Tundu Lissu tumia ujuzi wako wa sheria ndege iliyokamatwa iachiwe

Tundu Lissu tumia ujuzi wako wa sheria ndege iliyokamatwa iachiwe

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
3,891
Reaction score
8,448
Watanzania hawana haja ya kuteseka kuhusiana na kukamatwa kwa ndege ya Air Tanzania ambayo imefikisha miezi 6 sasa bila kuachiwa kwani walitumia kodi zao kusomesha wasomi wazuri wa sheria wenye uwezo wa kutetea hadi makampuni ya nje kama Acacia akina Tundu Lisu na wenzake.

Kwenye awamu ya tano kila ndege inapokamatwa Rais Magufuli alikuwa anamtuma Prof Kabudi na ndege zilikuwa zinaachiwa kwa kasi ya ajabu ndani ya mwezi mmoja kwa kutumia ujuzi wake wa sheria aliosomea kwa kodi za watanzania, leo kwenye awamu ya sita Prof. Kabudi ametumbuliwa hayupo.

Kwa kuwa Chadema wameamua kulamba asali na kuungana na awamu ya 6 basi tunamuomba Rais Samia amtume Tundu Lisu aende akaikomboe hiyo ndege kwani uzalendo wa Lisu utapimwa kwa kuwatetea watanzania na siyo kutetea kampuni la Acacia.
 
Mna mu overate Tundu Lissu kama mwanasheria.
Huyu hajui Company Law, bali nimwanasheria wa haki za binadamu.
Kuna vitu vya sheria TL hajui kabisa.
Mbona aliandika kitabu juu ya masuala ya sheria zinazosimamia mikataba ya madini hasa eneo la Kodi. Unaweza kweli kuchambua makampuni na sheria zinazowalinda bila kujua sheria yenyewe?!

Najua hii mada ni sarcastic lakini kusema Lissu hajui company law ambayo hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza anajua is purely underrating a lawyer from University of Warwick.

Prof.Wajackoyah mwenyewe anakiri Lissu alikua one of the best pale chuoni then a nobody humu JF unajifanya unaelewa academic brilliance ya Lissu?!
 
Mbona aliandika kitabu juu ya masuala ya sheria zinazosimamia mikataba ya madini hasa eneo la Kodi. Unaweza kweli kuchambua makampuni na sheria zinazowalinda bila kujua sheria yenyewe?!

Najua hii mada ni sarcastic lakini kusema Lissu hajui company law ambayo hata mwanafunzi wa kwanza anajua ni underating a lawyer from University of Warwick.

Prof.Wajackoyah mwenyewe anakiri Lissu alikua one of the best pale chuoni then a nobody humu JF unajifanya unaelewa academic brilliance ya Lissu?!
Prof Kabudi ndege ziliachiwa bila shida.

Sheria ya Tundu Lisu anaitumiaga kwa manufaa ya nani? Miga na Acacia?
 
Watanzania hawana haja ya kuteseka kuhusiana na kukamatwa kwa ndege ya Air Tanzania ambayo imefikisha miezi 6 sasa bila kuachiwa kwani walitumia kodi zao kusomesha wasomi wazuri wa sheria wenye uwezo wa kutetea hadi makampuni ya nje kama Acacia akina Tundu Lisu na wenzake.

Kwenye awamu ya tano kila ndege inapokamatwa Rais Magufuli alikuwa anamtuma Prof Kabudi na ndege zilikuwa zinaachiwa kwa kasi ya ajabu ndani ya mwezi mmoja kwa kutumia ujuzi wake wa sheria aliosomea kwa kodi za watanzania, leo kwenye awamu ya sita Prof Kabudi ametumbuliwa hayupo.

Kwa kuwa Chadema wameamua kulamba asali na kuungana na awamu ya 6 basi tunamuomba Rais Samia amtume Tundu Lisu aende akaikomboe hiyo ndege kwani uzalendo wa Lisu utapimwa kwa kuwatetea watanzania na siyo kutetea kampuni la Acacia.
kwani Lisu ni mwanasheria mkuu wa serikali?
 
Sheria ya Tundu Lisu anaitumiaga kwa manufaa ya nani? Miga na Acacia?
1. Sheria yake aliiitumia sana kupinga utapeli wa mabeberu kwenye madini hasa maeneo ya huko Tulawaka mpaka kule Nyamongo.

2. Aliwahi kusaidia directly kuwatoa gerezani zaidi ya watu 400 waliokua na kesi mbali mbali na kutupwa ndani kisa migogoro na migodi.

3. Sio hapo tu alikua LEAT ambapo walikua wanasheria wanapigania masuala ya mazingira hasa kupinga maviwanda yanayotiririsha Maji ya sumu kwenye vyanzo vya makazi ya watu.
 
Back
Top Bottom