Huyu nae hata kama tunamsapoti kuna mambo anapaswa atumie akili kiutawala, sitaki kuamini Lissu haelewi kilichofanyika. Hii sasa ataanza kupoteza watu tunaomuelewa.
In short, mama alichofanya ni kwamba angeweza kuamua kukaza kwani mngemfanya nini? Sababu waliofungiwa walitumia utaratibu wa Sheria iliyopo/zilizopo. Yawezekana Sheria hizo ndio kandamizi, Rais hawezi kuziongelea pale ndio maana ametoa kwanza waliofungiwa wafunguliwe halafu ndio tuanze upya.
Kwenye kuanza upya ndipo ataambiwa kwamba tatizo ni sheria iliwekwa ya kikandamizi sana hapo ndipo ataweza kuchukua steps zaidi.
Kimsingi hiyo ni amnesty/msamaha, sababu haimhusu yeye, yeye anataka uhuru wa habari uwepo ndio maana amegusia kwani ai angeweza kukaa kimya tu nani angemsumbua?
Sasa basi, kwa msamaha huo maana yaje ndio yale maneno kwamba tusameheane tuanze upya sasa Lissu anataka ligi ya nini?