Tundu Lissu: Wenje atoe video recording ya mjadala wa tuhuma dhidi yake na wenzake kupokea pesa za Abduli na mama yake

Tundu Lissu: Wenje atoe video recording ya mjadala wa tuhuma dhidi yake na wenzake kupokea pesa za Abduli na mama yake

Ubaya Ubwela

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2024
Posts
1,353
Reaction score
3,060
Ezekia Wenje amekiri mwenyewe kwamba kuna video recording ya mjadala wa tuhuma dhidi yake na wenzake kupokea pesa za Abduli na mama yake. Ni kweli. Walirekodi kikao hicho chote kwa video.

Ili kuondoa ubishi wa suala hili ninawashauri watoe video recording yote ya kikao hicho. Wasikate vipande vipande wala wasihariri chochote. Watoe video nzima ya mjadala huo ili wanachama na Watanzania wajue ni akina nani walituhumiwa kwa kupokea pesa ya Abduli na mama yake, ushahidi niliouwasilisha dhidi yao na wao wenyewe walijiteteaje!!!
IMG_20241221_004332.jpg
 
Utetezi wake hauwezi kushawishi watu.

Wenje anapinga madai ya kuhongwa kwa hoja nyepesi kuwa mbona anaendelea kuisema negative administration ya Samia.

This is weak argument
Sasa hiyo hongo ilikuwa ya nini kama hakuna chochote kilichobadilika kutoka kwa hao wanodaiwa kuhongwa kumnufaisha muhongaji?!
 
Sasa hiyo hongo ilikuwa ya nini kama hakuna chochote kilichobadilika kutoka kwa hao wanodaiwa kuhongwa kumnufaisha muhongaji?!
Kwani mapandikizi ambayo yanawekwa na watu wa system ndani ya chama huwa unategemea wawe wana behave kichawa kuwa upande wa serikali ?

Huoni kufanya hivyo kutaharibu mipango yao kwasababu itakuwa ni rahisi kusanukiwa?
 
Hakuna mapandikizi wala nini, hayo mapandikizi yangekuwa na maana yoyote kusingekuwa na hekaheka kubwa hivyo za dola kunyamazisha upinzani na ukosoaji kwa nguvu kubwa hivyo.
 
Naona wanasiasa wetu wanajivua nguo tu

Sisi wananchi tupate funzo tu kuwa hatuna chetu nchi hii ni ya wachache. Wanagawiana wao kwa wao. Walioko madarakani mama Abduli et al, sambamba na wanaowanyima usingizi(wapinzani).

Mwanasiasa akikwambia usiku mwema, kabla ya kumjibu toka nje uangalie kama kweli ni usiku ndipo umjibu asante na wewe pia.
 
Hakuna mapandikizi wala nini, hayo mapandikizi yangekuwa na maana yoyote kusingekuwa na hekaheka kubwa hivyo za dola kunyamazisha upinzani na ukosoaji kwa nguvu kubwa hivyo.
Kama hakuna mapandikizi jiulize tu why Raisi siku ya hotuba yake atoe kauli kuwa amepewa taarifa na mashushushu wake, ambao wako ndani ya hicho chama?

Wakidai Chadema walifanya kikao Arusha (Ngulelo) ambapo kuna ofisi ya Chama wakidai Chadema ilifanya kikao kwa ajili ya kufanya vurugu kuzua taharuki

Na katika maelezo yake alisema miongoni mwa wanachama walisema "tuwe makini maana raisi ana intelijensia kali" maana walijua upo uwezekano wa hizo taarifa zao kuvuja.
 
Back
Top Bottom