Pre GE2025 Tundu Lissu: Tubadilishe tarehe ya Uchaguzi Mkuu kwa Miaka miwili ili tuwe na tume Huru

Pre GE2025 Tundu Lissu: Tubadilishe tarehe ya Uchaguzi Mkuu kwa Miaka miwili ili tuwe na tume Huru

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kuendelea kufanya uchaguzi ambao hauna maana yoyote ni ujing na kupotezeana muda, tunakubaliana bora Samia aendelee kutawala atakavyo kuliko kutumia hela za umma na tutuchosha bure wananchi kufanya uchaguzi usio na maana yoyote ile.

Lissu yupo sahihi, aungwe mkono na wote wenye akili timamu.
 
mtanzania wa kweli mzalendo aliyejitoa maisha yako kwaajili ya wananchi maskini
Mtanzania wa kweli? Familia yake ni raia wa USA, yeye anaishi Ubeleji, utamwitaje Mtanzania wa kweli? Wewe na mimi wenye familia na ndugu zetu hapa tutaitwaje sasa?
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Mtanzania wa kweli? Familia yake ni raia wa USA, yeye anaishi Ubeleji, utamwitaje Mtanzania wa kweli? Wewe na mimi wenye familia na ndugu zetu hapa tutaitwaje sasa?
Uraia wa Tundu Lisu hauna mashaka yoyote, labda kwa nyie wafuasi wa siasa chafu. Na kuhusu familia yake kuishi US huo ni uamuzi wa familia. Hata sisi wengi ni kwakuwa hatuna connections za huko, ila tungekuwa nazo watoto wetu wangekuwa huko wakipata elimu bora.
 
Hii move ya NO REFORM NO ELECTION haita fanikiwa,ni vyema CHADEMA wangejiandaa tu na Uchaguzi ,wakaambulie chochote kitu kiwape nguvu za kupambana zaidi.

Mbaya zaidi hawana plan B endapo hyo movement ya No reform No election isipo fanikiwa,
 
Hayo mawazo ya kijinga sana yani umeshasikia Ngorongoro imeuzwa, Bandari ya DAR imeuzwa, Bandari ya Bagamoyo imeuzwa, ufisadi kila mahali fedha zinatoroshwa nje ya nchi, Bunge halitetea wananchi linatunga sheria mbovu za kuuza mali za tanganyika, alafu unasema waendelee kubaki madarakani kwa miaka mingine miwili? Tundu Lisu unaanza kuwapa mashaka watanzania unakuwa huna tofauti na mboe
Nini kifanyike?
 
Nini unataka kifanyike?
 
Serikali ya CCM HAIWEZI kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uchaguzi Mkuu upo palepale.
 
Tundu Lissu: Tubadilishe tarehe ya Uchaguzi Mkuu kwa Miaka miwili ili tuwe na tume Huru.
View attachment 3237191
Waati akihutubia Maelfu ya Watu huko Mkoani Singida hii leo, amesema Uchaguzi uahirishwe.

Amesema kuliko kufanya Uchaguzi katika mazingira haya ya sasa, Bora tarehe ya Uchaguzi isogezwe mbele kwani tarehe zimepangwa na binadamu.

Amedai kwamba CCM wanadai muda hautoshi wa kupitia katiba na sheria, kanuni za tume huru ya Uchaguzi. Kakubaliana na hali hiyo, ila akapendekeza kwasababu hiyo, bora tarehe isigogezwe mbele lakini sheria ifanyiwe marekebisho.

Tundu Lissu kadai bila mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi hakutakuwa na Uchaguzi
View attachment 3237199
Pia Kohoji kwanini Mawakala wanaosimamia Uchaguzi wanaapa kwa Mkurugenzi kuficha siri, ni siri gani hiyo wanaoyoficha? Ya wizi wa kura?

Kasema hataki tena mambo ya kuapa kwa Mkurugenzi, Mambo ya Polisi kuingia vituo vya kupigia kura kwanini ndo wanaingiza kura feki
View attachment 3237163View attachment 3237164View attachment 3237165
Kwa hiyo Rais, wabunge ( pamoja na wakina Halima) na madiwani waliopo nao waongezewe muda? Kiinua mgongo cha wabunge nacho kiongezwe? Na muda gani utatosha kufanya hayo marekebisho anayotaka?

Halafu theluthi mbili za wabunge hawa wa sasa ndio wapitishe Katiba Mpya au mabadiliko yeyote ya Katiba iliyopo?

Au kuna njia nyingine ya kubadilisha Katiba bila kupeleka rasimu Bungeni?

Amandla...
 
Atakayejaribu kufuata maelekezo ya huyo mjinga akawadhuru wasimamizi wa uchaguzi, aagane kabisa na familia yake. Udhurike kwa sababu mtu ana tamaa ya madaraka?
 
Kwa hiyo Rais, wabunge ( pamoja na wakina Halima) na madiwani waliopo nao waongezewe muda? Kiinua mgongo cha wabunge nacho kiongezwe? Na muda gani utatosha kufanya hayo marekebisho anayotaka?

Halafu theluthi mbili za wabunge hawa wa sasa ndio wapitishe Katiba Mpya au mabadiliko yeyote ya Katiba iliyopo?

Au kuna njia nyingine ya kubadilisha Katiba bila kupeleka rasimu Bungeni?

Amandla...
Anataka Samia aendelee kuwa Rais huyu.
 
..hizo ndizo gharama ambazo CCM imetuingiza kwa kuchelewa kufanya mabadiliko ya maana ktk sheria zetu za uchaguzi.

..nadhani kukiwa na nia njema kuanzia sasa hivi tunaweza kutumia muda mfupi kufanya mabadiliko kuliko huo anaopendekeza Tundu Lissu.
 
Hivi CCM hampendi Uchaguzi wa haki na wazi,wenye kusimamiwa na chombo huru pasipo kuua wale kuteka wananchi??...kumbukeni huwa mnaenda ibadani kila siku wengine Makka na Israel kuhiji
 
Back
Top Bottom