Mbangaizaji wa Taifa
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 493
- 844
Kama kuna kijana wa hovyo na asiye na fadhila hata kidogo aliyetoka Upinzani na anafanya kila juhudi kuumaliza Upinzani huo ambao ndio umemkuzà na kumlea na kumfanya awe alivyo leo ni huyu Kafulila wa sasa.
Eti leo hoja kubwa kubwa za Upinzani kama ukuaji wa deni la Taifa, Ubinafshaji wa Bandari na mengineyo huyu jamaa amekuwa akizieleza kwa data na mifano Sasa hata hatujui kama ni Kweli au ni data za kubumba tu lakini Upinzani tuko ziiii kwanini hatumjibu au hatuwezi au anayoyasema ni ya kweli?
Kama hamjui huyu Bwana ni mtu hatari kuliko akina Makalla na Wassira na kwakuwa yeye anafanya haya kwa maelekezo ya CCM na Samia na anayafanya kwa ustadi sana wewe jaribu kufuatilia tu maandiko yake humu utaona upotoshaji wake utaelewa nachosema.
Inauma kuona Kafulila anatamba tu na hoja humu bila kukabiliwa na yoyote labda kidogo Mpina na Job Ndugai lakini hata hivyo wote hawa ni watu wa CCM Upinzani tuko wapi?
Nashauri wachambuzi nguli wa Uchumi kama akina Zitto Kabwe, Ruge au Ambokile wa CHADEMA waje na majibu kwa hoja za huyu jamaa kwani anapenyeza agenda zake kwa umakini mkubwa na anafanya kimya kimya.
Makamanda tuendelee kuchangia chama hatuna mjomba Wala shangazi wa kutushika mkono.