Tundu Lissu: Usalama wa taifa(TISS), hawana mamlaka kisheria kukamata wanaopinga au kukosoa serikali

Tundu Lissu: Usalama wa taifa(TISS), hawana mamlaka kisheria kukamata wanaopinga au kukosoa serikali

Kipenzi chako jiwe alikusudia kuua kabisa upinzani halisi.

Yaani unakuta MTU anaongea kizalendo na kiakili Sana halafu anakwambia Magufuli ndo alikuwa mzalendo WA kweli...yaani unashindwa kabisa kuelewa the reasoning
 
Ukisema hivyo ni kama vile kuna jeshi ndio lina kibali kisheria kukamata wakosoaji wa serikali. Hakuna jipya alilosema hapo ndugu yetu Tundu Lissu.

Iko hivi, askari wote ni kama mimi na wewe, wanaweza kutii amri isiyo halali kulinda vibarua vyao. Lazima kuwe na taasisi imara zinazoweza kulinda yeyote sheria ikichezewa.

Unfortunately, hili litawezekana pale CCM watapogundua muda wao kutawala upo ukingoni penda wasipende! Pale tutapokuja kuwa na wapinzani halisi na si mapandikizi ya watu!
Andiko lililonyooka kabisa; isipokuwa huo mstari mmoja na nusu wa mwisho..

CCM hawawezi hata siku moja kugundua chochote kwa vile wanajuwa watu wanaowatawala hawajui lolote.

Panatakiwa pawepo na akina Lissu wengi huko kwenye upinzani, ili wauondoe ujinga unaotumiwa na CCM kuujaza vichwani mwa wananchi.
 
..aliyoyasema sio mapya kwako, je umejiuliza ni mapya kwa Watanzania wangapi?
Nimesoma andiko lako lote lililotanguliwa na mstari huo hapo juu.

Imenibidi nirudie kusoma mara kadhaa na kujiuliza swali: Hivi ujinga wa waTanzania ulianzia wapi na lini?
Mbona kama vile huko awali mambo haya yalikuwa yakifahamika vizuri, na hivi vyombo kila kimoja kilifanya majukumu ndani ya mipaka yake?

Mara tunajikuta sasa, mtu yeyote mwenye sare na mabuti, hata yule jamaa wa wanyama pori sasa hivi anaweza kuingia mahali na kuweka watu hatihati!

Jamaa wa uhamiaji anaweza kwenda sehemu yoyote na kutishia watu hata bila sababu, na watu wakatishika kweli!

Ni vyema Lissu kalichukua hili na kulichambua, lakini hili haliko huko peke yake, na siyo katika vyombo vya ulinzi pekee. Sehemu zote nchini taratibu za utendaji zimewekwa pembeni, kila mwenye nafasi anatumia nafasi yake anayoijuwa yeye na kuitumia atakavyo, kwani ujinga wa wananchi hauwezi kuhoji chochote.

Hawajui kitu, watahoji vipi!
 
..tunasubiri ELIMU atakayokuja kuitoa Tundu Lissu.
 
Back
Top Bottom