Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 16,003
Ndugu zangu,
Ghafla baada ya mwamba kujitosa, lile tangazo la Tundu Lissu kuomba michango ''kumsaidia kugombea urais'' limepotea. Tundu Lissu au wafuasi wake sio wajinga kwani sasa wanaelewa nini kinafuata. Zengwe lile lile lililowapata Zitto na Dr.Slaa ndilo linamwandama Tundu Lissu ambaye kwa sasa amepata mshituko.
Tundu na wafuasi wake wanajua hawawezi kuchuana na ''mwamba'' au mtu atakayependekezwa na ''mwamba'' (kumbuka Nyalandu yumo kwenye kinyang'anyiro).
Nini kitatokea, tutege sikio. Ila ninamshauri Tundu aache jazba, avumilie ili akomae ndani ya Chadema kwani bado ni ''mchanga'' ndani ya Chama.