Tundu Lissu una uhakika kuwa tatizo la Watanzania ni bei ya nyama kuwa sawa na ya maharage?

Tundu Lissu una uhakika kuwa tatizo la Watanzania ni bei ya nyama kuwa sawa na ya maharage?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kwahiyo umetoka nchini Ubelgiji (Ulaya) kuja (kurejea) Tanzania kuzungumzia Bei ya Nyama kuwa sawa na ya Maharage?

Kama wanasiasa wa Upinzani mpo this low ni bora tu GENTAMYCINE na Watanzania wenye akili tuendelee kuipigia kura CCM na CCM iendelee kutawala kama siyo kututawala milele!

I'm very disappointed, kwani nilidhani unarejea rasmi Tanzania na Agenda zako Kuu kuwa ni Katiba Mpya, Haki za Binadamu, Utekwaji na Mauwaji ya Watanzania, Huduma mbaya za Kiafya/Afya, Elimu yetu iliyoko ICU kwa sasa na Ujinga miongoni mwa Watanzania wengi (siyo wote), wewe unarudi na mambo ya Nyama na Maharage? au ulivimisi mno ulikokuwa huko Ulaya (Ubelgiji) na Marekani?
 
Bei ya maharage imegusa watanzania wote tokea nanjilinji hadi kyerwa. Beberu akiita "wide spectrum." Na hiyo ndiyo siasa ya akili sasa.
 
Bado hatuna chama cha upinzani, kinachoweza kutatua changamoto za Watanzania. Hao wanaojiita wapinzani ni CCM ,wachumia matumbo na walamba asali. Utawasikia wakisema "Hivi mnajua tumepoteza bilioni ngapi kwenye kupigania chama na watanzania".
 
Lissu ameanza kupigania mambo ya utawala bora wa sheria kabla ya wewe mleta mada kubalehe/kuvunja ungo.

Leo unaamka na kumpangia Lissu cha kusema.
Acha hizo aisee..
 
Leo kazungumzia bei za chakula ambayo ni kilio cha watu wengi kutona na mfumuko wa bei za bidhaa yuko sahihi, lakini kagusia katiba mpya ni sawa kwa kua mikutano anayo mingi ajenda nyingine atazungumzia siku nyingine wewe kama unapigia kura ccm pigia tu hakuna sababu ya kuleta visingizio
 
We mjinga hufahamu lolote kuhusu politics matters
Na wewe hufahamu lolote kuhusu economics na monetary policies.
Lissu ameongea kitu cha ajabu na kutaka kuingiza siasa kwenye suala la inflation.
Inflation is universal, na central banks wanajitahidi kuongeza riba Ili kupunguza inflation kwenda kwenye inflation limit ya 2-2.5%.
Unafahamu kule Ufilipino ya kuwa kitunguu kimoja kinauzwa sh.23000/= wakati nyama ya kuku inauzwa sh.9200/=?(hapa nimefanya conversion kwenda kwenyeTanzanian shillings )
 
Maharage ya siku hizi ni matamu kuliko nyama, so muda si mrefu yataipiku bei ya nyama.
 
Na wewe hufahamu lolote kuhusu economics na monetary policies.
Lissu ameongea kitu cha ajabu na kutaka kuingiza siasa kwenye suala la inflation.
Inflation is universal, na central banks wanajitahidi kuongeza riba Ili kupunguza inflation kwenda kwenye inflation limit ya 2-2.5%.
Unafahamu kule Ufilipino ya kuwa kitunguu kimoja kinauzwa sh.23000/= wakati nyama ya kuku inauzwa sh.9200/=?(hapa nimefanya conversion kwenda kwenyeTanzanian shillings )
huko ndio pa kuishi sasa

Kuku mtamu wewe
 
Back
Top Bottom