Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Tanzania haiwezi kuishi bila dunia ila dunia inaweza kuishi bila Tanzania

Hiyo kauli ni zao la utumwa na ni matokeo ya kutawaliwa kiakili na ukoloni orijino na ukoloni mamboleo. Hakuna kitu kibaya kuwahi kutokea kwa mtu mweusi kama kutawaliwa na wazungu.

Ukoloni umetuathiri kiasi kwamba miaka 50 baada ya uhuru unaona vichembe vya kutawaliwa bado vipo. Hatujiamini, tunacheza beat ya mzungu kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kauli hii ya Lissu ni matokeo hayo hayo; nilishangaa juzi niliposikia Lissu kasoma sijui Marekani huko. Tusipokuwa makini katika elimu zetu hizi kufahamu kuwa elimu ya kikoloni ipo designed kuendelea kumformat mtu acheze beat ya kikoloni tutajikuta tunatumia visomo vyetu kumnufaisha mzungu badala ya kutunufaisha sisi, nchi zetu na watoto wetu.

Hivyo, ni kweli kwamba Tanzania inaihitaji dunia lakini hili halimaanishi kwamba ndio tuweke akili zetu mifukoni na kushindwa kung'amua ni maeneo gani tunaihitaji dunia bila kuathiri maslahi yetu mapana.
 
Wale genetically born Wana akili, Sasa we linganisha na watu wako hata kutengeneza choo hawaeezi wanajisaidia porini Kama ngedere,
Sisi bado Sana ku catch up na dunia inabidi tusaidiwe Kwanza Kuna generation zitakuja kustaarabika baadaye
Shame On You Nachukuia sana Watu Wa Aina hii wanadharau Race yao Huna Adabu Akili yakoo in primitive sana
 
Hizo ulizozitaja sio nchi zilizoendelea
Mkuu, huwezi kufananisha Tanzania na hayo mataifa kama N.Korea na Cuba au Iran, hizo ni nchi zilizo katika ulimwengu wa kwanza(nchi zilizoendelea toka kitambo) ndo maana wana uwezo wa kusavaivo bila shida.
Sawa Tanzania hii kinchi masikini kama hiki tumekaa tunafarijiana kuwa Tupo uchumi wa kati hali ya kuwa raia wengi tuko hoi kimaisha.
Binafsi nayakubali kimtindo haya maneno ya Lissu kwani sisi bado hatujiwezi na kiburi hicho kwa mataifa makubwa hatuna.

Just emagine, taifa dogo lingeweza kuwa na migogoro na USA..? Naamini USA awezi kufanya battling na taifa lolote la kimasikini ambalo limeizidi kila kitu, So ukiona N.Korea, Iran sijui Cuba wanaweza kufanya battling na Marekana basi fahamu nao si haba(wameadvance)
 
Wengi hamjamwelewa vizuri huyo mgombea aliyeyatamka maneno hayo.
Kwa kifupi ni kwamba, yeye ameshaingia mikataba ya kuiuza Nchi yetu kwa MABEBERU, hasa kipindi kile alipokuwa anazurura katika Nchi za Ulaya na US.
Kwa hiyo anataka kama angebahatika kuwa Rais, aweze kuwaleta na kuwajaza hao MABEBERU karibu kila kona hapa Nchini kwa kisingizio cha kurejesha mahusiano, kumbe ukweli wake ni kwamba hao MABEBERU wake watakuwa wanakuja kuchukua chao kulingana na mkataba wao.
 
Wale genetically born Wana akili, Sasa we linganisha na watu wako hata kutengeneza choo hawaeezi wanajisaidia porini Kama ngedere,
Sisi bado Sana ku catch up na dunia inabidi tusaidiwe Kwanza Kuna generation zitakuja kustaarabika baadaye
Wakuu habarini za jioni,

Natumai mko salama na mnaendelea na majukumu yenu.

Nimeona niulete huu uzi wa mheshemiwa Tundu Lisu hapa tuujadili ili tuone kama kweli hoja hii ina mashiko . Nimemsikiliza huu mheshimiwa (Tundu Lisu) akiwa Shinyanga anasema kuwa Tanzania haiwezi kuishi bila Dunia ila Dunia inaweza kuishi bila Tanzania, na akasema akishinda uraisi basi atahakikisha anarudisha mahusiano mema ya Tanzania na nchi za magharabi ambazo Magufuli anaonekan a kujitenga nazo.

Je ni kweli kuwa Tanzania haiwezi kuendelea bila mahusiano mema na nchi za kibepari ? Kama ni kweli Je vipi kuhusu nchi kama Korea Kaskazini na Cuba ambazo ni kama zimetengwa na ulimwengu hasa mataifa makubwa lakini mbona wanaishi ?

Ukiangalia korea kaskazini ina uhusiano na China na Urusi pekee lakini Je mbona wanaendelea kusonga mbele na wameweza hadi kutengeza silaha za Nuclear kuwatisha hadi wamarekani, nawasilisha
Umemuuuereeewa leso yenyewe unasubiri mchina akitengenezee tulia hivyo hivyo
 
Kwanza kama kawaida yake tundu lissu ni muongo mkubwa na mtu hatari kwa nchi yetu. Si kweli tanzania haina mahusiano mema na nchi za magharibi. Kuna uhusisno wa kibalozi ila sio ule nchi hizo zinataka kua na nchi kama tanzania. Nchi za magharibi uchumi wao unashamiri kwa makampuni katika nchi zao kufanya biashara na uwekezaji wa kinyonyanyi na uporaji katikaka nchi changa hasa zile zilizowahi kuwa makoloni yao.
Nchi zenye uongozi kama wa magufuli zinaonekana korofi kwa kutetea maslahi yao ya kiuchumi ya nchi zao. Vibaraka wanaotengenezwa kama lissu ndio jitihada hufanyika kuwaingiza uongozini ili kulinda mirija ya unyonyaji ya nchi hizo. Sote tunajua jinsi lissu alivyotumika kujaribu kutetea maslahi ya acacia.
Tuwaepuke kina lissu kama ukoma.
 
Sisi tumetake risk wa kufa afe wa kuishi aishi na hicho kimesaidia, maana dunia haina full understanding na Corona it's a new disease, kwamba Kama una immunity ya kutosha you will survive, most of viral disease ipo hivyo kama nyie wajanja ebu anzen kuomba ukimwi uishe
Kuna kitu apo ukikijua tu basi, hata na huo Ukimwi na izo ARV tena soma humu humu JF, kuna threads zinaelezea, kuna mchezo wa mass mind programming unaendelea hapa duniani, nilikuwa nina wasiwasi kuamini iyo claim, lakini kwa hii corona, nimepiga mstari rasmi.. Tatizo kuamini ngumuuu..
 
Wakuu habarini za jioni,

Natumai mko salama na mnaendelea na majukumu yenu.

Nimeona niulete huu uzi wa mheshemiwa Tundu Lisu hapa tuujadili ili tuone kama kweli hoja hii ina mashiko . Nimemsikiliza huu mheshimiwa (Tundu Lisu) akiwa Shinyanga anasema kuwa Tanzania haiwezi kuishi bila Dunia ila Dunia inaweza kuishi bila Tanzania, na akasema akishinda uraisi basi atahakikisha anarudisha mahusiano mema ya Tanzania na nchi za magharabi ambazo Magufuli anaonekan a kujitenga nazo.

Je ni kweli kuwa Tanzania haiwezi kuendelea bila mahusiano mema na nchi za kibepari ? Kama ni kweli Je vipi kuhusu nchi kama Korea Kaskazini na Cuba ambazo ni kama zimetengwa na ulimwengu hasa mataifa makubwa lakini mbona wanaishi ?

Ukiangalia korea kaskazini ina uhusiano na China na Urusi pekee lakini Je mbona wanaendelea kusonga mbele na wameweza hadi kutengeza silaha za Nuclear kuwatisha hadi wamarekani, nawasilisha
Kwani Urusi na Uchina si mabepari!!!?
 
Wanaosema Lissu ni wakala wa mabeberu wanakuwa wamezisikia hoja zake, mfano hii ya sasa.

Tanzania ya awamu ya tano imejitambua thamani yake na inao muelekeo wa kuishi kulingana na thamani hiyo.

Madalali wa wezi wa kimataifa ndio wanaoamini sana katika kutaka kupendwa na wa huko nje. Ndio wanaoamini sana katika hizo falsafa za demokrasia kwa mujibu wa tafsiri ya kimagharibi.

Ni aina ya wasomi wengi waliojaa Twitter na Facebook na katika hii dunia ya viganjani.
 
Hiyo kauli ni zao la utumwa na ni matokeo ya kutawaliwa kiakili na ukoloni orijino na ukoloni mamboleo. Hakuna kitu kibaya kuwahi kutokea kwa mtu mweusi kama kutawaliwa na wazungu.

Ukoloni umetuathiri kiasi kwamba miaka 50 baada ya uhuru unaona vichembe vya kutawaliwa bado vipo. Hatujiamini, tunacheza beat ya mzungu kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kauli hii ya Lissu ni matokeo hayo hayo; nilishangaa juzi niliposikia Lissu kasoma sijui Marekani huko. Tusipokuwa makini katika elimu zetu hizi kufahamu kuwa elimu ya kikoloni ipo designed kuendelea kumformat mtu acheze beat ya kikoloni tutajikuta tunatumia visomo vyetu kumnufaisha mzungu badala ya kutunufaisha sisi, nchi zetu na watoto wetu.

Hivyo, ni kweli kwamba Tanzania inaihitaji dunia lakini hili halimaanishi kwamba ndio tuweke akili zetu mifukoni na kushindwa kung'amua ni maeneo gani tunaihitaji dunia bila kuathiri maslahi yetu mapana.
Mkuu jana nimesikiliza mahojiano ya mh.Lissu itv, unachosema ni kweli kabisa mfumo wetu umekaa kw maslah ya wakoloni ingawa bado tunahitaji watu makini kufahamu haya, nirudi kwa Mh.Lissu. Wkt wa mahojiano yake anasema anataka uhuru wa wananchi na taasisi binafsi kufanya watakayo kwa maendeleo ya JMT akatolea mfano kabla ya uhuru wa inchi kulikua na hospital,mashule na maofisi yaliyo tengenezwa na watu au taasisi za kidini na zilikua bora pia akaongelea vipaumbele wkt wa uhuru yan Umaskini,Ujinga na Maradhi ambavyo mpka sasa vipo na serikali imeshindwa ktk hili na pia akaongelea wakulima wa jembe la mkono inakuaje waachwe bila msaada ila wakitaka kuuza mazao yao wakutane na kodi????? Sasa binafsi naheshimu mawazo yake na mitazamo lkn nna yangu pia ukitaka kuondoa kodi ktk mazao,biashara ina maana pato la taifa upande wa kodi serikali bado itakwama kwani inataka pia kodi na pia serikali inatoa sehemu ya pembejeo kwa gharama za kawaida mno ili kuwasaidia hawa wakulima. Nikiongelea umasikini,ujinga na maradhi kbla ya uhuru na baada ya uhuru tuikua na idadi ndogo ya wa tz ambao ilikua rahisi kuwasimamia muda unaenda na changamoto zinakua kubwa, umasikini lazima kuwe na miundombinu bora ikiwemo barabara,maji,umeme,huduma za afya ili kumfanya huyu mwananchi aweze kupata na kupeleka bidhaa zake sehemu husika kwa ufanisi na apate faida. Maradhi lazima kuwe na vituo vya afya,watoa hizo huduma,madawa na pia barabara bora ktk kupata hizo huduma kwa wkt. Ujinga hapa ndo kunabeba sehemu kubwa ya jamii yetu, ujinga kuuondoa pia nikubali kujifunza na kukubali makosa ktk maisha yangu hapa kuna elimu na mazingira bora ya kujifunza pia hii haitoki sababu ya elimu tuu ila pia na makuzi yetu majumbani mwetu je tuko wangapi tunaowapa majibu sahihi watoto wetu yaan huwez kupata kiongozi bora bila kumtengeneza tokea mwanzo, shule hufundisha watoto wetu lkn maneno ya mtoto na tabia huanzia nyumbani then shule hufanya shape kwa huyu mtoto kupata tunachotaka ila ni bure kama bado nyumbani kuna tatizo yaan hiwez kutegemea mtoto asiwe fisadi kama anaona wzazi mmoja wao anajipendelea zaid au ni m'binafsi. Mwisho tunahotaji utaratibu mzuri wa kufanya vitu sisemi CCM AU CHADEMA AU ACT AU CUF AU CHAUMA NI BORA ILA TUNAHITAJI HAYA MAWAZO YAO KUA KWA WATU SAHIHI KWA MAENDELEO YA JMT. Kuna mengi mh.Lissu amesema we need Order to everything but is that order been useful or its just an harrasement to others????????!!!!!!!! Kuna mengi ya kuweka sawa na mengi ya mh.Lissu sijaandika hapa na wengine tusaidiane ili tupate uhakika wa nani tunampa kura zetu OCTOBER HAPA JMT
 
Lissu yupo ki"theory" za siasa za ujamaa vs siasa za ubepari. Inapokuja kwenye uhalisia utashangaa mambo yalivyo tofauti.

Iko hivi, kilichofelisha ujamaa wa Nyerere sio kanuni kwamba mambo yakiendeshwa na serikali au yakifanywa kijamaa yanafeli. Kilichofelisha uchumi wa kijamaa ni kuwa nchi yetu iliingia kwenye siasa za ujamaa na kujitegemea nyakati idadi kubwa ya watu wake wana elimu na maarifa kiduchu kuendesha uchumi wa ushindani. Waliokuwa nyuma ya mafanikio ya kiuchumi aliyoyazungumzia Lissu kabla ya mfumo wa siasa za kijamaa za 1967 ni wazungu/wakoloni. Nyerere alipointroduce siasa zake za kijamaa wazungu wakajisepa (maana mzungu na ujamaa kwa mtu mweusi ni kama maji na mafuta - hawapatani).

Lakini kwa nchi yetu kwa wakati ule ujamaa ulikuwa haukwepeki. Hakuna nchi inayoweza kupiga hatua bila watu fulani wachache kujitoa mhanga kwa ajili ya wengi. Hata Ulaya na Marekani zinavyojitapa kwamba ni nchi za kibepari, hawakwambii yaliyojificha nyuma ya pazia. Nchi zile zilijengwa na watu waliojipinda kufanya kazi wakijitoa mhanga kwa gharama kubwa ikiwemo maisha yao kwa ajili ya nchi zao na vizazi vyao. Hata ukoloni na ajenda ya kutafuta makoloni ilikuwa ni watu wachache kuamua/kutumwa kuvuka mipaka ya nchi zao kwenda nchi za mbali kwenda kutafuta masoko ya viwanda vyao. Wapo watu wao wengi sana waliokufa baharini au kutokana na hali mbaya ya mazingira waliyokutana kwenye nchi za kigeni ikiwemo magonjwa kama malaria, n.k. kwa ajili ya nchi zao. Kama huo si ujamaa kwa ajili ya nchi zao ni kitu gani?

Sisi style yetu ya ujamaa ilikuwa ni kwa Nyerere kuweka mfumo kwamba watu wachache wenye nguvu zao, maarifa na elimu ya kutosha tuliokuwa nao mara tu baada ya uhuru wajitoe sadaka kufanya kazi kwa niaba ya wengi. Tatizo watu hawa walikuwa wachache mno. Na hapo ndio tulifeli. But idea kwamba ujamaa ni kitu kibaya si kweli na nchi zote za Magaharibi wana balance ujamaa na ubepari. Nchi za Scandnavia anazozitolea mfano Lissu ni very socialistic.

Tukirudi kwenye wazo la Lissu kwamba serikali ya Tanzania inatoza kodi utitiri na kudunisha wakulima, hizo ndio zinaitwa siasa za wanasiasa. Kiuhalisia, ukija kwenye ilani yake anayozungumza kwamba atajenga trams za treni jijini Dar, atawekeza kwenye renewable energy, atapandisha maslahi ya wafanyakazi/na kulipa malimbikizo, na blah blah nyinginezo, utashangaa kwamba gharama zake itambidi amnyonye mkulima mara kumi ya wanavyonyonywa sasa. Nimewachunguza wanasiasa wote na naweza kwambia Magufuli ni bonge la kiongozi. Huyu mzee ni very pragmatic katika sera zake -- toka mwanzo alivoingia Ikulu na kusoma hali ya uchumi wa nchi na mwenendo wake, hivi alivyofanya ndivyo ilibidi iwe. Hamna kudanganyana, watu lazima tujiongeze katika biashara, vilimo na shughuli zetu zote na serikali lazima ichukue kodi zake. Muhimu, ukitukamua kodi tunataka tuone huduma bora kutoka serikali yetu.
 
Lissu yupo ki"theory" za siasa za ujamaa vs siasa za ubepari. Inapokuja kwenye uhalisia utashangaa mambo yalivyo tofauti.

Iko hivi, kilichofelisha ujamaa wa Nyerere sio kanuni kwamba mambo yakiendeshwa na serikali au yakifanywa kijamaa yanafeli. Kilichofelisha uchumi wa kijamaa ni kuwa nchi yetu iliingia kwenye siasa za ujamaa na kujitegemea nyakati idadi kubwa ya watu wake wana elimu na maarifa kiduchu kuendesha uchumi wa ushindani. Waliokuwa nyuma ya mafanikio ya kiuchumi aliyoyazungumzia Lissu kabla ya mfumo wa siasa za kijamaa za 1967 ni wazungu/wakoloni. Nyerere alipointroduce siasa zake za kijamaa wazungu wakajisepa (maana mzungu na ujamaa ni kama maji na mafuta - hawapatani).

Well analyization
 
Tundu Lisu re uchumi
Uchumi uko wa aina mbili open economy ambayo nchi haiwezi ishi bila kutegemea nchi ingine

Aina ya pili ya uchumi ni closed economy ambapo nchi hukataa kuishi kwa kutegemea nchi nyingine kabisa
Nchi zote zilizoendelea zilianza na closed economy mfano China mwaka 1949 Mao tse Tung alitangaza mapinduzi ya kiutamaduni alifunga mipaka yote akasema kila kitu kinachohitajika china wachina wenyewe wagundue vingine wafe hakuna kuna ku mport wala kuexport chochote China iwe elimu au bidhaa au huduma

Wachina wakaingia kazini kugundua vitu kibao kuanzia dawa za kichina nk Baadaye uchumi wa china ukafunguliwa yeye ndio biggest exporter wa Bidhaa world wide anakopesha hadi marekani

Magufuli kuna vitu kufanya ni close economy ili ku save pesa za kigeni ili kujenga Maendeleo ya ndani badala ya hizo pesa kupelekwa nje kwa kisingizio cha semina,warsha na safari za Raisi na ujumbe wake ulaya na marekani
Hivi nani alikudanganya kuwa China kabla na wakati wa Mao hawakuwa na Teknolojia? Hafu soma historia vizuri wakati wa utawala wa Mao alipambana sana asipinduliwe kutokana na shida ambazo wananchi walizipata, Tanzania usiifananishe na China nchi ambayo ilisyaarabika kabla hata ya wazungu hawajui kuvaa nguo, China inarudi kule ilipokuwa katika Marne za zamani, Mwalimu Nyerere alifanya hiyo unayoita closed economy nchi ikafilisika na viwanda kufa, Watanzania hatuna purchasing power ya kutosha kununua bidhaa zote za viwandani
 
Wale genetically born Wana akili, Sasa we linganisha na watu wako hata kutengeneza choo hawaeezi wanajisaidia porini Kama ngedere,
Sisi bado Sana ku catch up na dunia inabidi tusaidiwe Kwanza Kuna generation zitakuja kustaarabika baadaye
Huu ni uongo sisi watanzania tuna akili sana cha msingi ni kujiamini na kujielimisha na kuwa na maarifa tu. Unajua pale microsoft kuna programmer mtanzania , na kunawatanzania wengi tu wanafanya makubwa ulaya, naomba usitudhalilishe tunao uwezo utegemezi tuukimbie kabisa Tunaomba Mungu atusimamie.
 
Lissu yupo ki"theory" za siasa za ujamaa vs siasa za ubepari. Inapokuja kwenye uhalisia utashangaa mambo yalivyo tofauti.

Iko hivi, kilichofelisha ujamaa wa Nyerere sio kanuni kwamba mambo yakiendeshwa na serikali au yakifanywa kijamaa yanafeli. Kilichofelisha uchumi wa kijamaa ni kuwa nchi yetu iliingia kwenye siasa za ujamaa na kujitegemea nyakati idadi kubwa ya watu wake wana elimu na maarifa kiduchu kuendesha uchumi wa ushindani. Waliokuwa nyuma ya mafanikio ya kiuchumi aliyoyazungumzia Lissu kabla ya mfumo wa siasa za kijamaa za 1967 ni wazungu/wakoloni. Nyerere alipointroduce siasa zake za kijamaa wazungu wakajisepa (maana mzungu na ujamaa ni kama maji na mafuta - hawapatani).

..Mwalimu aliwafukuza wafanyabiashara wakubwa na kutaifisha viwanda, mabenki, etc.

..watu hawakuondoka kwa hiari yao, walinyang'anywa mali na biashara zao.

..hatua hizo za utaifishaji za Mwalimu Nyerere zilisababisha zao kama la mkonge kuporomoka.

..zao hilo liliporomoka kwasababu Mwalimu Nyerere hakuwa na watu wenye ujuzi na uzoefu wa kuendesha mashamba, viwanda, na biashara ya mkonge.

..Na kipindi hicho Tanzania tulikuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa uzalishaji wa mkonge duniani.

..Mwalimu pia alianzisha mfumo wa vijiji vya ujamaa na mpango huo ulitiliwa mkazo mkubwa maeneo ya kusini mwa Tanzania.

..wananchi walikuwa wanahamishwa toka maeneo waliyoishi kwa muda mrefu, na kupelekwa maeneo mapya ya vijiji vya ujamaa.

..wakati wa zoezi hilo wako wananchi wengi waliacha mashamba yao ni kwenda maeneo mapya. mpango wa vijiji vya ujamaa ulisababisha kilimo kuathirika sana mikoa ya kusini na kupelekea zao la korosho kuporomoka.

..kuna viwanda vilikuwa vinafanya vizuri kabla ya zoezi la utaifishaji lakini navyo viliporomoka kwasababu walioteuliwa kuviongoza walikuwa hawana ujuzi wala uzoefu ktk kuendesha viwanda hivyo.

..Mwalimu hakutakiwa kutaifisha mali za watu, alichotakiwa kufanya ni kuanzisha makampuni ya serikali/umma yafanye kazi bega kwa bega na makampuni ya watu binafsi.

..Ni lazima tuwe wakweli kuhusu nini kilisababisha uchumi wetu ukaporomoka wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere.

NB:

..kipindi chote cha utawala wa Mwalimu Nyerere isipokuwa kipindi kifupi cha mwaka 1980--84 Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi zilizokuwa zikipokea misaada mingi zaidi kutoka nchi za magharibi.
 
Back
Top Bottom