Wakuu kamanda Lissu anafanya press, sasa hivi Makao Makuu ya Chadema na haya ndiyo amezungumza;
- Wadau wa Zanzibar hawajashirikishwa hata kidogo na hawakuwepo kwenye ratiba ya Kamati.
- Kamati ilipanga kwenda Zanzibar kutembea na sio kuonana na wadau, kwa sabab walitakiwa pkutembelea miradi ya TASAF, OFISI YA MAKAMU WA RAIS NA OFISI YA BUNGE.
- Wakakataa na kuomba kwa katibu wa Bunge kuwaona wadau wa Zanziba, Katibu wa Bunge alikubali.
- Walitengeneza orodha ya wadau.
- Yalianza maneno pembeni kuwa hakuna usalama Zanzibar wakati huohuo Kamati ya Ulinzi na Usalama ilikuwa Zanzibar.
- Wakazuiliwa kwenda na hivyo hakuna mdau wa Zanzibar aliyehusishwa.
- Kama haya ni makosa uzandiki na unafiki unatoka wapi wakati hoja ya kwenda Zanzibar yeye aliyeitoa?
Nitaendelea kuwapa update
- Kama hakuna ulazima kwa mujibu wa kanuni kwenda Zanzibar ofisi ndogo za Bunge Zanzibar zina maana gani, kwa hili rais amepotoka na hajui analolifanya.
- Hawajawahi kukutana na mjumbe wa Baraza la wawakilishi Zanzibar, na hata M/sheria amekiri.
UTEUZI KWENYE TUME YA KATIBA
- Hoja ni mamlaka ya Rais kuteua wajumbe 166
- Walipinga 2011 Ikaondolewa na wakairudisha tena kwenye muswada huu
- Uteuzi wa wajumbe wa Tume usilinganishwe na uteuzi wa wajumbe wa Bunge la Katiba. Ushahidi wa TEC , CCT na Shirikisho la walemavu kutoteuliwa pamoja na kupeleka majina kwa Rais ulitolewa kwenye Kamati ya Bunge, uongo wake unatoka wapi?
- Shirikisho la walemavu halikumpendekeza Al Shaimar Kwegir na hivyo Rais aliteua watu alkyewaona yeye wanafaa. Uongo unatoka wapi?
Maneno ya Rais,
- Hatamuita mzindiki, mnafiki wala mwongo ila ametoa hitimisho kwa maneno ya sikia sema (hearsay) kwa sababu ametumia maneno "nimeambiwa, nimesikia na nimejulishwa" mara tisa kwenye hotuba yake.
Kuhusu kuwa na mazungumzo ya pamoja;
- Kama ana nia njema basi asiusaini muswada na Katiba inamruhusu kufanya hivyo.
- Akiusaini ataendekeza mambo ya kiccm na hana haja ya kuaminiwa tena.
- Kamati ya Sheria na Utawala ya Bunge inakutana kuanzia kesho na hivyo anasubiri sheria husika iliyopitishwa kinyemela kurudishwa Bungeni.
Mwisho. Anakaribisha maswali;
- Ukiwa na mchakato mbovu yatatokea mambo kama ya Zimbabwa miaka 16 ndiyo ikapata Katiba na Kenya miaka 11 ndipo wakapata Katiba, kwa sababu mwanzoni hakukuwa na mchakato shirikishi.
- Wanachokifanya CCM sasa ndicho walichokifanya KANU kule Kenya
- Wananchi hawatanyamaza kamwe katika mchakato huu.