Tundu Lissu: Tutazipima kauli za Kikwete kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala!

Rais ana nia njema sana ula nina mashaka makubwa sana na washwaauri wake, Washauri wa rais wanatakiwa kuwa makini sana na mustakabali wa hii nchi yetu, kinyume na hivyo Ccm ndio itakuwa ya kwanza kuharibu amani yetu
 

Smart Lissu

Ameamua kuwalaumu waliomwambia, waliomjulisha na waliomsikilizisha Raisi maneno...hivyo Kamsafisha Raisi huku akiwacharaza vibaya walio karibu na Raisi, wale wanaoiaminisha ati kazi yao ni kumshauri raisi...Bila shaka washauri wa Raisi wanakabiliwa na msongo mbaya wa mawazo kwa kuchelewesha ukweli unaoibuliwa kiulaini na Mh Lissu.

kazi iko
 
Nahisi JK anapelekeshwa vibaya sana na wapambe wake. Hivi hao wapambe wanafurahi nini kumwona boss wao akifadhaika kwa maneno aliyokwisha toa bila kutafakari ukweli wake? Huo unaitwa mkenge. Wapambe saa hii wanakunywa wisky wakichekelea jinsi boss wao alivyoropoka. President hapaswi kumsema mtu.
 

Al Shaymar hakupendekezwa na shirikisho la vyama vya wenye ulemavu, sasa unaweza kutuambia raisi Kikwete alilitoa wapi jina lake hadi akamteua kuwawakilisha walemavu?

Buku saba fc mnafikiri Tundu Lissu anabahatisha? Alipowaambia kuwa kuna majaji vihiyo wameteuliwa na raisi Kikwwte kwasababu za ushikaji mkabisha hivihivi, alipoweka hadharani majina yao mkapoteana.
 

" Lissu ajibu



Akizungumza na gazeti hili (Tanzania Daima), Lissu amehoji hotuba ya Rais Kikwete iliyojaa neno "nimeambiwa" akisema ana uhakika gani wale waliomwambia kama hawakumdanganya?


"Maneno yaliyotajwa na rais kuhusu uteuzi wa wajumbe toka Shirikisho la Vyama vya Wenye Ulemavu, TEC na CCT yalizungumzwa kwenye kamati sio maneno yangu. Kikwete hakuwepo kwenye kamati, mimi nilikuwepo. Sasa mawaziri wake na wabunge wake wa CCM wamwambie ukweli, waache kumdanganya.



"Kikwete amesema mimi ni muongo, mnafiki, lakini hoja ambazo tulizipinga mfano ya ushiriki wa wadau wa Zanzibar, hata Waziri wa Sheria na Katiba wa Zanzibar, Abubakari Khamisi naye ameniunga mkono. Je, na huyu ni mzushi, muongo na mfitini?" alihoji.


Aliongeza kuwa hoja ambayo rais anakimbilia kwamba alimzuia asiteue wajumbe 166, ilikuja bungeni mwaka 2011, wakaipinga, ikaondolewa. Lakini mwaka huu wameirejesha tena"

nukuu hii toka Gazeti la Tanzania Daima Jumapili
 
Huyo ni muongo tu hata aitishe press conference ya dunia nzima. TEC na CCT wameshirikishwa au hawakushirikishwa?
kiukweli watu wa TEC na CcT wanalalamika hivo, kuwa mtu aliyechukuliwa ni tofauti na mapendekezo yao! Jk aangalie sana hao washauri wake!
 
Lissu anashindana na tembo...

Mkuu pole na majukum.

Tatizo sio ukubwa wa tembo bali madhara anayoweza yapata tembo, mbona bastola ni kitu kidogo nacho huangusha mijitu?

Je hoja za lisu zinaukweli? kama sivo kikwete apuuzie na atie saini, Huku tanganyika hakuna shida maana niupepo utapita

Kule zanzibar .....Allah-akbar, kikwete atajuta na maisha yake yote atajilaum kwanini alimpuuza Lisu.

Anawapuuza wazenji????...take it pu Ritz
 
Mwenyeezi Mungu hamfichi mnafik, uyaseme wewe yaliyo moyoni mwako uwasingizie wengine, Unanchekesha!



1. Je ni kweli wazanzibar kupitia taasisi zao wameshirikishwa? mojawapo ya hoja za Lisu-unaweza kututhibitishia

2. Je ni kweli kunavipengele takribani 6-vimeingizwa kinyemela bila wenzentu wa zanzibar kushirikishwa?-Lisu

Tuutafute ukweli kwenye haya kwanza.....FaizaFoxy kunaukweli wowote hapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…