Tundu Lissu toa ushauri kusaidia Nchi ishinde kesi kimataifa na kufufua shirika la ndege

Basi atoe mawazo mbadala kwamba Yeye na chama chake Wana mawazo Gani kuhusu ndege zilizopaki ambazo zilinunuliwa Kwa Kodi zetu na wananchi tunakamuliwa kulipa mikopo hiyo ilhali TIJA haionekani.
Wale ndege wamelala pale eapoti wanataga mayai, yakianza kutotoa Tanzania tutakuwa na ndege nyingi kuliko ulaya na tutawezesha wasanii wetu kutapakaa ulaya na asia.
 
Kwa wenzetu ushauri ni kazi na hulipiwa, mlipeni Tundu Lissu awashauri namna bora ya kuendesha Air Tanzania kwa faida na ndege zenu zisikamatwe kwa madeni.
Ni Kweli ushauri unalipiwa,

Lakini Kwa Lissu ni zaidi ya hapo, mtoto kumwomba mama amlipe pesa Ili kuziba ufa katika nyumba ya familia inayovuja , ni kukosa UZALENDO.

Maana sasa anazunguka Nchi nzima kuelimisha umma juu ya HAKI zao, halipwi hata mia.

Mwananchi ni muhimu kujitolea, Uzalendo uzidi. Amen
 
..kuna mtu nimesikia kuibuka na kesi ya miaka ya 60 anaidai serikali.

..serikali za Ccm zimefanya mambo ya kibwege sana ambayo yanaigharimu nchi.
Hao wafungua kesi Wana connection na watu wa serikalini Ili kuhujumu Taifa,

Jiulize mbona utawala wa Mkapa na Magu, hapakuwa na case za namna hiyo?

Lissu asaidie kuitaja chain hiyo na kuweka hadharani mipango Yao,

Ili hujuma Kwa Taifa ikome.
 
Salaam, Shalom!

Mh Mwanasheria msomi Tundu Lissu, ninafuatilia sana ziara zako nchini,

Ni Kweli unafungua macho Watanzania juu ya yanayoendelea nchini,

Kwa sasa, Nchi yetu inazo ndege za kutosha zilizonunuliwa Kwa Kodi zetu, ndege hizo mara kadhaa zimedaiwa kukamatwa kisa kuvunja baadhi ya masharti ya kimataifa kuhusu nashauri Fulani Fulani.

Ninakuomba, kupitia majukwaa ya kisiasa, ueleze umma njia ambazo Nchi unaweza kuzitumia Ili tuondokane na kesi hizo ikibidi tumia usomi wako Nchi ishinde case hizo, ndege zetu zinufaishe Taifa uchumi wa Nchi ukue.

Ningependa nione kama Mtanzania mwenzio, ukitoa dira ya nini chama chako kitafaifanyia Nchi Kwa kutumia usomi na ubobevu wako katika Sheria. Hotuba zako zilenge Kutoa mawazo mbadala juu ya nini wewe na chama chako mtafanya Ili wananchi tuwapime.

Wananchi tungependa kusikia ukisema, ikiwa Watanzania wataichagua CHADEMA kuongoza Dola, mtahakikisha mnapeleka wataalamu kutetea Nchi na kuhakikisha nchi inashinda case zote zinazotukabili.

Napenda nikusikie katika Upande huo wa UZALENDO juu ya nchi Yako Tanzania.

Ni hayo tu ndugu Mzalendo TUNDU Antipas Mugwai Lissu, ubarikiwe.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni.
Mambo ni mengi tatizo muda
 
Hao wafungua kesi Wana connection na watu wa serikalini Ili kuhujumu Taifa,

Jiulize mbona utawala wa Mkapa na Magu, hapakuwa na case za namna hiyo?

Lissu asaidie kuitaja chain hiyo na kuweka hadharani mipango Yao,

Ili hujuma Kwa Taifa ikome.
Mkuu Rabbon unapozidi kukomaa na hii mada jiulize swali la msingi kabisa: CCM wanataka kufufua ATCL?

Tafuta wataalamu wa biashara ya usafiri wa anga wakupe abc zote za hiyo biashara halafu upime mwenyewe kama yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika (toka awamu iliyopita) yanaashiria utashi wa watu wenye nia ya kufufua shirika la ndege.

Achana na kusaka ushauri wa Lissu na CHADEMA kuhusu hili suala. Hautakiwi kabisa. Walielezea mkakati wao mara kadhaa na kuuweka katika ilani lakini wamepuuzwa moja kwa moja. CCM na wananchi wake wanaendelea kushangilia “midege ya JPM” ya “hapa kazi tu” na “kazi iendelee”!

Kuhusu kesi, Lissu alishatoa ushauri concrete kwa dhihaka wakambandika nembo ya “tutashitakiwa MIGA”! Aseme nini tena?
 
Lissu kuwaza kuzikamata ndege zilizonunuliwa Kwa JASHO letu, hiyo Si sawa.

Kipimo Cha Uzalendo kinapunguka hapo.
 
Yeye alioneshwa uzalendo upi kwa kupigwa risasi ili afe?Uzalendo si wa upande mmoja tu.Kila upande uuoneshe huo uzalendo kwa vitendo.
 
Sasa ashambuliwe na wasiojulikana, hasira iweje aelekeze kwenye ndege zetu?

Ndege Si za wasiojulikana, ni Mali ya Watanzania maskini wavuja JASHO.
 
Hebu tumia akili zako kadiri ya uwezo wako wewe!Mpaka leo kichwani mwako kuna neno "wasiojulikana"?
 
Lissu kuwaza kuzikamata ndege zilizonunuliwa Kwa JASHO letu, hiyo Si sawa.

Kipimo Cha Uzalendo kinapunguka hapo.
Waliotaka kumuua ndio wazalendo? Tuache masihara kwenye uhai wa mtu.

Afrika hatuko serioua ndio maana mtu anaweza kuwatamkia wanaotekwa na kuuawa kuwa wanafanya masihara. Yaani unataka kuniua na umenikosa kosa risasi ila nikikamata ndege zako mimi ndio nionekane mbaya ila wew
we je? Come on!!
 
Sasa ashambuliwe na wasiojulikana, hasira iweje aelekeze kwenye ndege zetu?

Ndege Si za wasiojulikana, ni Mali ya Watanzania maskini wavuja JASHO.
We najamaa nilikuwa naliona unajielewa kumbe wewe ni wale wale. Hizo ndege ulishawahi kupanda? Ni zenu wewe na nani?
 
Waliotaka kumuua ndio wazalendo? Tuache masihara kwenye uhai wa mtu.

Afrika hatuko serioua ndio maana mtu anaweza kuwatamkia wanaotekwa na kuuawa kuwa wanafanya masihara. Yaani unataka kuniua na umenikosa kosa risasi ila nikikamata ndege zako mimi ndio nionekane mbaya ila wew
we je? Come on!!
Watanzania maskini walipakodi hawakuhusika kumshambulia Lissu.

Hapo Kuna kundi Fulani analitumikia kufanikisha maslah Fulani.
 
We najamaa nilikuwa naliona unajielewa kumbe wewe ni wale wale. Hizo ndege ulishawahi kupanda? Ni zenu wewe na nani?
Ndege ni zetu zimenunuliwa Kwa Kodi zetu, mikopo hiyo tutalipisgwa sie.

Karibu.
 
Salaam, Shalom!

Mh Mwanasheria msomi Tundu Lissu, ninafuatilia sana ziara zako nchini,

Ni Kweli unafungua macho Watanzania juu ya yanayoendelea nchini,

Kwa sasa, Nchi yetu inazo ndege za kutosha zilizonunuliwa Kwa Kodi zetu, ndege hizo mara kadhaa zimedaiwa kukamatwa kisa kuvunja baadhi ya masharti ya kimataifa kuhusu nashauri Fulani Fulani.

Ninakuomba, kupitia majukwaa ya kisiasa, ueleze umma njia ambazo Nchi unaweza kuzitumia Ili tuondokane na kesi hizo ikibidi tumia usomi wako Nchi ishinde case hizo, ndege zetu zinufaishe Taifa uchumi wa Nchi ukue.

Ningependa nione kama Mtanzania mwenzio, ukitoa dira ya nini chama chako kitafaifanyia Nchi Kwa kutumia usomi na ubobevu wako katika Sheria. Hotuba zako zilenge Kutoa mawazo mbadala juu ya nini wewe na chama chako mtafanya Ili wananchi tuwapime.

Wananchi tungependa kusikia ukisema, ikiwa Watanzania wataichagua CHADEMA kuongoza Dola, mtahakikisha mnapeleka wataalamu kutetea Nchi na kuhakikisha nchi inashinda case zote zinazotukabili.

Napenda nikusikie katika Upande huo wa UZALENDO juu ya nchi Yako Tanzania.

Ni hayo tu ndugu Mzalendo TUNDU Antipas Mugwai Lissu, ubarikiwe.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni.
Suluhisho ni kufuata sheria za Kitaifa na Kimataifa na kulinda haki na uhai wa binadamu.
 
Back
Top Bottom