zimmerman
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 1,644
- 3,176
Hiyo kauli ni zao la utumwa na ni matokeo ya kutawaliwa kiakili na ukoloni orijino na ukoloni mamboleo. Hakuna kitu kibaya kuwahi kutokea kwa mtu mweusi kama kutawaliwa na wazungu.
Ukoloni umetuathiri kiasi kwamba miaka 50 baada ya uhuru unaona vichembe vya kutawaliwa bado vipo. Hatujiamini, tunacheza beat ya mzungu kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kauli hii ya Lissu ni matokeo hayo hayo; nilishangaa juzi niliposikia Lissu kasoma sijui Marekani huko. Tusipokuwa makini katika elimu zetu hizi kufahamu kuwa elimu ya kikoloni ipo designed kuendelea kumformat mtu acheze beat ya kikoloni tutajikuta tunatumia visomo vyetu kumnufaisha mzungu badala ya kutunufaisha sisi, nchi zetu na watoto wetu.
Hivyo, ni kweli kwamba Tanzania inaihitaji dunia lakini hili halimaanishi kwamba ndio tuweke akili zetu mifukoni na kushindwa kung'amua ni maeneo gani tunaihitaji dunia bila kuathiri maslahi yetu mapana.