09 November 2024
Mtaa wa Medeli
Dodoma Tanzanoa
CHADEMA YAMJIA JUU MSIMAMIZI MSAIDIZI BAADA YA KUKATA JINA LA MGOMBEA WA MTAA WA MEDELI DODOMA
View: https://m.youtube.com/watch?v=RfFvzbn7b8k
Mtaa wa Medeli mjini Dodoma vituko vya wasimamizi wasaidizi kukata jina la mgombea wa CHADEMA Amosi Sylvester Lyaki yawekwa wazi ...
Mgombea huyo wa Amosi Sylvester Lyaki mkazi wa mtaa Kisasa Medeli Dodoma amekuwa kwa miaka 5 mjumbe wa serikali ya mtaa wa Kisasa Medeli toka mwaka 2019 hadi 19 October 2024.
Cha kushangaza nyumba yangu ipo Medeli, nina familia na ninejiandikisha katika daftari la mkazi wa mtaa wa Medeli, kitambulisho cha mpiga kura ni mkazi wa Medeli .... lakini naambiwa mimi siyo mkaazi wa Medeli wakidai mimi ni mkazi wa Bwawani
Kwanini wagombea wa CHADEMA tu ndiyo tunaenguliwa, tunaonelewa sana sisi wapinzani ... mimi nimemuongoza msimamizi msaidizi kama mjumbe wa serikali ya mtaa ...
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma atoa maelekezo ya uchaguzi wa serikali za mitaa
Imewekwa tarehe: September 28th, 2024
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
WANANCHI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshauriwa kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa tarehe 27 Novemba, 2024 ili kuchagua viongozi bora.
Kauli hiyo ilitolewa na Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko alipokuwa akitoa Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 kwa waandishi wa habari ofisini kwake leo tarehe 26 Septemba, 2024.
Dkt. Sagamiko alisema “niwahamasishe wananchi wa halmashauri ya jiji la Dodoma kujitoleza kwa wingi siku ya uchaguzi ambayo ni jumatano ya tarehe 27 Novemba, 2024 ili kuchagua viongozi bora watakaoongoza”.
Msimamizi huyo wa uchaguzi alisema kuwa wananchi wenye sifa za kushiriki wanatakiwa kushiriki. “Ninatoa wito kwa wananchi wote wenye sifa kushiriki kikamilifu katika mchakato huu wa uchaguzi, kuanzia hatua ya kujiandikisha kwenye orodha ya mpiga kura. Kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura ni hatua inayompa kila mwananchi mwenye sifa haki ya kisheria kushiriki uchaguzi kama mpiga kura au mgombea nafasi ya uongozi” alisema Dkt. Sagamiko.
Akiongelea nafasi zitakazogombewa alizitaja kuwa ni mwenyekiti wa mtaa, wajumbe wa kamati ya mtaa mchanganyiko na kundi la wanawake. “hivyo, wananchi wenye sifa wanahimizwa kuchukua na kurudisha fomu za kugombea nafasi hizo kwa tarehe zilizoainishwa katika maelekezo haya. Ushiriki wa wananchi wengi katika kugombea nafasi hizi ni muhimu katika kukuza demokrasia na kuhakikisha upatikanaji wa viongozi bora kwa maendeleo ya taifa letu” alisisitiza Dkt. Sagamiko.
Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Jiji la Dodoma alitoa maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 mbele ya waandishi wa habari, viongozi wa vyama vya siasa na makundi maalum pamoja na wadau wengine.
MWISHO