Tungekuwa wapi leo bila Rais Samia?

Kwenye kupanda daraja na VRF ya bodi ya mikopo mie ni mnufaika. Kwa hili namshukuru Mama Samia.

Mungu azidi kumpa afya na busara aweze kuongoza kwa haki.
Hata Wale wote wanaompinga na wao niwanufaika tu
 
... kwani wasiojulikana wamewahi ku-exist? Kama jibu ni ndio, awachukulie hatua na haki ionekane inatendeka ili tumshukuru badala ya kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa kama unavyojaribu kufanya ewe mnafiki!
Umewasikia tena tangu Rais Samia Suluhu Hassan awe madarakani
 

Umesahau kuweka namba yako ya simu
 
( unayempinga Rais Samia leo Je umewahi kujiuliza kama ungekuwa hai mpaka leo kama sio huyu Rais Samia unayempinga leo?)

DAAH HANGAYA AKUKUMBUKE TU KWENYE TEUZI ZIJAZO.
 
Hata mwaka hajatimiza Mheshimiwa Rais Mama Samia ameonyesha kutotetereka. Miradi ya Watangulizi wake anaikamilisha na miradi mipya juu. Kwenye siasa hakuna hoja za msingi toka kwa Wapinzani. Waliojaribu kumuyumbisha wamefyatuliwa.....


Sikutegemea haya kama angeweza kuyafanya. Kila siku anazidi kukomaa kisiasa na kiuongozi.
 
( unayempinga Rais Samia leo Je umewahi kujiuliza kama ungekuwa hai mpaka leo kama sio huyu Rais Samia unayempinga leo?)

DAAH HANGAYA AKUKUMBUKE TU KWENYE TEUZI ZIJAZO.

Mkuu kwani ukiandika lazima uteuliwe? Lazima tujifunze kuisemea nchi yetu na rais Wetu Vizuri.
 
Hilo genge la jiwe la watekaji amelisambaratisha kweli?
Wangapi Kati yao tayari wamo Lupango?!!
8. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angewaachilia huru Mashekhe wetu wa uamsho waliosota gerezani kwa miaka zaidi ya 10 bila kosa au Nani angewaachia Wana-CHADEMA waliokuwa wametapakaa karibu kila gereza hapa Tanzania?
Kweli mashekhe aliwaachia, ila hao wa Cdm wengi bado wamo ndani!!!

#Kama Sio Katiba kwa kudra za mwenyezi Mungu huyu Mama alitakiwa apewe miaka 20 ila katiba iheshimiwe twende na Mama mpaka 2030 itatufaa sana,Wewe unasemaje?
2025 inatosha mkuu

Mengine ni propaganda tuu
 
Mama anastahili pongezi nyingi
 
Machozi yamelinga hii mada aise, Mungu amlinde huyu Mama
Yote Tisa maelezo haya ndio kwangu muhimu sana kwa uwepo wake: " Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu,Je watu wasiojulikana wangekuwa wamepoteza wenzetu wengine wangapi mpaka leo,Wewe unayempinga Rais Samia leo Je umewahi kujiuliza kama ungekuwa hai mpaka leo kama sio huyu Rais Samia unayempinga leo?"

Asikudanganye mtu, uhai ndio kila kitu. Na mtu yeyote yule anayejinasibu au kuwa maarufu kwa kutoa uhai wa binaadamu wenzake, atapatwa na madhara makubwa sana huko mbeleni.

M Mungu ampe maisha marefu Rais wetu Samia Suluhu Hassan.
 
Tupo hapa leo badala ya kule kutokana na fikra duni kama hizi...., Kudhani kwamba tunahitaji mtu ili kufika au kutufikisha kule na sio kwamba kwa umoja wetu wote ndio either tutafikishana mbele au kurudishana nyuma....

It's all on Us....
 
Hilo genge la jiwe la wasiojulikana amelisambaratisha kweli?
Wangapi Kati yao wapo Lupango?!!

Kweli mashekhe aliwaachia, ila hao wa Cdm wengi bado wamo ndani!!!


2025 inatosha mkuu

Mengine ni propaganda tuu
MKUU Mama is here to stay mpaka 2030
 
Hivi wewe una akili kweli?
Wasio julikana Kila siku wapo mahakamani kutoa ushahidi ili wamfunge Mbowe.
Wasio julikana sasa wanajulikana Nani kawashughurikia zaidi ya kuwapandisha vyeo!
Kwa akili yako unadhani walikuwa wakimtumikia mwenda zake?
Walikuwa wanaitumikia Dora na Hadi sasa bado wapo kazini.
Kama wewe Ni mjinga hivyo sisi sio.
 
Sina cha kuongeza

R.I.P JPM
 
Unaoushahidi kuwa ni hao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…