Hebu toka ndani ya mioyo yetu tutafakari haya kwa pamoja huku tukimshirikisha Mungu wetu:
1. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu,Je watu wasiojulikana wangekuwa wamepoteza wenzetu wengine wangapi mpaka leo,Wewe unayempinga Rais Samia leo Je umewahi kujiuliza kama ungekuwa hai mpaka leo kama sio huyu Rais Samia unayempinga leo?
2. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu tungefanyaje kumaliza upungufu wa madarasa wa miaka mingi yapatayo elfu 15 sawa na madarasa matatu katika kila Shule ya Sekondari ya Serikali nchi nzima na mengi elfu 3 kwa shule za msingi Shikizi najua mnajua kabla yake tulisema Tanzania hatuna maambukizi ya Covid 19,
3. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nilini tungekusanya kodi inayofikia Shilingi trilioni 2.51 kwa mwezi mmoja tena bila kunyanyasa wala kukimbiza walipakodi wetu,Kwani simnakumbuka Mzee Jakaya yeye alikusanya wastani wa trilioni 10 kwa mwaka mzima??!!
4. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angeweza kuongeza mzunguko wa fedha kwenye nchi ( M3 ) kwa mara mbili zaidi kutoka asilimia 6.5 hadi asilimia 12.7 tena kwa miezi tisa tu,
5. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angeufikisha Uchumi wetu ukuaji wa Pato la Taifa la asilimia 5.4 kutoka mdororo wa asilimia 2.1 wakati wa mtangulizi wake,
6. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu ni lini tungeifikia sera yetu ya 50/50 kwenye nyadhifa mbalimbali za Kivyama, kiserikali na taasisi nyingine mbalimbali kwani kupitia yeye Tanzania na dunia vimejifunza kuwa ni kweli kuwa " A Woman Can Lead anywhere "
7. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angeinusuru miradi hii mikubwa ya kimkakati ya SGR na SG iliyokuwa ikijengwa kwa mikopo ya masharti ya kibiashara,Je umewahi kuwaza nini ingekuwa hatma ya Tanzania na Watoto wa Watanzani kwa madeni haya hatari ya kibiashara?
8. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angewaachilia huru Mashekhe wetu wa uamsho waliosota gerezani kwa miaka zaidi ya 10 bila kosa au Nani angewaachia Wana-CHADEMA waliokuwa wametapakaa karibu kila gereza hapa Tanzania?
9. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angeifungua Tanzania kimataifa baada ya kuchafuliwa vibaya na kwa muda mrefu na akina Tundu Lissu na wenzake kiasi cha kunyimwa misaada na mikopo ya masharti|riba nafuu kulikotulazimu kama Taifa kuanza kuiingiza nchi yetu kwenye mikopo ya kibiashara wakati nchi haifanyi biashara ila inatoa huduma,
10. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angewaongeza mishahara na madaraja makubwa makubwa watumishi wetu waliosota miaka mitano mfululizo bila kuona senti ya Serikali?
11. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu angewaondolea Wasomi wetu VRF ya asilimia 6 toka makato ya asilimia 15 toka HESLB kwani leo wanakatwa 9% tu tena mpaka upate kazi ndio uanze kukatwa,
12. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angeivusha CCM yangu mwaka wa Uchaguzi 2024|25 hii ni baada ya CCM yangu kabla ya Rais Samia kupoteza ushawishi kwa jamii|Umma kutokana na matendo ya Serikali yake,
#Kama Sio Katiba kwa kudra za mwenyezi Mungu huyu Mama alitakiwa apewe miaka 20 ila katiba iheshimiwe twende na Mama mpaka 2030 itatufaa sana,Wewe unasemaje?