Mwananchi Huru
JF-Expert Member
- Nov 20, 2021
- 2,128
- 1,896
- Thread starter
-
- #41
Mungu ni mkubwa mno,Yote Tisa maelezo haya ndio kwangu muhimu sana kwa uwepo wake: " Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu,Je watu wasiojulikana wangekuwa wamepoteza wenzetu wengine wangapi mpaka leo,Wewe unayempinga Rais Samia leo Je umewahi kujiuliza kama ungekuwa hai mpaka leo kama sio huyu Rais Samia unayempinga leo?"
Asikudanganye mtu, uhai ndio kila kitu. Na mtu yeyote yule anayejinasibu au kuwa maarufu kwa kutoa uhai wa binaadamu wenzake, atapatwa na madhara makubwa sana huko mbeleni.
M Mungu ampe maisha marefu Rais wetu Samia Suluhu Hassan.
Kwani hii mada inajambo gani baya mkuu au wewe unachuki tu Rais Samia Suluhu Hassan,
mfumuko wa bei mbona ni dunia nzima?
Hilo la mhimili wa bunge kuwa mbovu chondechonde usimlaumu mama, maana hata mbingu zitakushangaa. Hayati Magufuli alichokifanya kwenye uchaguzi mkuu 2020 ni ajabu sana kutegemea kuwa na bunge imara. Bunge imara liliishia miaka ya 2017 huko hayati alipoanza kulinajisi bunge.Ningekua hapahapa Tanzania nilipo sasa hivi ila haya yafuatayo yasingekuwepo.
Tusingekua tunatoa tozo.
Wanaomiliki nyumba wangeendelea kulipia kodi za majengo bila kuathiri bei ya umeme.
Tusingeona jinsi mhimili mmoja ulivyo dhaifu na wanaoutengeneza huo muhimili kuwa wanafiki na wanaojali matumbo yao zaidi kuliko kazi ya kuwakilisha wananchi.
Bei za vitu zisingeruka namna hii kama hali ilivyo sasa.
Amina.Kwenye kupanda daraja na VRF ya bodi ya mikopo mie ni mnufaika. Kwa hili namshukuru Mama Samia.
Mungu azidi kumpa afya na busara aweze kuongoza kwa haki.
Yaani huo wimbo, hata JPM alikuwa anaimbiwa hivyo hivyo!Ngoja aje Rais mwingine,mtaanza kumshambulia Samia,machawa ni kama funza tu!
Mungu akusaidie mkuu wanguMkuu mfumuko hadi kwenye vyakulaa?? Unazingua ujue. Toka kwa shemeji yako hapo ndo utajua nn sisi wakubwa tunaongea
Mkuu zama zimebadilika lakini ujueYaani huo wimbo, hata JPM alikuwa anaimbiwa hivyo hivyo!
Mama atawale tu mpaka achoke tumemkubali sana,Hebu toka ndani ya mioyo yetu tutafakari haya kwa pamoja huku tukimshirikisha Mungu wetu:
1. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu,Je watu wasiojulikana wangekuwa wamepoteza wenzetu wengine wangapi mpaka
Mungu ni fundi sana,Kitu cha kwanza kinachonipa furaha katika utawala huu na ambacho kutoweka kwake kulinipa tabu sana na kupelekea kuichukia sana awamu iliyopita, japo najua watanzania sisi ni wasahaulifu na tayari wengi wameshasahau, ni FREEDOM OF SPEECH na ukatili wa wasiojulikana ambao ulitumika kuondoa kabisa hiyo. freedom.
Nafahamu mama ni binadamu na ana makosa yake mengi tu, ila kwa hili, jinsi ninavyoona na kusikia watanzania wengi wakijiachia kwa uhuru kabisa kuukosoa na kuutusi utawala wa awamu hii bila hofu, nasamehe hayo makosa mengine yote. Namuombea asije kubadilika kabisa.
Katika awamu iliyopita ilikuwa ni kuchunga kila kauli, tulielekea mahala hata ukitaka kukohoa unaangalia pande zote kama hufuatiliwi! Ilikuwa ni unakihofia hata kivuli chako, hukiamini! Watu tulichukua kadi za ccm bila kupenda! Yaani nikisikia mtu anasifia ile awamu na kuiponda hii huwa nasikitika sana!
Sikupenda kifo cha Magu, ila utawala wake niliuondoa kabisa kichwani mwangu na nikaacha kuuombea (kama alivyotuomba) tangu 7/9/2017.
Hata USA kuna mfumuko wa bei, kwa hiyo Joe Budden ameshindwa kutawala America.??Samia ndo rais mwenye machawa wengi sana. Yani mtu akitaka teuzi anasifia sifia hata kama ujinga ili aonekane.
Ila ukweli huyu mama nchi imenshinda mfumuko wa bei za bidhaa kila kona, maisha yamekua magumu sana. Mfuko wa cement juu, bati juu, nondo usisemeee aisee mama anaupiga mwingi.
Kwa taarifa yako, Dikteta wa Chato ndiye alikuwa kopa kopa kuliko Marais wote waliomtangulia. Ila kwa UPUMBAVU wenu aliwadanganya kuwa ni fedha za ndani na mkakubaliTumegeuka ombaomba gafla toka kutaka kupunguza utegemezi ,aibu sana kwa taifa
Kwani AWAMU ya 5 inaisha lini? Je ukihudumu AWAMU ya 5 unaruhusiwa kuhudumu tena AWAMU YA 6?Hebu toka ndani ya mioyo yetu tutafakari haya kwa pamoja huku tukimshirikisha Mungu wetu:
1. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu,Je watu wasiojulikana wangekuwa wamepoteza wenzetu wengine wangapi mpaka leo,Wewe unayempinga Rais Samia leo Je umewahi kujiuliza kama ungekuwa hai mpaka leo kama sio huyu Rais Samia unayempinga leo?
Weka yako itafaa tu mkuu
Kwa taarifa yako, Dikteta wa Chato ndiye alikuwa kopa kopa kuliko Marais wote waliomtangulia. Ila kwa UPUMBAVU wenu aliwadanganya kuwa ni fedha za ndani na mkakubali
Mbona namuona anatajwa mpaka JK?Kwani AWAMU ya 5 inaisha lini? Je ukihudumu AWAMU ya 5 unaruhusiwa kuhudumu tena AWAMU YA 6?
Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
Umeme kila kona wanao tayariWatu walikubali na kuridhika kutokana na vitu ambavyo amefanya, just emagine miaka mitano umeme ni elf 27 now hata mwaka mmoja bado umeme laki sita hahaha
-Hatuna tishio la kutekwa na WASIOJULIKANAMachozi yamelinga hii mada aise, Mungu amlinde huyu Mama
Waliopata ni wengiUmeme kila kona wanao tayari