Kitu cha kwanza kinachonipa furaha katika utawala huu na ambacho kutoweka kwake kulinipa tabu sana na kupelekea kuichukia sana awamu iliyopita, japo najua watanzania sisi ni wasahaulifu na tayari wengi wameshasahau, ni FREEDOM OF SPEECH na ukatili wa wasiojulikana ambao ulitumika kuondoa kabisa hiyo. freedom.
Nafahamu mama ni binadamu na ana makosa yake mengi tu, ila kwa hili, jinsi ninavyoona na kusikia watanzania wengi wakijiachia kwa uhuru kabisa kuukosoa na kuutusi utawala wa awamu hii bila hofu, nasamehe hayo makosa mengine yote. Namuombea asije kubadilika kabisa.
Katika awamu iliyopita ilikuwa ni kuchunga kila kauli, tulielekea mahala hata ukitaka kukohoa unaangalia pande zote kama hufuatiliwi! Ilikuwa ni unakihofia hata kivuli chako, hukiamini! Watu tulichukua kadi za ccm bila kupenda! Yaani nikisikia mtu anasifia ile awamu na kuiponda hii huwa nasikitika sana!
Sikupenda kifo cha Magu, ila utawala wake niliuondoa kabisa kichwani mwangu na nikaacha kuuombea (kama alivyotuomba) tangu 7/9/2017.