Tundu Lissu: Rais Samia Suluhu Hassan atakuwa shahidi wangu apelekewe barua ya wito

Tundu Lissu: Rais Samia Suluhu Hassan atakuwa shahidi wangu apelekewe barua ya wito

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876

WhatsApp Image 2026-08-21 at 11.35.56e.jpeg

WhatsApp Image 2026-08-21 at 11.36.024.jpeg

WhatsApp Image 2026-08-21 at 11.35.59.jpeg
Baada ya Mahakama kutoa uamuzi kwamba mshtakiwa Tundu Lissu ana Kesi ya kujibu, Lissu amesema kwamba atakuwa na mashahidi 11 ikiwemo yeye mwenyewe kujitetea, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mstaafu Dkt. Mpango, Waziri Mkuu mstaafu, Kassim Majaliwa.

Wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Mkuu wa majeshi, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Brenda Rupia.

Upande wa Jamhuri umeileza Mahakama kwamba mashahidi wote waliotajwa na Tundu Lissu hawakutajwa wakati wa "committal review".


================================​

Wakili Katuga: Si busara Mahakama kuwaita mashahidi saba waliotajwa na Lissu, akiwemo Rais Samia

Wakili Mkuu wa Serikali, Nassoro Katuga, amesema hakuna haja ya Mahakama kuwaita mashahidi ambao mshtakiwa, Lissu, amewataja na ambao wanatokana na Serikali.

Amesema ushahidi ambao tayari umetolewa na upande wa Jamhuri umehusisha baadhi ya watendaji wa Serikali ambao ni miongoni mwa mashahidi hao. Hivyo, kwa mujibu wa Katuga, mashahidi waliotajwa na Lissu tayari wamewasilisha ushahidi wao kupitia watendaji hao.

Amesema baadhi ya mashahidi waliotajwa na mshtakiwa wanafanya kazi kwa niaba ya Rais, hivyo hakuna umuhimu wa Mahakama kuwaita kutoa ushahidi.

Katuga amesema si busara kwa Mahakama kutoa wito kwa mashahidi waliotajwa na mshtakiwa kwa sababu tu wametajwa.

Amesema kwamba hawana shida na mashahidi wengine ambao hawatokani na Serikali isipokuwa utaratibu uzingatiwe.
WhatsApp Image 2026-08-21 at 11.35.578.jpeg
WhatsApp Image 2026-08-21 at 11.35.57o.jpeg

===========================
​
Lissu: Utaratibu unaruhusu Rais kupelekewa wito na Mahakama, ataamua mwenyewe kuuheshimu

Mshtakiwa Tundu Lissu akijibu hoja ya Jamhuri katika shauri la uhaini linalomkabili amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kupelekewa wito na Mahakama kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi au Katibu Binafsi wa Rais, ili kusaidia Mahakama kufikisha wito huo.

Awali, upande wa Jamhuri uliieleza Mahakama kwamba haina mamlaka ya kumuita Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha mshtakiwa Tundu Lissu, akijibu hoja ya upande wa Jamhuri kwamba mashahidi aliowataja hawakuwepo katika committal proceedings, amesema kuwa katika Mahakama ya Kisutu, hakimu alikataa kurekodi majina ya mashahidi wake alipoanza kuwataja.

Amesema baada ya kesi kufika Mahakama Kuu, alilalamikia suala hilo, ambapo Mahakama ilimpa nafasi ya kuwataja mashahidi wake ili majina yao yawekwe kwenye kumbukumbu.

Kufuatia maelezo hayo, Lissu amesema hoja ya upande wa Jamhuri haina mashiko, kwa kuwa tayari mashahidi hao wapo kwenye kumbukumbu za Mahakama.
 
Waacheni waje tu wote.... Jamuhuri...
Hawatoboi...- Kwamba Mahakama haingii zaidi kupima uzito wa Ushahidi....!!!!!!???Kwa Leo tu au..!!?Ni..kawaida kwa Kesi za Jinai hiyo..lakini hitimisho ni hukumu ya Mwisho ...! -Beyond reasonable doubt- hamna hapo..
 
Baada ya Mahakama kutoa uamuzi kwamba mshtakiwa Tundu Lissu ana Kesi ya kujibu, Lissu amesema kwamba atakuwa na mashahidi 11 ikiwemo yeye mwenyewe kujitetea, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mstaafu Dkt. Mpango, Waziri Mkuu mstaafu, Kassim Majaliwa.

Wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Mkuu wa majeshi, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Brenda Rupia.
Duuh
 
Najaribu tu kuwaza, hivi hao Majaji wakitoka hapo wakiwa peke yao huwa wanajiskiaje?

Dhamira zao huwa ni kweli zinawaambia maamuzi yao ni ya haki?

Kwamba wameshawishika na hoja za mashahidi kuwa Lissu ndio aliyechapisha video kwenye account ya Jambo TV, na hivyo kumfanya awe na kesi ya kujibu?

Kweli jamani, hili nalo linahitaji taaluma ya sheria kuweza kujua huu ni uongo?

Lissu ana moyo wa kijasiri mno, mi pale ningekuwa mimi ningekuwa mimi tayari ningeshamuita mtu mseng£. Kwasababu namjua nikimuona hata ajifiche kwenye lile box.
 
Najaribu tu kuwaza, hivi hao Majaji wakitoka hapo wakiwa peke yao huwa wanajiskiaje?
Hakuna kitu chochote wanachojisikia we unadhani mpaka wamekuwa Majaji kwa Nchi zetu hizi wamefikafikaje
 
Back
Top Bottom