Pre GE2025 Tundu Lissu: Tubadilishe tarehe ya Uchaguzi Mkuu kwa Miaka miwili ili tuwe na tume Huru

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kuendelea kufanya uchaguzi ambao hauna maana yoyote ni ujing na kupotezeana muda, tunakubaliana bora Samia aendelee kutawala atakavyo kuliko kutumia hela za umma na tutuchosha bure wananchi kufanya uchaguzi usio na maana yoyote ile.

Lissu yupo sahihi, aungwe mkono na wote wenye akili timamu.
 
mtanzania wa kweli mzalendo aliyejitoa maisha yako kwaajili ya wananchi maskini
Mtanzania wa kweli? Familia yake ni raia wa USA, yeye anaishi Ubeleji, utamwitaje Mtanzania wa kweli? Wewe na mimi wenye familia na ndugu zetu hapa tutaitwaje sasa?
 
Reactions: Tui
Mtanzania wa kweli? Familia yake ni raia wa USA, yeye anaishi Ubeleji, utamwitaje Mtanzania wa kweli? Wewe na mimi wenye familia na ndugu zetu hapa tutaitwaje sasa?
Uraia wa Tundu Lisu hauna mashaka yoyote, labda kwa nyie wafuasi wa siasa chafu. Na kuhusu familia yake kuishi US huo ni uamuzi wa familia. Hata sisi wengi ni kwakuwa hatuna connections za huko, ila tungekuwa nazo watoto wetu wangekuwa huko wakipata elimu bora.
 
Hii move ya NO REFORM NO ELECTION haita fanikiwa,ni vyema CHADEMA wangejiandaa tu na Uchaguzi ,wakaambulie chochote kitu kiwape nguvu za kupambana zaidi.

Mbaya zaidi hawana plan B endapo hyo movement ya No reform No election isipo fanikiwa,
 
Nini kifanyike?
 
Nini unataka kifanyike?
 
Serikali ya CCM HAIWEZI kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uchaguzi Mkuu upo palepale.
 
Kwa hiyo Rais, wabunge ( pamoja na wakina Halima) na madiwani waliopo nao waongezewe muda? Kiinua mgongo cha wabunge nacho kiongezwe? Na muda gani utatosha kufanya hayo marekebisho anayotaka?

Halafu theluthi mbili za wabunge hawa wa sasa ndio wapitishe Katiba Mpya au mabadiliko yeyote ya Katiba iliyopo?

Au kuna njia nyingine ya kubadilisha Katiba bila kupeleka rasimu Bungeni?

Amandla...
 
Atakayejaribu kufuata maelekezo ya huyo mjinga akawadhuru wasimamizi wa uchaguzi, aagane kabisa na familia yake. Udhurike kwa sababu mtu ana tamaa ya madaraka?
 
Anataka Samia aendelee kuwa Rais huyu.
 

..hizo ndizo gharama ambazo CCM imetuingiza kwa kuchelewa kufanya mabadiliko ya maana ktk sheria zetu za uchaguzi.

..nadhani kukiwa na nia njema kuanzia sasa hivi tunaweza kutumia muda mfupi kufanya mabadiliko kuliko huo anaopendekeza Tundu Lissu.
 
Hivi CCM hampendi Uchaguzi wa haki na wazi,wenye kusimamiwa na chombo huru pasipo kuua wale kuteka wananchi??...kumbukeni huwa mnaenda ibadani kila siku wengine Makka na Israel kuhiji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…