Tundu Lissu: Tutazipima kauli za Kikwete kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala!

Tundu Lissu: Tutazipima kauli za Kikwete kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala!

Rais hajakosea ni kweli 'aliambiwa' 'amekisia', 'amefahamishwa'. Hoja ni nani waliomwambia na kumfahamisha. Bila shaka ni mawaziri na wasaidizi wake bungeni. Hapa lazama kuna alipata briefing kutoka kwa watu kama mzee wa kanuni za 64, mzee tyson na wengineo. Je, tuligemea wamwambie au wamfahamishe nini? Akili za kuambiwa, changanya na za kwako!

Wakuu kamanda Lissu anafanya press, sasa hivi Makao Makuu ya Chadema na haya ndiyo amezungumza;

- Wadau wa Zanzibar hawajashirikishwa hata kidogo na hawakuwepo kwenye ratiba ya Kamati.
- Kamati ilipanga kwenda Zanzibar kutembea na sio kuonana na wadau, kwa sabab walitakiwa pkutembelea miradi ya TASAF, OFISI YA MAKAMU WA RAIS NA OFISI YA BUNGE.
- Wakakataa na kuomba kwa katibu wa Bunge kuwaona wadau wa Zanziba, Katibu wa Bunge alikubali.
- Walitengeneza orodha ya wadau.
- Yalianza maneno pembeni kuwa hakuna usalama Zanzibar wakati huohuo Kamati ya Ulinzi na Usalama ilikuwa Zanzibar.
- Wakazuiliwa kwenda na hivyo hakuna mdau wa Zanzibar aliyehusishwa.
- Kama haya ni makosa uzandiki na unafiki unatoka wapi wakati hoja ya kwenda Zanzibar yeye aliyeitoa?

Nitaendelea kuwapa update

- Kama hakuna ulazima kwa mujibu wa kanuni kwenda Zanzibar ofisi ndogo za Bunge Zanzibar zina maana gani, kwa hili rais amepotoka na hajui analolifanya.
- Hawajawahi kukutana na mjumbe wa Baraza la wawakilishi Zanzibar, na hata M/sheria amekiri.
UTEUZI KWENYE TUME YA KATIBA
- Hoja ni mamlaka ya Rais kuteua wajumbe 166
- Walipinga 2011 Ikaondolewa na wakairudisha tena kwenye muswada huu
- Uteuzi wa wajumbe wa Tume usilinganishwe na uteuzi wa wajumbe wa Bunge la Katiba. Ushahidi wa TEC , CCT na Shirikisho la walemavu kutoteuliwa pamoja na kupeleka majina kwa Rais ulitolewa kwenye Kamati ya Bunge, uongo wake unatoka wapi?
- Shirikisho la walemavu halikumpendekeza Al Shaimar Kwegir na hivyo Rais aliteua watu alkyewaona yeye wanafaa. Uongo unatoka wapi?

Maneno ya Rais,
- Hatamuita mzindiki, mnafiki wala mwongo ila ametoa hitimisho kwa maneno ya sikia sema (hearsay) kwa sababu ametumia maneno "nimeambiwa, nimesikia na nimejulishwa" mara tisa kwenye hotuba yake.

Kuhusu kuwa na mazungumzo ya pamoja;
- Kama ana nia njema basi asiusaini muswada na Katiba inamruhusu kufanya hivyo.
- Akiusaini ataendekeza mambo ya kiccm na hana haja ya kuaminiwa tena.
- Kamati ya Sheria na Utawala ya Bunge inakutana kuanzia kesho na hivyo anasubiri sheria husika iliyopitishwa kinyemela kurudishwa Bungeni.

Mwisho. Anakaribisha maswali;

- Ukiwa na mchakato mbovu yatatokea mambo kama ya Zimbabwa miaka 16 ndiyo ikapata Katiba na Kenya miaka 11 ndipo wakapata Katiba, kwa sababu mwanzoni hakukuwa na mchakato shirikishi.
- Wanachokifanya CCM sasa ndicho walichokifanya KANU kule Kenya
- Wananchi hawatanyamaza kamwe katika mchakato huu.
 
- Kwa hiyo Tundu Lissu alitegemea Rais wa Jamhuri aamuliwe nani wa kumchagua kwenye kamati na hivyo vyama uchwara ndio katiba itakuwa sawa? duh!!

Le Mutuz
 
Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu amesema hotuba ya kila mwezi ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa siku tatu zilizopita, imejaa maneno mengi ya kuambiwa hasa kuhusu mchakato wa Katiba Mpya, ikiwa ni pamoja na uteuzi alioufanya wa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za makao makuu wa Chadema, Lissu alisema kauli zilizotolewa na Rais za kumshutumu yeye (Lissu) kuzungumza uongo bungeni, kuhusu uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba zilikuwa zakuambiwa, hazina ukweli wowote.

“Pengine rais Kikwete angesoma hotuba yangu niliyoitoa bungeni asingezungumza vile kuhusu mimi.”

Katika hotuba yake, Rais Kikwete alimshutumu Lissu kwa kusema kwamba katika uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa Rais hakuheshimu mawazo ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).

Rais Kikwete alisema kauli hiyo ya Lissu ni uzushi, uongo na uzandiki wa hali ya juu huku akisisitiza kuwa Lissu alitoa kauli hiyo ili kupotosha ukweli na pengine isaidie kujenga hoja yake ya kutaka Rais asiteue wajumbe 166 wa Bunge Maalum la Katiba.

Katika maelezo yake ya jana, Lissu alisema kuwa alipinga Rais kuteua wajumbe wa Bunge la Katiba kwa sababu hata wakati akiteua wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba baada ya kupelekewa majina na taasisi mbalimbali, alifanya uteuzi wa watu ambao hawakupendekezwa na taasisi mbalimbali, ikiwemo TEC na CCT.

Lissu ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala alisema kamati hiyo ilipokutana na wawakilishi wa TEC na CCT (majina yanahifadhiwa kwa kuwa hatukuwapata kuthibitisha hilo), wawakilishi hao walikiri wazi kuwa majina waliyoyapendekeza sio ya watu walioteuliwa na Rais.

“Sasa hapo uongo na uzandiki wangu ni nini, labda hao wawakilishi wa TEC na CCT walisema uongo, hata wawakilishi wa Shirikisho la Vyama vya Walemavu Tanzania nao waliieleza kamati kuwa majina waliyoyapendekeza, sio ambayo Rais aliteua” alisema Lissu.

Alisema kuwa Rais amemshutumu bila kuujua ukweli, kusisitiza kuwa kama angesoma hotuba yake aliyoisoma katika mkutano wa 12 wa Bunge, asingezungumza maneno hayo dhidi yake.

“Ndio maana katika hotuba yake rais Kikwete alikiri wazi kwa kusema, nimeambiwa, nimesikia, nimeelezwa ukweli ni kwamba wasaidizi wake wamemdanganya,” alisema Lissu.
 
- Kwa hiyo Tundu Lissu alitegemea Rais wa Jamhuri aamuliwe nani wa kumchagua kwenye kamati na hivyo vyama uchwara ndio katiba itakuwa sawa? duh!!

Le Mutuz

chama uchwara hapa bongo ni ccm tu,sijawahi ona chama dhaifu chenye wanachama dhaifu wenye kutumikia matumbo kama wewe! chama cha mauza unga,wezi,majambazi,mafisadi,wang'oa meno na kucha,majangili na bahati mbaya chama kinaongozwa na jangili,HIKI NDIO CHAMA UCHWARA NA KINAPATIKANA TZ TU.
 
huyu jamaa yupo makisana alafu uzuri wa nchi hii wakiujua unajuaju sheria basi wanakuona ww kama mwiba polisi wanakuogopa usalama wataifa pia wanakuogopa viongozi wandamizi wa nchi pia wanakuogopa mfano rais wetu hobuba nzima kwenye katiba kamtaja lisu inaonesha jinsi gani udhaifu alionao wa kumuogopa lisu na kumpa ujiko yeye kama kiongozi wa nchi hii kwenye ile hotuba asinge mtaja lisu aliemwandikia rais hotuba kampotosha good job lisu usomi wako unautumia vizuri
Mkuu ni kweli usemavyo. Jk hakutakiwa kutaja majina kwenye ile hotuba. At least angesema neno, 'msemaji wa kambi ya upinzani kuhusu katiba ni mwongo na mzandiki' lkn sio kumtaja TL binafsi.
 
- Kwa hiyo Tundu Lissu alitegemea Rais wa Jamhuri aamuliwe nani wa kumchagua kwenye kamati na hivyo vyama uchwara ndio katiba itakuwa sawa? duh!!

Le Mutuz

tunammiss le mutuz@nyc,le mutuz@sea view ni wa kujipendekeza kwa maccm ili apate hela ya kunywa bia na akina jokate.
 
- Kwa hiyo Tundu Lissu alitegemea Rais wa Jamhuri aamuliwe nani wa kumchagua kwenye kamati na hivyo vyama uchwara ndio katiba itakuwa sawa? duh!!

Le Mutuz

Inasemekana ameteua tofauti na Majina aliyopelekewa na taasisi hucka mfano shirikisho la walemavu! km nihvyo kulikuwa na7bu gani yakuziambia taasisi zipendekeze Majina ikiwa alijua hatachagua majina yatakayoletwa!!
 
- Kwa hiyo Tundu Lissu alitegemea Rais wa Jamhuri aamuliwe nani wa kumchagua kwenye kamati na hivyo vyama uchwara ndio katiba itakuwa sawa? duh!!

Le Mutuz
have you ever noticed that you are an idiot who has clue?you are stuck in the eighties dumb a*s
 
mkuu mimi naamini hata kama utachanganya watu wa ukoo wenu wote hamuwezi kufikia akili ya jk ni kiongozi wa pekee sana japo wapo watu ambao hawamwelewi.

Mkuu sio hawamwelewi ni kwamba wapo watu wanaomdanganya na kumshauri vibaya hakiwepo mjomba wangu ni washauri wa baya sana kwa Mh. Rais JK yeye ni mstaarabu na mwenye kufikiri sana ni kichwa.
 
“Tuliambiwa na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah tungepewa fedha za kukaa Zanzibar hata kwa wiki nzima, na tulilipwa fedha nyingi tofauti na tunavyolipwa kwa utaratibu wa kawaida,” alisema. Hii nchi kweli inakamuliwa! Yaani watu wanalipwa fedha nyingi tofauti na utaratibu, hii inaashiria nini hasa kwetu sisi walala hai!
 
Hata kama Lissu amekosea lakini haingii akilini ni namna gani Rais anauwezo wa kuwachagulia TEC au CCT mtu anayefaa kuwawakilisha?Alipaswa kuliweka jina lamtu aliyechaguliwa na vyama/taasisi za kijamii au kidini na siyo kuwachagulia.Kama alifanya hivyo basi Rais wetu alikosea na anapaswa kuwaomba radhi aliowakosea.Vinginevyo Lissu atasimamia kauli yake kuwa ina ukweli.
 
Ni kweli kabisa, kayageuza ya Zanzibar wakati kuhusu uongo wake Rais aliyasema ya TEC na CCT.

Huyu jamaa ni muongo, mfitini aka fataani, mnafik na mzandik mkubwa sana.
Dada Faizafoxy naomba nikujibu kwenye hili la TEC ba CCT,hakuna aujuaye ukweli kama kweli Rais amewachagulia au kutowashirikisha wajumbe waliochaguliwa na TEC na CCT.Ukumbuke pia taasisi hizi zinaongoza watanzani wa dini tofauti na Rais hivyo siyo haki na wala haingii akilini pale Rais wetu atakapowachagulia mtu ambaye wao hawakumchagua sababu TEC na CCT ndiyo wanaojua yupi atawafaa kuwawakilisha.Hivyo ni vyema Rais akatwambia je majina aliyopelekewa ndiyo aliwateua?Au aliwateua wakwake?Je,waliochaguliwa na taasisi hizi mbili yaani TEC na CCT wamewekwa kwenye haya Makamati ya katiba au wametupwa kapuni na kutowakilishwa?Inabidi kabla ya kumtukana mtu ufanye utafiti wa kina kuyajua haya.Simtetei yoyote kati ya Lissu na Rais wetu,kwani wote ni binadamu na wanakosea tunachohitaji ni ukweli tu.
 
Wacha kuwa punguani na wewe. Wameshirikishwa, atawachaguliaje kama hawajashirikishwa?

Nyinyi basi hata uongo, fitina, uzandik mtautetea tu hata kama mnajuwa unaleta madhara?
 
Sikubaliani kabisa na maneno ya MBOWE kuwa, Rais JAKAYA KIKWETE kumshambulia TUNDU LISSU wakati wa hotuba yake kuwa alimuonea kwa madai kuwa maneno ya LISSU hayakuwa yake bali ni ya kambi rasmi ya upinzani.

Nadiriki kusema kuwa wanachokifanya hivi sasa CHADEMA ni kujaribu kumusafisha LISSU na tabia yake ya siku nyingi kutoa maneno ya kizushi, dhihaka kwa serikali na mbwebwe nyingine nyingi ambazo kwa uhakika wanaolitakia amani taifa letu, ndani ya Bunge(wale wa chama tawala na upinzani), nje ya bunge, wasomi na hata wananchi wa kawaida walishaanza kuingiwa wasiwasi na utimamu wa akili ya Mbunge huyu.

Siku chache zilizopita , LISSU amepambwa sana kwenye vyombo vya habari, wapambe wake, kwenye mitandao ya kijamii kuwa ni mtu tishio, lakini hakuna aliyesimama na kusema siyo yeye aliye tishio bali ni chama kwa ujumla, ila leo ambapo Rais ameonesha kukerwa na pengine sasa kama mkuu wa nchi anaona anakoelekea LISSU ni hatari kwa amani ya nchi yetu ndipo wanaibuka akina MBOWE na kusema kuwa yale yalikuwa maneno ya Kambi ya Upinzani na kwamba Rais hajamtendea haki na kwamba amuombe msamaha, kwa lipi mpaka rais amuombe msamaha LISSU kama siyo kumkosea adabu mheshimiwa Rais na kuendelea kulea ugonjwa kwa vile LISSU ataona kama amepewa go ahead na mkubwa wake kuendelea kusema hovyo.

MBOWE anasemaje Rais amuombe radhi LISSU wakati huo wanampongeza kwa hotuba yake huku wakisema amewaaibisha wana CCM ambao walionekana kuunanga muungano wao vyama vitatu, muungano ambao kimsingi umekosa mashiko hasa baada ya hotuba ya Rais JAKAYA KIKWETE. Wanamtaka Rais awaite kwenda ikulu kufanya nini kama kweli wanaona LISSU ameonewa?
 
Back
Top Bottom