Tundu Lissu: Tutazipima kauli za Kikwete kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala!

Tundu Lissu: Tutazipima kauli za Kikwete kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala!

kama viongozi wa upinzani wangekuwa na maono kama ya jk hili taifa lingekuwa mbali sana wao wanaandamana na kupigana lakini jk hoja tu watu wanashuka wenyewe.
 
MNADHIMU wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu, amesema kuwa watapima kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuhusu muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba, watakapokutana leo katika Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Lissu alisema kuwa Rais Kikwete katika hotuba yake kwa taifa juzi alisema kuwa suala hilo linazungumzika.

“Mimi ninataka kuona leo kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala liwepo suala hilo katika ratiba kati ya mambo yatakayojadiliwa tayari kwa ajili ya kurejesha muswada bungeni.

“Kama suala hilo halitakuwepo, basi hotuba ya rais itakuwa ni porojo za Magogoni (Ikulu). Rais asiposaini muswada huo ataonyesha nia nzuri aliyokuwa nayo, na hayo tuyaone katika ratiba ya kamati,” alisema.

Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) na msemaji mkuu wa kambi hiyo kwa Wizara ya Katiba na Sheria, alieleza mshangao wake kwa Rais Kikwete kuhutubia taifa kwa habari za kuambiwa, kuelezwa na kufahamishwa bila yeye kujiridhisha.

Alisema kuwa rais alimtuhumu kwa kumuita “mzushi na muongo mtupu mwenye kauli za kinafiki, fitina na uzandiki wa hali ya juu”, lakini akahoji ni kwanini anawataka wapinzani wakae mezani wazungumze naye wakati ni waongo.

“Hoja zangu zilihusu Zanzibar kutokushirikishwa katika mchakato wa kuboresha muswada wa mabadiliko ya sheria, nilisema hakuna mdau hata mmoja au mtu binafsi aliyeonana na wajumbe wa kamati.

“Kwa upande wa bara kulikuwa na wadau 22, ukijumlisha na vyama vya siasa 22, hivyo bara peke yake tulisikiliza wadau 44. Je, fitina, uzandiki na uongo anauosema Kikwete upo wapi?” alihoji.

Lissu alitaja baadhi ya taasisi za bara walizokutana nazo kuwa ni Ongeza Elimu ya Juu, vyama vya siasa na watu binafsi mfano Jaji Mkuu mstaafu, Barnabas Samatta na Prof. Issah Shivji.

Alisema kuwa kwa Zanzibar walipewa ratiba ya kutembelea miradi ya Tasaf, ofisi ndogo ya Bunge na ofisi ya Makamu wa Rais, na kwamba walilalamika kubadilishiwa ratiba hiyo wakiwa Zanzibar.

“Tuliambiwa na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah tungepewa fedha za kukaa Zanzibar hata kwa wiki nzima, na tulilipwa fedha nyingi tofauti na tunavyolipwa kwa utaratibu wa kawaida,” alisema.

Lissu alisema kuwa Kikwete aliwahakikishia Watanzania kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilishirikishwa, lakini Waziri wa Sheria wa Zanzibar alisema kuwa walipelekewa muswada na Mwanasheria Mkuu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Wiliam Lukuvi na kuwataka watoe maoni siku hiyo hiyo.

Kwamba Wazanzibari waliona mambo manne waliyopelekewa katika muswada wa mabadiliko ya sheria hayakuwa na shida wakasema sawa, lakini muswada uliopelekwa bungeni ulikuwa na mambo zaidi ya 11.

“Je, hapa kuna uzandiki? Unafiki uko wapi? Je, na waziri huyo wa Zanzibar naye ni mwongo?” alihoji.

Aliongeza kuwa Rais Kikwete katika hotuba yake alisema ‘ameambiwa’, ‘ameelezwa’ na ‘amefahamishwa’, maneno ambayo ameyatamka mara tisa, na hivyo kuhoji inakuwaje rais anahutubia taifa kwa maneno ya kuambiwa ambayo kisheria hayana nguvu?

“Rais ana uwezo wa kukataa muswada na ana mamlaka ya kukataa mambo ya kijinga yanayopitishwa na wabunge. Tunaomba asisaini muswada huo.

“Rais wetu afanye kama Obama aliyenukuliwa siku za hivi karibuni akisema wabunge wakipitisha mambo ambayo hayana tija kwa taifa hatasaini,” alisema.

Akizungumzia athari za haraka kama rais atasaini muswada huo, Lissu alisema nchi itapata katiba mbovu ya hovyo na matukio ya vurugu kama ya Zimbabwe na Kenya yatajitokeza Tanzania.

Alisema kuwa nchi hizo zilifikia hapo baada ya serikali kujidai inahodhi muswada wa katiba, ikijipendelea yenyewe badala ya kusikiliza wananchi waseme.

Kuhusu wadau ambao waliwasilisha majina halafu rais akateua kadiri alivyoona bila kuteua majina hayo, Lissu alisema hayo hayakuwa mawazo yake, bali waulizwe mwakilishi wa Baraza la Maaskofu Katoliki, Dk. Charles Kitima na Mchungaji Rohho wa CCT.

Kwa wawakilishi wa Shirikisho la Vyama Vya Wenye Ulemavu (Shivyawata), Lissu alidai kuwa walisema kuwa Alshaymar Kweygir, rais ndiye anajua alivyomteua kwani hawakumpendekeza.

Lissu anatapatapa, na ni mnafiki kweli, yeye alikuwa kwenye kamati kwa nini aliruhusu vipengele vingine viongezwe? mnafiki sana huyu mtu. Amebaki kulalama kwa vile Rais amemchana live.
 
ninachowapendea watz wote si waoga hata kidogo maana mtu hata bila kuelewa kinachoendelea anakurupuka na ku- criticize jamani......uwezo wa kufikiria wa TL ni mkubwa kias cha wewe kutoelewa hata anachosema....siyo wewe tu hata wale wakina "nimeambiwa"

kumbe mtu ukiwa unawaza negative ndiyo uwezo kubwa wa kufikiri?,tundu lisu anawaza negative ni mzushi,mnafiki,mbea hilo halina ubishi,
ukiona mpaka rais anaona unafiki na umbe wa mtu huyo mtu ni mbea kweli.
 
kama viongozi wa upinzani wangekuwa na maono kama ya jk hili taifa lingekuwa mbali sana wao wanaandamana na kupigana lakini jk hoja tu watu wanashuka wenyewe.

Mkuu mimi nilkjua tu siku JK akishuka nondo watabaki kutapatapa tu kama anavyofanya LISSU sasa.
 
kama utaki basi amuige abdallah bulembo,,le baharia,,ndugai,,wasira,lukuvi,chikawe..
Wauaji wa CHADEMA ndiyo hao na mtawakumbuka daima jinsi walivyo mwiba kwenu, teh teh teh.
 
Wakuu kamanda Lissu anafanya press, sasa hivi Makao Makuu ya Chadema na haya ndiyo amezungumza;

- Wadau wa Zanzibar hawajashirikishwa hata kidogo na hawakuwepo kwenye ratiba ya Kamati.
- Kamati ilipanga kwenda Zanzibar kutembea na sio kuonana na wadau, kwa sabab walitakiwa pkutembelea miradi ya TASAF, OFISI YA MAKAMU WA RAIS NA OFISI YA BUNGE.
- Wakakataa na kuomba kwa katibu wa Bunge kuwaona wadau wa Zanziba, Katibu wa Bunge alikubali.
- Walitengeneza orodha ya wadau.
- Yalianza maneno pembeni kuwa hakuna usalama Zanzibar wakati huohuo Kamati ya Ulinzi na Usalama ilikuwa Zanzibar.
- Wakazuiliwa kwenda na hivyo hakuna mdau wa Zanzibar aliyehusishwa.
- Kama haya ni makosa uzandiki na unafiki unatoka wapi wakati hoja ya kwenda Zanzibar yeye aliyeitoa?

Nitaendelea kuwapa update

- Kama hakuna ulazima kwa mujibu wa kanuni kwenda Zanzibar ofisi ndogo za Bunge Zanzibar zina maana gani, kwa hili rais amepotoka na hajui analolifanya.
- Hawajawahi kukutana na mjumbe wa Baraza la wawakilishi Zanzibar, na hata M/sheria amekiri.
UTEUZI KWENYE TUME YA KATIBA
- Hoja ni mamlaka ya Rais kuteua wajumbe 166
- Walipinga 2011 Ikaondolewa na wakairudisha tena kwenye muswada huu
- Uteuzi wa wajumbe wa Tume usilinganishwe na uteuzi wa wajumbe wa Bunge la Katiba. Ushahidi wa TEC , CCT na Shirikisho la walemavu kutoteuliwa pamoja na kupeleka majina kwa Rais ulitolewa kwenye Kamati ya Bunge, uongo wake unatoka wapi?
- Shirikisho la walemavu halikumpendekeza Al Shaimar Kwegir na hivyo Rais aliteua watu alkyewaona yeye wanafaa. Uongo unatoka wapi?

Maneno ya Rais,
- Hatamuita mzindiki, mnafiki wala mwongo ila ametoa hitimisho kwa maneno ya sikia sema (hearsay) kwa sababu ametumia maneno "nimeambiwa, nimesikia na nimejulishwa" mara tisa kwenye hotuba yake.

Kuhusu kuwa na mazungumzo ya pamoja;
- Kama ana nia njema basi asiusaini muswada na Katiba inamruhusu kufanya hivyo.
- Akiusaini ataendekeza mambo ya kiccm na hana haja ya kuaminiwa tena.
- Kamati ya Sheria na Utawala ya Bunge inakutana kuanzia kesho na hivyo anasubiri sheria husika iliyopitishwa kinyemela kurudishwa Bungeni.

Mwisho. Anakaribisha maswali;

- Ukiwa na mchakato mbovu yatatokea mambo kama ya Zimbabwa miaka 16 ndiyo ikapata Katiba na Kenya miaka 11 ndipo wakapata Katiba, kwa sababu mwanzoni hakukuwa na mchakato shirikishi.
- Wanachokifanya CCM sasa ndicho walichokifanya KANU kule Kenya
- Wananchi hawatanyamaza kamwe katika mchakato huu.

Mbona haya anayasema leo baada ya kuchanwa live na Rais?
 
kumbe mtu ukiwa unawaza negative ndiyo uwezo kubwa wa kufikiri?,tundu lisu anawaza negative ni mzushi,mnafiki,mbea hilo halina ubishi,
ukiona mpaka rais anaona unafiki na umbe wa mtu huyo mtu ni mbea kweli.

inawezekana kama ukimtumia rais kama malaika/mungu......alaf sioni haja ya mzee (happy birthday) kumuita TL hayo majina yote wakati basis ni ....kuambiwa,kusikia,nk....siyo sahihi maana inawezekana walokwambia wamekudanganya...na hili suala la kudanganya ikulu linaelekea kuota mizizi....
 
inawezekana kama ukimtumia rais kama malaika/mungu......alaf sioni haja ya mzee (happy birthday) kumuita TL hayo majina yote wakati basis ni ....kuambiwa,kusikia,nk....siyo sahihi maana inawezekana walokwambia wamekudanganya...na hili suala la kudanganya ikulu linaelekea kuota mizizi....

umeamka na hangover?
 
Hapana bhana , mimi nakataa ! Tundu lisu ni neema .
namshangaa sana tundu la ushuzi sijui anaona WTZ kama makalio yake, acha uzezeta, mwanaizaya we, hiyo akili uliyopewa mbona unaitumia kuangamiza watu wasio na hatia? kama kweli mnania hiyo mbona mmejipanga ikiludi bungeni mtatoka nje ili katiba mpya isipatikane? ivi kweli nyie viongozi wa chadema mnawaza kwa kutumia nini? kweli mmevulugwa vya kutosha, kumbukeni mmetumwa kama wawakilishi bungeni kwa niaba ya Wananchi, mnavyokimbia vikao vya bunge wanaoumia ni wananchi waliowaagiza au matumbo yenu? acheni ubahadhuri wana watoka pabaya, wana wajambia -----. huyu mtu hafai ktk jamii ya kitanzania.
 
Hili nalo neno!!


Aliongeza kuwa Rais Kikwete katika hotuba yake alisema ‘ameambiwa’, ‘ameelezwa’ na ‘amefahamishwa’, maneno ambayo ameyatamka mara tisa, na hivyo kuhoji inakuwaje rais anahutubia taifa kwa maneno ya kuambiwa ambayo kisheria hayana nguvu?
 
user-online.png
chama kipya

Today 07:57
#14
MemberArray


Join Date : 30th September 2013
Posts : 81
Rep Power : 317
Likes Received5
Likes Given6



.

Join date: 30th September, 2013

Huhitaji kujua ni member mwingine wa buku7 project
 
mkuu mimi naamini hata kama utachanganya watu wa ukoo wenu wote hamuwezi kufikia akili ya jk ni kiongozi wa pekee sana japo wapo watu ambao hawamwelewi.

Akili! kwa kigezo kipi? darasani wote tunajuwa alichovuna, katika uongozi wewe mwenyewe unajuwa mara ngapi amekiri kupewa ushauri mbovu, alikochukuwa net za futi 2 unajuwa aliwapa nini, bandari ya bagamoyo na gasi pia ni akili labda ya kulinda maslahi ya familia, kushindwa kukemea vitendo vya kifisadi, rushwa na wizi wa mali ya umma nayo pia ni akili?! MIMI SIDHANI BENDELA KUFUATA UELEKEO WA UPEPO NI AKILI. Tupo hapa tulipo kwa sababu ya kuweka madarakani viongozi wasio na upeo wa kulinda mali za nchi, kusimamia umoja wetu katika sekta za elimu, afya, mahakama na ajira.
 
Tundu lissu zidi kutupa ukweli, ufisadi tumechoka na hatutaki,hotuba nzima Tundu lissu-go ahead Brother Tundu.
 
Tundu lissu zidi kutupa ukweli, ufisadi tumechoka na hatutaki,hotuba ni Tundu lissu-go ahead Brother Tundu.
 
Nakelwa sana na mtu mzima kama lisu kuwa mbea,mnafiki,mzandiki na mzushi kwani ndiyo kazi aliyotumwa na wananchi wa singida mi najua haya mambo hufanyika kwenye vyumba vya kusukia nywele sijui naye kama ni mdau ni tabia ya ajabu sana kwa mtu anayedhaniwa ni mbunge kuwa mnafiki na mbea.

Namuomba mod wa Lumumba akupe red card, huna unachofanya.... Unazidiwa hadi na Le Mutuz
 
wauaji wa chadema ndiyo hao na mtawakumbuka daima jinsi walivyo mwiba kwenu, teh teh teh.

kwa taarifa yako hakuna anayeiweza chadema ,,maana chadema nikama pumzi utake usitake utaivuta tu,,ukijifanya mkaidi tunakupoteza,,,,,,labda waishinde chadema kwakuendeleea kumdanganya mzee wa magogoni,,,NILIAMBIWA AKA NILIAMBIWA AKA NILIAMBIWA AKA,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
 
Back
Top Bottom