital kubwa 69 sio maajabu
Kukarabati shule za sekondari ambazo haziguswa toka mkoloni si maajabu
Chadema mjipange sana na lissu wenu mtajikuta mmeishiwa maneno baada ya wiki moja tu toka kuanza kampeni
Kwenye mchezo wa mpira: Mshindani anaweza kumchagulia mbinu mshindani wake? Ndivyo ilivyo kwenye siasa.
 
Kosa kingine kwa Tundu lissu
Lissu hatakiwi kumshambulia Magufuli
Lissu anatakiwa atuambie atafanya Nini,kukomaa na Magufuli ni sawa na kuzidi kujipunguzia kura tu
Hivi kujenga hospital kubwa 69 sio maajabu
Kukarabati shule za sekondari ambazo haziguswa toka mkoloni si maajabu
Chadema mjipange sana na lissu wenu mtajikuta mmeishiwa maneno baada ya wiki moja tu toka kuanza kampeni
Awamu ya pili utawala wa mkono wa chuma utatamalaki zaidi, JPM na CCM yake sasa basi.
 
haoni reli? haoni madini? haioni dodoma? haoni ndege? haoni vituo vya afya? haoni meli? haoni elimu bite, haioni ubungo? haoni majizi kushughulikiwa? haoni makusanyo yakodi kuongezeka? haoni ccm safi? Nk. Nk. Haoni?

akatafute shughuli nyingine ya kufanya, akaombe hko ulaya ama ajiajiri mahali
Sina uhakika na umri wako, pengine kuna vitu vingi hukuviona. Lakini kwa umri wangu vyote ulivyo viorodhesha haikutakiwa tuwe tunavizungumzia kwa sasa, kwa sababu vingi vilikuwepo na tukavipoteza kutokana na mfumo mbaya wa uongozi wa ccm. Miaka zaidi ya 50 bado ccm ina ahidi tu?
 
Kosa kingine kwa Tundu lissu
Lissu hatakiwi kumshambulia Magufuli
Lissu anatakiwa atuambie atafanya Nini,kukomaa na Magufuli ni sawa na kuzidi kujipunguzia kura tu
Hivi kujenga hospital kubwa 69 sio maajabu
Kukarabati shule za sekondari ambazo haziguswa toka mkoloni si maajabu
Chadema mjipange sana na lissu wenu mtajikuta mmeishiwa maneno baada ya wiki moja tu toka kuanza kampeni
Yote hayo fanya maana ni kodi zetu na resouces zetu, shida umuhimu wa kujenga Airpot Chato nyumbani??
Chachu kidogo huchachua donge zima!!
Bunge lilipitisha hiyo au ni CCM ndiooooooo???
Matumizi yasiyo na mpangilio unaoeleweka unbudgeted exepencies, kama vile unatoa kwenye mfuko wa familia!!
Huo ni udectateta, tunahitaji katiba nzuri ya kudhibiti mambo aina hiyo!!
Mwana sheria nguli Tundu Lisu atatupatia hiyo katiba with rules & regulations!!
 
je hivo ni mahitaji ya wanachato kwamba maisha yao ni magumu sababu avikuwepoo hivo vitu kabla.Pamoja na vyote hivo mbona je bado akubaliki kwao

Kutokukubalika hakuzuii kufanyika maendeleo,
 
Sina uhakika na umri wako, pengine kuna vitu vingi hukuviona. Lakini kwa umri wangu vyote ulivyo viorodhesha haikutakiwa tuwe tunavizungumzia kwa sasa, kwa sababu vingi vilikuwepo na tukavipoteza kutokana na mfumo mbaya wa uongozi wa ccm. Miaka zaidi ya 50 bado ccm ina ahidi tu?
Siyo issue ya umri ni welewa you... Sasa vitu vimerudi lazima tupongeze jitihada zilizovirudisha... Chadema miaka 28 haina hata ofisi yake binafsi sasa wanaubunifu gani mpaka wapewe nchi?? Kazi kupeana viti maalumu,kukosoa na kuzini. Wapotee huko matapeli wa kisiasa
 
Hehee, nikue mara ngapi, kama ulikuwa na vyeti feki, au unapata hela burebure mianya imezibwa, jilaumu mwenyewe.
October ndio chepeo la mwisho kwenye jeneza la chadema, ACT is next
mnaukimbiza upepo,
 
Tundu Lissu akihutubia mamia ya wafuasi wa Chadema na wananchi wasio na itikadi ya chama chochote mkoani Dodoma ametoa hoja kali ambazo CCM hawana uwezo wa kuzijibu zaidi ya kupanic na kukimbilia kwenye vyombo vya habari viwahurumie wasirushe mikutano ya Tundu Lissu.

Mosi, amezungumza kuwa jipya na la ajabu kwenye utawala huu ni Rais kujenga uwanja mkubwa Chato wakati marais waliopita hawakufanya maajabu haya, amesisitiza Tundu Lissu.

Pili, ni kitendo cha Rais kupeleka mbuga Chato. Hili ni ajabu kuu ambalo halijawahi kufanyika amesisitiza Tundu Lissu.

Tatu, Lissu amesisitiza kuwa watu wamedhalilishwa, hasa viongozi wa serikali na akina Mama kwa kauli chafu zinazotolewa.

Lissu amesisitiza hii nchi sio kila mtu ni mjinga na unaweza kuwadanganya kirahisi. Kuna watu werevu na wanakwenda kuwaambia wananchi kwa miaka mitano madudu yaliyofanyika.

Je, haya maajabu ni kweli yamefanyika huko Chato?

Je, wakazi wa Lindi, Dodoma, Mbeya, Ruvuma, Arusha, Mtwara, Kilimanjaro mnafahamu maajabu haya ya huko Chato?

Kwa hoja hizi ambazo hata mimi sikuzijua kwa miaka mitano, sasa nimeamshwa usingizini.

Hoja haipigwi rungu, bali hujibiwa kwa hoja. Hii ni kauli ya Dkt Jakaya Kikwete

CCM oyeee oyeeee oyeeee, jibuni hoja hizo!
Hizi ndio hoja zitakazo mshushia hadi na heshima huyu Lissu. Watanzania sasa hivi wantaka hoja siyo maelezo yanayo nhusu mtu binafsi and in this case Rais Magufuli. Ni watu wachache sana watateka akili na hoja hizi, in fact watakao zishabikia ni wana CHADEMA tu. Hivyo watamuunga mkono, sasa hao neutrals atawateka kwa hoja zipi? Hizi hizi za KIANA UHARAKATI au nyingine? Ni vizuri Lissu ashauriwe aachane na UANA HARAKATI na afanye SIASA. Hii ni hoja yangu, asiyekubaliana nayo aje na hoja mbadala SIYO MATUSI ambayo hayayatufikisha popote.
 
haoni reli? haoni madini? haioni dodoma? haoni ndege? haoni vituo vya afya? haoni meli? haoni elimu bite, haioni ubungo? haoni majizi kushughulikiwa? haoni makusanyo yakodi kuongezeka? haoni ccm safi? Nk. Nk. Haoni?

akatafute shughuli nyingine ya kufanya, akaombe hko ulaya ama ajiajiri mahali
Huyu Tundu Lissu ndiye anayedhani WaTZ ni wajinga. Anajifariji. Nani asiyeona hayo? Hivi aliporudi juzi alimleta yule dereva wake?
 
Population nayo inaongezeka,huyo lissu ataleta maajabu gani
Hatokuwa na maajabu sana lakini ni vizuri kupokezana ili kuwepo na ushindani lakini kikubwa si sawa kupewa ahadi za mambo ya jamii ambayo ni lazima kila serikali ifanye. Tuwapime namna watakavyo kuza uchumi kwa kuongeza shughuli za uchumi na uzalishaji, biashara za nje na ndani na upanuaji wa shughuli za kuajili watu wengi vijijini nk ambapo serikali haitafanya biashara bali itaweka mazingira rafiki kwa wekezaji na yenyewe itakusanya kodi ili kutumika kwenye maendeleo ya jamii.
 
Back
Top Bottom