Siku zote watu wanaosimama katika haki bila kutetereka, kama alivyo Lisu, huheshimika na watu wote wapenda haki Dunia nzima. Laana huwa ni kwa wadhulumu haki. Wala haitashangaza kuona Lisu akipewa nishani mbalimbali za kimataifa, linapokuja suala la haki. Watu kama Lisu ni nadra sana kupatikana Duniani! Watu wanamhonga, wanamwahidi pesa na madaraka ili aisaliti haki, lakini anaamua kubakia katika matesa ili tu kuipambania haki. Tulio wengi, huenda mateso ya siku moja tu, tungekuwa tumenyosha mikono, lakini, Lisu ni tofauti kabisa.
Basi tunamwomba Mungu azidi kumwimarisha Tundu Lisu ili kupitia Lisu, ukuu wa Mungu ukapate kuonekana, kwa maana Mungu wetu, ni Mungu wa ukweli na haki.