Tunduma: Ally Mwafongo na wenzake 57 watimiza siku 143 Gerezani

Utawala wa CCM una uonevu sana...sijui huwa wanakwenda makanisani na misikitini kufanya nini - huku ni kumdhihaki Mwenyezi Mungu.
 
Ni vizuri kutoa taarifa kama ulivyofanya hapa, lakini nadhani kama chama CHADEMA bado mnaonyesha kutokuwa na umakini sana juu ya mambo kama haya.

Hawa ndio wapiganaji wenu wakubwa. Huwezi kumwacha askari wako na kumtelekeza kiasi hiki bila ya hatua, kama zile zilizochukuliwa kwa yule mama wa Dar es Salaam..., Maki...nani yule!
Huu ni uonevu unaovuka mipaka ya ubinaadam kabisa, na unafyanywa hivyo maksudi kuwaogopesha wanachama wenu wengine wote, na waTanzania kwa ujumla wao, ili hawa viongozi wa hovyo waendelee na ukandamizaji wao.

CHADEMA imefanya nini kuwapigania hawa wanachama wake, ili angalau wafikishwe mahakamani? Mbona huko Dar es Salaam imewezekana, huku Tunduma kwa nini haiwezekani?

Haya mapambano mnayafanya kuwa magumu sana kwenu kwa kutoyapa umakini mkubwa unaotakiwa kila mahala. Watesi wetu sote wanapenda sana hali hii.

Itisheni michango, watu wachange kutafuta mwanasheria asimamie jambo hilo, huo ndio utakuwa mchango wetu sisi wengine tulio pembeni katika ukombozi wa taifa letu. Tunategemea uongozi wenu.
 
Siku yakimkuta mama yako mzazi ndio itaeleweka kama shetani ana rafiki au la .

what goes around comes around

Kuna list ya mijamaa ambayo hamna hata haja ya kubishana nayo.

Ikisikia Chadema, Mbowe, katiba mpya au hata chanjo na tahadhari ya Corona inakuwa fulu kupagawa.

Pana haja ya kuipuuza yenyewe, nyuzi na hata comments zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…