Tundu Lissu: Tutazipima kauli za Kikwete kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala!

Tundu ni kamanda wa ukweli huwa anani inspire sana anaitendea haki masters degree yake ya law
hakuna kulala mpaka kieleweke
 
Hata Jaji mkuu wa Kenya amemtaja Mh Tundu Lissu kama mmoja wa Wanasheria vijana wanaoijua sheria Afrika mashariki. Nitaweka link soon. Big up Mh Tundu Antipass Mugwai Lissu, Jk hana ubavu wa ku argue na wewe.
 
Hata mzazi wako anaweza kuwa mzandiki lazima Useme ukweli! Mzandiki ni mzandiki tu! Lissu ni mzandiki aseme wajumbe wa kutoka TEC au CCT wapo au hawapo kwenye tume ya Jaji Warioba

wapo wasioteuliwa na TEC naCCT majina hayo Jk kayatoa anakojua mwenyewe yale matatu aliyopewa hakuteua.
 
mimi tangu mwanzo niliona hawa ma ccm , kuna mtu alitakiwa kudanganywa lakini hadanganyiki(tundu lisu)
 

Tangu nimeanza kusikia hoja za Serikali sijapata kusikia Serikali mekili udhaifu wake hata pale ambapo kuna shida. Nani anieleze au aseme wazi lini serikali iliwahi kukiri mapungufu yake pale ilipokwenda kinyume hata cha sheria? Imetokea mauaji na mateso watu wamepanda vyeo baada hata ya wanaharakati kupiga kelele juu ya hayo mauaji.

Hata pale walipoona kuna mateso na ukatili wa aina mbalimbali hapa nchini jeshi limeendeleza aina fulani za senema tu bila kuwapata wahusika na kuwafikisha mahala panapohusika.

Wakati fulani kulitokea mauaji ya mbwa wa serikali/polisi wahusika walitafutwa hadi kupatikana na kushughulikiwa kikamilifu. Inakuwaje leo hili la katiba litendewe haki kama linavyohitajika kuwa? NITASHANGAA SANA KAMA ITAKUWA HIVYO....

HII NDO BONGO BWANA, THE WRONGS ARE ALWAYS RIGHT.... LABDA IPO SIKU MUNGU ATATUSIKIA....
 
Amemfundisha spika sheria,amemfundisha mwanasheria wa serikali sheria, amemfundisha waziri mkuu sheria, amewafundisha kina ndugai, wasira, lukuvi, nk. "na sasa anamfundisha rais wetu sheria. Jamani si aongezewe mshahara

naomba makamanda wamwongezee ulinzi maana magamba watamtaftia watu wa kumlimboka. Maana Akina ighondu ni balaa
 
haya ya kikwete na lisu,yana maslahi kwa taifa hili?kj kutumia hotuba kumshambulia raia mmoja kwa hoja alizozitoa tena ndani ya bunge hiyo ni busara?ni vema angewaachia akina lusinde,nkamia na komba waendelee kumsemea yale aliyoyataka kusema kwa lisu ila hayapaswi kutokea kwenye mdomo wa rais wa nchi
 
Mkuu Mbelwa umenena,japo CCM hawawezi kukiri hadharani lakini wakiwa vyumbani mwao wanajisemea kimoyo moyo.......Lissu ni mwalimu wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…