Tundu Lissu: Vincent Mashinji alikosa uadilifu ndani ya CHADEMA. Hakuna pengo kuondoka kwake

Tundu Lissu: Vincent Mashinji alikosa uadilifu ndani ya CHADEMA. Hakuna pengo kuondoka kwake

Chadema nzima kuna PhD tatu tu na sasa zimebaki mbili ulitegemea muujiza gani labda mwenyekiti angekuwa Baregu.

A/c ya ruzuku iko Arusha kwa mwenye chama ulitaka Dr Mashinji atendeje?.......Wachangaji wenyewe ndio hao kina Gekui na Waitara wamekimbia......mnyonge mnyongeni haki yake mpeni bwashee!

PhD zina issue gani, jiwe ana PhD lakini kuongea kwa lugha aliyopatia PhD Ni vituko. Cdm hawaangalii PhD wanaangalia uwezo. Kama PhD zingekuwa na maana Mashinji angefanya la maana. PhD zinatakiwa ccm maana huko hawaangalii uwezo kwakuwa vyombo vya dola vinawabeba.
 
Kama hakuwa muadilifu shida ni aliyemteua na waliompitisha kuwa KM!

Mashinji hakujiteua, alifuatwa na hao "waadilifu uchwara"

Hapo aliyelipuliwa ni Mfalme mwenyewe kwa kuleta watu wa hovyo hovyo na Lisu akishiriki kikao cha kumpitisha Mashinji!

Mashinji aliwekwa kwenye hicho cheo na Lowassa, na Mbowe hakuwa na jinsi maana yeye na genge lake walikuwa wamekula hela ya Lowassa.
 
Kwa hiyo kuhama kwa Dr Slaa na Patrobas Katambi kwenyewe kulikiathiri chama kwa kuwa walikuwa bado na vyeo vyao?

Sasa mbona mlikuwa mnajibaraguza siku zote kwamba hakuna athari?
 
Mbowe amehojiwa jana na Clouds FM kipindi cha Jahazi. Amesema very clear Kuwa wahuni wote wanajulikana. Hata ambao wapo kwenye negotiations wanajulikana. Lakini kama chama hawatawafukuza. Watashughulika nao kwa akili na mwishowe watajitoa wenyewe. Wakianza kufukuzwa watapata public sympathy watakapoanza kulia lia wamefukuzwa na hivyo kuondoa ajenda muhimu ya chana kwa sasa. Kwaiyo wanaofika bei wanajulikana, waliofika bei wanajulikana. Mbowe akamalizia kwa kusema Chadema ipo imara kuliko nyakati zote zile!

Sent using Jamii Forums mobile app

Zitto na Kitila walipata hiyo huruma ya umma?
 
Tatizo kila akitaka kukigeuza chama, anakuta na nguvu kubwa ya "Mwamba".

Cha ajabu ni hao hao Chadema wanasema wamenyimwa uhuru wa kufanya siasa wakati ndani ya chama kuna visiki kibao vya kisiasa.
Kwani si kweli wamezuiwa kufanya siasa?

Pili, kuna “mercenaries”, ambao ni askari wa kulipwa. Hao wanapigania maslahi yao yanayotokana mafunzo yao na siyo uzalendo kwa kile wanachokipigania.

Huyu Mashinji alikuwa ni “mercenary” wa kisiasa. Anategemea vyeti zaidi kuliko uzalendo wake. Hayo mavyeti yote hakuna substance.
 
Lilikuwa kosa la kuleta vyama vya upinzani mapema hapa nchini, wakati bado kujitambua kwetu sio kamili.

Mambo yanayoendelea katika siasa zetu yanastaajabisha kabisa.

Yaani unakuta mwanasiasa mpaka anastaafu keshapiga tripu kwenye vyama vitatu na kote huko anapata nafasi. ( Mfano Maalim Seif, CCM, CUF na sasa ACT)

Nashindwa kuelewa inakuwaje mwanasiasa wanabadili itikadi zaidi ya mara tatu na bado wanaaminika kwa wananchi.
 
Huyo Mashinji ana rundo la vyeti na cv ni exceptional. Lakini utendaji ulikuwa sifuri. Aliwekwa akidhaniwa atafanya vyema kanda ya ziwa.

Ila kusoma na kuelimika ni vitu viwili tofauti kabisa. Maana unaweza ukawa msomi ambaye hujaelimika!
Kwa ufupi Mashinji sio mwanasiasa na hatakuja awe kamwe,namuona kama Bashiru vile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema nzima kuna PhD tatu tu na sasa zimebaki mbili ulitegemea muujiza gani labda mwenyekiti angekuwa Baregu.

A/c ya ruzuku iko Arusha kwa mwenye chama ulitaka Dr Mashinji atendeje?.......Wachangaji wenyewe ndio hao kina Gekui na Waitara wamekimbia......mnyonge mnyongeni haki yake mpeni bwashee!
Acha porojo Bwashee 😀

Kwani Dr Slaa alitendaje?

Zaidi ya mavyeti kibao sijaona la maana kwenye utendaji wake. Ameshindwa kui “utilize” elimu yake.
 
Mashinji zaidi ya hivyo vyeti vyake sioni kama ana uwezo wa kuongoza chochote kile. Labda familia yake.

Unaweza kuta na yeye ni wale waliokariri tu. Mavyeti yote hayo halafu hakuna utofauti aliouleta tujuwe alielimika!
Ukweli ni kwamba Dr. Mashinji alifanya kazi na watu wenye uelewa na darasa dogo - mwenyekiti na katibu msaidizi wake hawana hata kadigree ka kwanza! Wewe utafanya nao kazi vipi? - You will always be out of phase of each other! It is not his fault. Alionekana slow maana boss wake elimu ndogo, hivyo Mashinji alikuwa anavutwa kusudi waende pamoja na boss wake!
 
Mkuu unawezaje kutenganisha polisi na CCM na Sumaye analijua hilo,kwake hiyo ilikuwa gia ya kuondokea,lakini anazo sababu lukuki za kimaslai zilizomlazimisha aondoke.
Chadema wanaamini katika kupambana na polisi badala ya kuichallenge CCM kwa hoja by Frederick Sumaye

Katika mazingira hayo mlitaka Dr Mashinji afanyaje?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli ni kwamba Dr. Mashinji alifanya kazi na watu wenye uelewa na darasa dogo - mwenyekiti na katibu msaidizi wake hawana hata kadigree ka kwanza! Wewe utafanya nao kazi vipi? - You will always be out of phase of each other! It is not his fault. Alionekana slow maana boss wake elimu ndogo, hivyo Mashinji alikuwa anavutwa kusudi waende pamoja na boss wake!
Mkuu hoja yako hii naichukulia kuwa ni “hoja mfu”, na nina mifano mingi tu ya ku prove hilo.
 
View attachment 1363963

Makamu Mwenyekiti wa Chadema Mh Tundu Lissu amesema kwamba kuondoka kwa Mashinji na waliomtangulia ndani ya Chadema , wakati tayari wamevuliwa vyeo hakuwezi kuathiri chama chake kwa lolote .

Amedai kwamba wangeweza kuathirika iwapo kama wahusika wangehamia ccm wakiwa na vyeo vyao , lakini kwa style hii hawawezi kuathiri chochote .

Lissu pia amegusia uadilifu wa Mashinji , ambapo amedai kwamba hakuwa Muadilfu ( hakufafanua )
TALKING TOO MUCH WITHOUT ACTION ITS LIKE RUNNING VERY FAST WITH ZERO DISTANCE COVERED WHICH ENDING THE RESULTS WITH 0 WORKDONE.
 
Wewe na zero brain mwenzako hovyo kabisa..kwani hizi phd na doctorate si ndio zimesababisha watu kupotezwa zilipoanza kudadisiwa? wasomi wa kweli wako nje ya CCM hata kama huwaoni kwenye nafasi za uongozi Chadema lakini ndo wanasuka mambo nyuma ya pazia. Kama chama kinavutiwa na watu wa aina ya Bansen bana na kuwa ubalozi what do you expect? Bana ailete faida nchi hii? Kweli?
Thehe thehe thehe ile PHD ya what is a cataryst? A cataryist is something that speeds up ze reaction but it itself remain unchanged. Ilihojiwa jamaa aliyehoji akang'olewa macho na kucha na kufukiwa pembeni ya mto ruvu under gun point!!
 
That’s why I said it’s sour grapes!
Tundu Lissu kaleta argument ya kijinga inayoweza kuwaridhisha watu wenye mahaba na waliojitoa akili.

CHADEMA inatakiwa ijipange kuhusu vetting. Inawezekana kila mikakati inayopanga inavuja kwa CCM kwa sababu viongozi wanakwenda CCM na kutoa siri huko.

Si jambo la leo wala mara moja. Wameanza kuondoka kina Dr. Walid Amani Kabourou huko. Shibuda alivyoingia CHADEMA niliwatahadharisha atawaletea matatizo, namjua personally. Hawakunisikia. Kilichofuatia ni fedheha.

Habari ni ile ile kwa Lowassa, Sumaye na sasa Mashinji.

Ama CHADEMA ina udhaifu katika sera na uongozi wake, watu wanaona chama hakifai wanaondoka, ama ina udhaifu katika kuchuja viongozi.

Either way, that is not a good look.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom