Pre GE2025 Tundu Lissu: Rais Samia, Kiongozi wetu Deus Soka Ametekwa, Hajulikani Alipo kwa Wiki Mbili

Pre GE2025 Tundu Lissu: Rais Samia, Kiongozi wetu Deus Soka Ametekwa, Hajulikani Alipo kwa Wiki Mbili

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Siku moja nilikumbuka zile theories nikiwa student wa mlimani miaka ile ambazo hufundisha kuangalia genesis na causes na si effects, nikasema kuna nini kiko mbele muda huu nikaona kumbe shida kubwa ni uchaguzi , watu wanatekwa na kuuawawa, wengine wanalawiti vitoto, wengine wanauana na kunyofoana viungo!

African bloody elections are cursed!!
Bora uchaguzi upite tubaki salama!!
Kama sababu za matendo hayo ni uchaguzi, basi tuna wanasiasa wajinga sana, wasiofaa kwa nyakati hizi za sayansi na teknolojia.
Kuna haja ya kufanya mabadiliko makubwa katika fikra za watu kwa kuwachagua viongozi wenye fikra na akili chanya, wanaopenda uwazi na ukweli.
 
Samia wa Waarabu Uarabuni
.....DP WORLD....

Kwa mwezi tunaingiza trilioni 26....

Wakati wa ile tenda ,wazungu wa Ubelgiji hawakuwepo nao wakaingia katika ushindani wa zabuni?!!

NEVER GIVE WISDOM TO UNWORTHY AS IT IS UNJUST TO THE KNOWLEDGEABLE [emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Ni lini Tanzania itakuwa na amani ya kweli?.
Samia anatakiwa asafishe vyombo vyake vya usalama.
Kuanzia waziri ,IGP mpaka usalama wa taifa.yaani mtu akiwa kwenye vyombo hivyo anafanya anavyotaka na hakuna wa kumfanya kitu.mmechukuliana mademu anakuteka anakupoteza,una mdai anakuteka anakupoteza.na viongozi wao wapo na wanajua ila wana walinda
 
Simba wa Kizimkazi Tundu Lissu amepeleka kilio kwa Rais Samia juu ya kutekwa kwa Deus Soka

"Nakusihi kwa moyo wangu wote: usijesahau ya mtangulizi wako alikufa huku damu ikimlilia. Angalia yasije yakakufika yaliyomfika".
maneno mazito sana haya!, they have something to do with karma.
p
 
Yes, mgekubali kuungana pamoja kipindi kile tunawaambia Dkt Magufuli hahusiki anasingiziwa ila kuna kikundi cha wahuni wanaochafua taswira yake mlikataa na kushangilia mkisema mtekaji kafa ila sasa mnaanza kulia lia
Aliyeasisi CCM ni nyerere hayupo sasa na bado CCM ipo.. je hapa waweza sema nini tena
 
Simba wa Kizimkazi mh Tundu Antipas Lisu amepeleka kilio chake kwa Rais wa JMT mh Dr Samia juu ya kutekwa na kupotea kwa kijana Deus Soka

Makamu Mwenyekiti huyo wa Chadema ametoa kilio chake ukurasani X

Ahsanteni Sana 🐼

======
Rais Samia, kijana huyu anaitwa Deus Soka; ni kiongozi wetu wa chama katika wilaya ya Temeke. Tarehe 26 Julai alikuja kunipokea Dar International Airport niliporudi safari ya Ulaya. Sasa, baada ya vitisho vingi, watu wako wamemteka nyara. Hajulikani alipo kwa zaidi ya wiki mbili

Waliomteka nyara wanajulikana. Ni watu wa kikosi kazi chenye makao makuu yake nyuma ya Kituo cha Polisi Chang'ombe, Dar es Salaam. Kikosi kazi hiki ni kundi la maharamia, hata kama wanajiita askari polisi au usalama wa taifa na wanalipwa mishahara kwa kodi zetu. Ni kundi haramu.

Kwa Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa kama ilivyo leo, wewe, Rais Samia, unahusika moja kwa moja & maharamia hawa. Sheria hiyo inasema wanawajibika kwako. Wote wako chini ya mamlaka yako kikatiba & kiutendaji. Mimi nasema wewe ndiye unayewatuma wafanye uharamia wao kwa wananchi.

Nakusihi kwa moyo wangu wote: usijesahau ya mtangulizi wako & kikosi kazi chake cha 'watu wasiojulikana.' Yeye alikufa huku damu ya Ben Saanane & ya Azory Gwanda & ya Simon Kanguye ikimlilia. Angalia yasije yakakufika yaliyomfika. Mrudishe Deus Soka & wenzake wakiwa hai & salama

Pia soma:Kuelekea 2025 - Watu Wasiojulikana: Malisa aelezea tukio la kutekwa kwa Deus Soka na vijana wengine wawili wa CHADEMA
Mama Dr Samia Suluhu Hassan asaidie viongozi hawa wapatikane
 
Naogopa akipewa motano tena hiyo 2025. Kama pamoja na hofu ya uchaguzi hiyo 2025 anaweza kuwa katili kiasi hiki, akiwa hana cha kupoteza nani atamfunga speed governor?
Sijui kama waTanzania wana ufahamu ukweli huu.

Huyu akichaguliwa, kwa kura za wizi (kwani kikawaida hawezi kushinda), nchi yetu itakuwa kwenye matatizo makubwa.

Siyo uuaji tu na mateso kwa watu; huyu atauza raslimali zote za nchi. WaTanzania tutakuwa watu tegemezi kwa kila kitu; hakuna tutakachoweza kukifanya sisi wenyewe kwa ufanisi. Sasa niambie ni nchi gani iliyo wahi kupata maendeleo kwa kuwa tegemezi kwa wengine!
 
Hata hivyo,

Hatutaogopa,

Wala kutishwa ,

Hadi pale Giza la UOVU litakapoondoka juu ya anga la nchi yetu nzuri tuipendayo TANZANIA 🇹🇿. Amen
 
Kazi za akina Makamba Cop ndio zimeanza lasimi bado picha za viroba baharini,watafanya kila mbinu mpaka wahakikishe Samia 2025 amechafuka, kama walivyokuwa wakifanya enzi za Magufuli, vita lasimi ya kiti cha urais ndio zimeanza, lakini Samia mwache nae haionje maana ndiye waasisi wa haya mambo mpaka Magufuli alikuwa mpaka alikuwa analalamika siri za Serikali yake kuvujishwa,kumbe kikulacho.
Mnachafua wenyewe then mnasingizia watu.

Mara hii hawasingiziwa Mabeberu?
 
Kazi za akina Makamba Cop ndio zimeanza lasimi bado picha za viroba baharini,watafanya kila mbinu mpaka wahakikishe Samia 2025 amechafuka, kama walivyokuwa wakifanya enzi za Magufuli, vita lasimi ya kiti cha urais ndio zimeanza, lakini Samia mwache nae haionje maana ndiye waasisi wa haya mambo mpaka Magufuli alikuwa mpaka alikuwa analalamika siri za Serikali yake kuvujishwa,kumbe kikulacho.
Kwahiyo unataka kusema kijana hajapotea?
 
Back
Top Bottom