Tundu Lissu ni mwanasiasa anayerudi nchini Tanzania kula bata baada ya matakwa yake yote kutimizwa, utakuta kuna mtu anamsubiri Tundu Lissu akiamini ni mpinzani, la hasha, Tundu Lissu anarudi nchini Tanzania baada ya yale yote aliyoyapigania katika harakati zake kutimizwa na Hayati Rais Magufuli, Tundu Lissu si yule wa mwaka 2009 aliyekuwa anaandika vitabu na kufanya tafiti kule North Mara kuhusu migodi akiwa pamoja na Viongozi wa Kitaifa wa Chadema wakipitia mikataba ya madini na kusema tunadhulumiwa sana kwenye mikataba yetu ya madini, Tundu Lissu sio yule wa 2008 akionekana TBC1 akielezea issue ya mgodi wa North Mara,Buzwagi na GGM.