LGE2024 Tundu Lissu yuko sahihi, mfano Kilosa Kuna Vijiji 138 CHADEMA ina Wagombea 70, Kuna Vitongoji zaidi ya 800 CHADEMA ina Wagombea 200!

LGE2024 Tundu Lissu yuko sahihi, mfano Kilosa Kuna Vijiji 138 CHADEMA ina Wagombea 70, Kuna Vitongoji zaidi ya 800 CHADEMA ina Wagombea 200!

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
..Ccm inapokea ruzuku BILLIONI 3.2 kila mwezi.

..Cdm inapokea ruzuku chini ya milioni 5 kwa mwezi.

..pamoja na hali hiyo bado Ccm inataka kuengua wagombea wa Cdm.

CCM chama Cha kijinga sana
 
Moja ya Sifa kuu ya Tundu Lissu ni Mkweli

Alisema CHADEMA bado haijawa na Wagombea wa kutosha kuikabili CCM

Hiyo imejionesha kwenye wilaya karibu zote

Mfano mzuri ni Kilosa Vijiji 138 Chadema ina wagombea 70 tu

Vitongoji zaidi ya 800 lakini Chadema ina wagombea 200 na ushee tu

Safari bado ni ndefu 🐼

Mnaengua wagombea halafu mnaleta ngonjera
 
16 November 2024
Dodoma, Tanzania

PATASHIKA; CHADEMA DODOMA WALIOENGULIWA WAKWAMA KWENYE RUFAA, POLISI WAZUNGUKIA, VILIO VYATANDA

View: https://m.youtube.com/watch?v=xzEix_7kRU0
Mfano Mgombea huyo wa Amosi Sylvester Lyaki mkazi wa mtaa Kisasa Medeli Dodoma amekuwa kwa miaka 5 mjumbe wa serikali ya mtaa wa Kisasa Medeli toka mwaka 2019 hadi 19 October 2024... lakini yeye na wagombea wa Chadema rufani zao...

Hii sio haki kabisa
 
TUNDU LISSU - WALIOENGUA WAGOMBEA WA CHADEMA NI WAHUNI, HAWANA MAMLAKA HAYO KISHERIA

Tundu Lissu - Huwezi Kuwekewa Pingamizi na Mtu Asiye Mgombea,

Tundu Lissu achambua Maana ya zoezi hili la uteuzi 07 November 2024 lililofanywa na TAMISEMI

View: https://m.youtube.com/watch?v=nECJK6jR04Q

Majina yote yanatakiwa kwanza yawekwe katika ubao wa matangazo ili wagombea wawekewe pingamizi ikiwa lipo, na pia mkurugenzi au TAMISEMI haina mamlaka kisheria kuengua, kuweka pingamizi kwa wagombea asisitiza Tundu Lissu...

Sasa hawa wagombea wetu wamewekewa pingamizi na nani kwa siri kuu? ...

Akitoa semina elekezi wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, makamu mwenyekiti wa CHADEMA taifa bara Tundu Lissu amefafanua kuwa watendaji na wakurugenzi wote waliotangaza kuenguliwa wagombea ni wahuni wasiofuata sheria na kanuni...

Ni wagombea wa nafasi tu ndiyo wamepewa nguvu kisheria na kikanuni kwenda kuangalia majina ya walioteuliwa katika mbao za matangazo ndiyo wanaweza kuweka pingamizi

Kazi ya wakurugenzi na watendaji ni kubandika majina yote wa wagombea katika mbao za matangazo na kuachia wagombea kuwekeana pingamizi baina yao ..

Mkurugenzi au mtendaji hana mamlaka ya kutundika jina la fulani tu, bali analazimika kurmrundika majina yote bila kisingizio cha kuwepo kosa, wagombea ndiyo pekee wenye kuweza kuweka pingamizi .

Ila ccm ni wahuni Sana. Wanaona nchi ni Mali yao
 
Mchengerwa afumbia macho wahuni wakurugenzi walioteka nyara mchakato wa uchaguzi wa serikali ya mitaa 2024 walioamua kuwaengua wagombea

08 November 2024

Mchengerwa: Mgombea asiyeridhika na uteuzi akate rufaa​

View: https://m.youtube.com/watch?v=yBMTHBdD0T0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa amewataka wanaodai kuenguliwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuacha kulalamika pembeni badala yake watumie siku mbili zilizowekwa kikanuni kuwasilisha malalamiko yao.

Mbali na hilo, Mchengerwa amewataka wasimamizi wasaidizi katika maeneo yote kuhakikisha wanatenda haki na kuzingatia misingi ya 4R kama ambavyo kanuni, taratibu zilivyotoa miongozo ya nini cha kufanya.

Akizungumza na waandishi wa habari Dodoma leo Novemba 8, 2024 amesema zipo siku mbili za kupokea changamoto na malalamiko mbalimbali, kupitia taratibu ambazo wagombea wanatakiwa kuzifuata

Tangu lini Jaji akasimamia kesi yake mwenyewe? Mchengerwa aache ujinga.
 
Mbabaishaji tu huyo mkurugenzi
 
9 November 2024
CCM ARUSHA WALIA na kulaani TUME ya UCHAGUZI HURU - WAWAKILISHI WAO wa SERIKALI za MTAA WAKATWA MAJINA...

View: https://m.youtube.com/watch?v=snTQVvXaxS0
Msimamizi msaidizi ngazi ya mtaa wamewaengua na kutowateua wagombea wa CCM ngazi ya mtaa serikali za mitaa ...

CCM yaomba wasimamizi wasaidizi kurejea maamuzi yao na kama haki haitapatikana CCM itakwenda ngazi ya juu ya kamati ya rufaa ngazi ya wilaya ili wagombea wa CCM walioenguliwa wapate haki yao asema katibu muenezi wa CCM wilaya ya Arusha

Maigizo tu
 
Watu wanatekwa na kuuawa hovyo, huku familia zao zikibaki na majonzi. Hivyo watu wameamua kukaa pembeni
Katika hali ya sasa ya kisiasa, vyama vya upinzani havipaswi kulaumiwa au kuchekwa kwa kushindwa kuweka wagombea kila mahali ktk uchaguzi wa serikali za mitaa kwani gharama ni kubwa sana kulinganisha na uwezo wa vyama.
Malalamiko ambayo yanapaswa kushughulikiwa ni haya ya kuhusu kuenguliwa kwa wagombea wa upinzani kwa upendeleo wa wagombea wa chama Tawala CCM.
Hapo tutakuwa na uchaguzi ulio huru na wa haki!
 
Back
Top Bottom