TUNDU LISSU - WALIOENGUA WAGOMBEA WA CHADEMA NI WAHUNI, HAWANA MAMLAKA HAYO KISHERIA
Tundu Lissu - Huwezi Kuwekewa Pingamizi na Mtu Asiye Mgombea,
Tundu Lissu achambua Maana ya zoezi hili la uteuzi 07 November 2024 lililofanywa na TAMISEMI
View: https://m.youtube.com/watch?v=nECJK6jR04Q
Majina yote yanatakiwa kwanza yawekwe katika ubao wa matangazo ili wagombea wawekewe pingamizi ikiwa lipo, na pia mkurugenzi au TAMISEMI haina mamlaka kisheria kuengua, kuweka pingamizi kwa wagombea asisitiza Tundu Lissu...
Sasa hawa wagombea wetu wamewekewa pingamizi na nani kwa siri kuu? ...
Akitoa semina elekezi wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, makamu mwenyekiti wa CHADEMA taifa bara Tundu Lissu amefafanua kuwa watendaji na wakurugenzi wote waliotangaza kuenguliwa wagombea ni wahuni wasiofuata sheria na kanuni...
Ni wagombea wa nafasi tu ndiyo wamepewa nguvu kisheria na kikanuni kwenda kuangalia majina ya walioteuliwa katika mbao za matangazo ndiyo wanaweza kuweka pingamizi
Kazi ya wakurugenzi na watendaji ni kubandika majina yote wa wagombea katika mbao za matangazo na kuachia wagombea kuwekeana pingamizi baina yao ..
Mkurugenzi au mtendaji hana mamlaka ya kutundika jina la fulani tu, bali analazimika kurmrundika majina yote bila kisingizio cha kuwepo kosa, wagombea ndiyo pekee wenye kuweza kuweka pingamizi .