Tundu Lissu toa ushauri kusaidia Nchi ishinde kesi kimataifa na kufufua shirika la ndege

Tundu Lissu toa ushauri kusaidia Nchi ishinde kesi kimataifa na kufufua shirika la ndege

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom!

Mh Mwanasheria msomi Tundu Lissu, ninafuatilia sana ziara zako nchini,

Ni Kweli unafungua macho Watanzania juu ya yanayoendelea nchini,

Kwa sasa, Nchi yetu inazo ndege za kutosha zilizonunuliwa Kwa Kodi zetu, ndege hizo mara kadhaa zimedaiwa kukamatwa kisa kuvunja baadhi ya masharti ya kimataifa kuhusu nashauri Fulani Fulani.

Ninakuomba, kupitia majukwaa ya kisiasa, ueleze umma njia ambazo Nchi unaweza kuzitumia Ili tuondokane na kesi hizo ikibidi tumia usomi wako Nchi ishinde case hizo, ndege zetu zinufaishe Taifa uchumi wa Nchi ukue.

Ningependa nione kama Mtanzania mwenzio, ukitoa dira ya nini chama chako kitafaifanyia Nchi Kwa kutumia usomi na ubobevu wako katika Sheria. Hotuba zako zilenge Kutoa mawazo mbadala juu ya nini wewe na chama chako mtafanya Ili wananchi tuwapime.

Wananchi tungependa kusikia ukisema, ikiwa Watanzania wataichagua CHADEMA kuongoza Dola, mtahakikisha mnapeleka wataalamu kutetea Nchi na kuhakikisha nchi inashinda case zote zinazotukabili.

Napenda nikusikie katika Upande huo wa UZALENDO juu ya nchi Yako Tanzania.

Ni hayo tu ndugu Mzalendo TUNDU Antipas Mugwai Lissu, ubarikiwe.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni.
 
Swali fikirishi je kabla ya kuzinunua ndege hamkuandika andiko la biashara ,(andika la mradi)
Jikite kwenye future.

Yaliyopita hayatosaidia Nchi kwenda mbele,

Wananchi tunampenda kusikia CDM Ina MIKAKATI Gani na mipango Gani kulivusha Taifa?

Nakumbuka sana Dr Slaa, alikuwa akitoka way forward.
 
Ule msemo wa kudai, adui mwombee njaa kwetu hautasaidia,

Wananchi wote CCM, CDM na wasio na vyama, tunalipia ndege zilizopaki bila kufanya KAZI.

Lissu na CDM njooni na mpango MIKAKATI, Ili wananchi tuone tofauti yenu na hao CCM!!

..kwani sasa hivi huoni tofauti kati ya Ccm na Chadema?
 
Maji yamekuwa ya shingo nini? Wako wapi waliokiwa wanashangilia kununua ndege bila mpango, na wale wa mikataba ya siri?
Nafikiri hawezi kutoa ushauri wa kitaalamu bila kuona mkataba na mwenendo wa kesi. Kama kweli utaalamu wa Lissu unahitajika wahusika wanajua jinsi ya kum.engage.
 
Ununuzi wa hizo ndege enzi za Magufuli Tundu Lisu na wenzie Bungeni si ndo walikuwa wakipiga kelele mkaishia kusema wametumwa na mabeberu?,Au unataka kusema mmesahau?

Mliwashutumu wapinzani kwamba wametumwa na mabeberu halafu leo watu walewale mliowashutumu unataka wakusemee?

WATANZANIA WENGI WANAPASWA KUWA MIREMBE!
 
Jikite kwenye future.

Yaliyopita hayatosaidia Nchi kwenda mbele,

Wananchi tunampenda kusikia CDM Ina MIKAKATI Gani na mipango Gani kulivusha Taifa?

Nakumbuka sana Dr Slaa, alikuwa akitoka way forward.
Mimi siyo mwanacha wa Chama chochote ila ni mtaalamu wa elimu ya ujasiriamali karibu pia naandika kita cha ujasiriamali
 
Ununuzi wa hizo ndege enzi za Magufuli Tundu Lisu na wenzie Bungeni si ndo walikuwa wakipiga kelele mkaishia kusema wametumwa na mabeberu?,Au unataka kusema mmesahau?

Mliwashutumu wapinzani kwamba wametumwa na mabeberu halafu leo watu walewale mliowashutumu unataka wakusemee?

WATANZANIA WENGI WANAPASWA KUWA MIREMBE!
Leo hii wananchi wakiipa CDM kuongoza,

Watafanya nini kuhusu ndege zilizopaki?

Usinirudishe nyuma, nataka way forward, màana mkopo wa ndege hata Lissu analipa kama mtz.
 
Mimi siyo mwanacha wa Chama chochote ila ni mtaalamu wa elimu ya ujasiriamali karibu
Kodi Yako ilitumika kununua ndege, na zimepaki,

Unazilipia deni la mkopo na zimepaki,

Hapo ndipo unaibuka mzizi wa HOJA ya mada hapo juu kutaka kujua plan na way forward ya CDM kama chama kikuu Cha upinzani.

Karibu
 
..mpango wa Ccm ni upi?

..tuujue kwanza huo ili hata yakitolewa mapendekezo tuwe na cha kulinganisha.
 
Mimi siyo mwanacha wa Chama chochote ila ni mtaalamu wa elimu ya ujasiriamali karibu pia naandika kita cha ujasiriamali
Mimi pia Sina chama chochote Cha siasa,

Ni Mtanzania mlipa Kodi tu kama wewe,

Lakini Kwa kuwa Kodi yangu ilitumika kununua ndege ,ni gehitaji kujua kipi ni kipi na way forward ni nini.
 
Kodi Yako ilitumika kununua ndege, na zimepaki,

Unazilipia deni la mkopo na zimepaki,

Hapo ndipo unaibuka mzizi wa HOJA ya mada hapo juu kutaka kujua plan na way forward ya CDM kama chama kikuu Cha upinzani.

Karibu
This is a national issue, in reality though opposition parties are not involved in political decisions made by a ruling party, in this case ruling party is CCM (prevailing government)
 
..mpango wa Ccm ni upi?

..tuujue kwanza huo ili hata yakitolewa mapendekezo tuwe na cha kulinganisha.
Mimi ni Mtanzania Sina chama Cha siasa zaidi ya kuwa mtumishi wa Mungu, mlipa Kodi wa kawaida.

CCM hawana mpango wamelala USINGIZI fofofo.
 
Back
Top Bottom