Tungekuwa wapi leo bila Rais Samia?

Tungekuwa wapi leo bila Rais Samia?

Mimi nimeona kuna kitu raisi wa awamu ya tano mama $$H ameshakihisi kutokana na kesi nyingi zinazoendeshwa mahakamani kukosa ushahidi na hivyo kuchukua hatua ya kubadilisha kifungu cha katiba ya sheria ya mwaka 2021 Na.7 131A kwamba ili mtu yeyote ,,,, awe DPP,polisi,au mtu mwenye haki ya kutoa mashitaka na kumfikisha mtu mahakamani ni lazima awe na upelelezi ulio kamilika na kithibitisho cha ushahidi. ili kuepuka watu kuwekwa rumande huku upelelezi unaendelea.........Hii hata mimi niliona ni kupotezeana muda..kwasababu, upelelezi unafanyika miaka 5 halafu hukumu inakuja kupitishwa unahukumiwa miaka 2 hauoni ni dharau hii eti upo kizuizini..Maana ya upelelezi ni kwamba bado hauna uthibitisho kwamba mimi ndo muhusika wa tukio( mtenda)....
swala hili nimeliona kwa upande wa kesi ya mbowe na pamoja kwa aliyekuwa mkuu wa mkoa Paul makonda kufunguliwa mashitaka..kwa hili swala la makonda huyu jamaa anapoteza muda wake Angemwachia mungu tu sababu kunautofauti mkubwa ni sawa na machinga amshitaki bhakresa kwamba alishawahi kuchukua bidhaa kwake na hakumlipa sasa hapo nani atakaa rumande [emoji1787][emoji1787][emoji1787]..kwanza mimi nahisi kuna ile kauli ukienda kituo cha polisi UNAAMBIWA NJOO KESHO ukiona umeambiwa zaidi ya mara 3 nakuendelea achana na hiyo kesi pita hivi
 
Unalazimisha kiki mzee
Je,Tanzania ingekuwa wapi kama ingepata kiongozi mzalendo?

1: Uchumi wa Tanzania ungekuwa wa kati daraja la juu tofauti na hali ilivyo sasa ambapo Tanzania imeporomoka kutoka nafasi yake ya 8 kati ya nchi 10 zenye uchumi bora Africa mpaka nje ya top 10 na kuzidiwa na vinchi kama Ghana na Angola

2: Nidhamu na uwajibikaji kazini ungekuwepo.Leo hii tunashuhudia wananchi wakihoji kuhusu hali ya umeme nchini pasipokuwa na majibu au majibu yenye uwalakini. Lakini pamoja na hayo bado viongozi wamebaki wakiwa maofisini pasipo kuwajibika kwa namna yoyote.

3: Kwa miaka kadhaa Tanzania imekuwa ikiifanya juhudi kubwa kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa na ya kimkakati. Licha ya kwamba tangu Rais S.S.H aingie madarakani hakuna mradi wowote wa kimkakati ulioanzishwa bali pia hata ile miradi iliyokuwa ikiendelea imekuwa ikisuasua

4: Umeme usingekuwa wa mgao.Tangu Rais S.S.H aingie madarakani hali ya upatikanaji wa umeme nchini imekuwa mbaya sana.Hali hii imepelekea kurejea kwa mgao wa umeme ambao watanzania wengi walishausahau tangu miaka kadhaa iliyopita.Hali inayopelekea kuwatesa wananchi hususan wale wanaotegemea umeme kujipatia vipato katika shughuli zao za kila siku.

5; Hali ya upatikanaji wa maji imekuwa ya kusuasua.Kwa miezi kadhaa hususan katika jiji la Dar es salaam pamekuwa na mgao wa maji.Hali iliyopelekea kukosekana kwa maji kwa muda mrefu katika maeneo mengi.Hali ambayo hakuwahi kushuhudiwa hapo awali.

6: Tozo zisizokuwa na tija na zilizoua uchumi wa wengi.Serikali ya awamu ya sita imedhulumu na kunyang'anya kwa nguvu fedha za wananchi kwa kigezo cha tozo katika miamala ya simu.Mama mjane anapomtumia mgonjwa wake hospitali kwa ajili ya matibabu anakatwa fedha ambayo kimsingi haikuwa ya biashara. Kwa mujibu wa report kutoka Vodacom hivi karibuni miamala ya simu imepungua kwa asilimia zaidi ya 30!.Hili si jambo la kupuuza hata kidogo kwa uchumi wa nchi.Ni sawa na kutoa fedha mfuko wa kushoto na kuhamishia Kulia.

7: Kupanda kwa bei ya Mbolea.Mara tu baada ya awamu ya sita kuingia madarakani bei ya mbolea ilipanda karibu mara mbili ya bei ya awali.Hii ni imepelekea uchumi wa watanzania wengi ambao ni masikini na wanategemea kilimo kudhoofika.

8; Kupanda kwa bei ya mafuta ya kupikia
9; Kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol
10; Kupanda kwa bei ya bidhaa za ujenzi kama cement,Nondo n.k
11; Teuzi za viongozi wasiokuwa na weledi kwa kigezo cha favour/Undugu/Kujuana (Mf. Riziwani Kikwete,Nape Nauye n.k) Tanzania ina vijana wasomi na wenye upeo mpana wa kifikra. Lakini cha kushangaza teuzi zimekuwa hazina matumaini ta kuipeleka Tanzania kule tunapotarajia.

12: Ukosefu wa uzalendo na ubadhirifu miongoni mwa watumishi wa umma.Siku si nyingi tumeshuhudia kiongozi mkuu wa serikali akiwaasa watumishi wake wale kwa urefu wa kamba zao.Hii inaashiria kwamba hata kiongozi mkuu anashiriki katika ulaji huo.Hali hii ni hatari kwa rasilimali za nchi.

13; Wananchi hususan wa hali ya chini kukosa nafasi katika nchi yao.Siku si nyingi tumeshuhudia wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga wakinyanyaswa kwa kuhamishiwa katika maeneo yasiyokuwa tija kwao.Vuta nikuvute hii imepelekea hali ya unyonge na sintofahamu miongoni mwao na kupelekea kuongezeka kwa umasikini miongoni mwa watanzania

14; Mikopo isiyokuwa na tija kwa taifa.Tangu Tanzania ipate uhuru viongozi wake wote walisisitiza kufanya mambo yetu kwa fedha zetu wenyewe bila kutegemea wahisani. Tanzania imebarikiwa rasilimali za kila aina.Mito,Maziwa,Bahari,Madini kama Tanzanite,Mbuga za wanyama,Gesi n.k Inashangaza Sana kuona kiongozi badala ya kusisitiza au kubuni namna ya kuzitumia rasilimali hizi ziweze kuwa na tija kwa watanzania,Badala yake tumekuwa tukijivunia mikopo!

15 ; Kuongezeka kwa gharama za uunganishaji umeme kutoka 27,000 iliyokuwepo mpaka zaidi ya 300,000 ya hivi sasa.Hali hii imepunguza mno kasi ya usambaaji wa umeme

16 ; Muingiliano baina ya mihimili kwa kigezo cha uchama.Inasikitisha kuona kiongozi wa mhimili mmoja anakosa uwezo wa kuikosoa na kuurekebisha mhimili mwingine kwa kuhofia kibarua chake.hili tumelishuhudia baada ya kuona spika wa bunge la JMT kujiuzulu baada ya kuhoji kuhusu mikopo na tozo.

17 ; Safari zisizokuwa na tija wala umuhimu kwa taifa.Tumeshuhudia safari nyingi mno za nje ya nchi,Safari hizi zimekuwa zikiigharimu nchi fedha nyingi.Safari za vikao visivyokuwa na tija kama mkutano wa kujadili athari za gesi ya ukaa sidhani kama ina tija hususan kwa nchi ambazo bado uchumi wake ni mdogo

18 ; Kukosekana uhuru na ukandamizaji wa demokrasia. Tunaweza kusema kwamba pia hata katika awamu zilizopita hili lilikuwepo, Lakini hili la sasa limekuja kwa namna tofauti.Wakati mwingine baba anaweza kumpa mtoto adhabu ya kulima shamba,Mtoto akalia na kulaumu sana,Lakini shamba hilohilo baadaye likaleta chakula mezani wote wakala na kufurahia. Ila tofauti iliyopo sasa,Hakuna chakula kinachokuja mezani!

19 ; Kushughulikia zaidi mambo yasiyokuwa na tija kwa wananchi kuliko yale yenye umuhimu na tija kwa watanzania. Imekuwa jambo la kawaida kwa awamu hii kujihusisha zaidi na makongamano,Semina elekezi,Birthday Party pamoja na hafla mbali mbali badala ya kujikita katika kufufua na kubuni miradi ya kimaendeleo itakayosaidia kuwapunguzia wananchi mzigo wa umasikini na kuinua uchumi.Hafla ya machifu na watemi si muhimu kama hafla ya utiaji saini mradi wa uchimbaji na usambazaji wa gesi ya Mtwara!

20 ; Kukosekana ajira. Ubunifu na uibuaji wa miradi mipya si tu umekuwa na tija kiuchumi Bali umekuwa ukiajiri vijana wengi.Kukosekana kwa ubunifu na sera mbovu za serikali zimesababisha kukoseka kwa ajira miongoni mwa vijana wengi

21 ; Kuongezeka matukio ya uhalifu.
Mara tu baada ya awamu ya sita kushika hatamu sote tumeshuhudia jinsi wimbi la uhalifu lilivyoongezeka.Sio tu matukio ya wizi na ujambazi bali mpaka uchomaji wa masoko kama Kariakoo, mchikichini n.k wizi mauaji na utekaji nyara vimeongezeka kwa kasi mno. Hii inaonyesha udhaifu katika usimamizi wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama

22 ; Kuongezeka gharama za simu
Kutokana na kodi za miamala Kuongezeka kampuni za simu zimejikuta zikilazimika kupandisha gharama za muda wa maongezi na huduma zinginezo za simu kama vile huduma za vifurushi ili kuweza kubalance gharama za uendeshaji. Hali hii imesababisha mzigo mzito kwa wananchi hasa ukizingatia mawasiliano ni nyenzo muhimu sana katika shughuli zao za kila siku

Hakika ni mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanyika kinyume na matarajio ya watanzania wengi ambao waliwaamini viongozi wao na kuwaweka madarakani huku wakiwa na matumaini makubwa ya kuondokewa na maradhi, ujinga na umasikini ambao ndio maadui wakuu wa taifa kama ilivyobainishwa na Mwl Nyerere badala yake watanzania hao ambao wengi ni masikini na wameteseka kwa umasikini kiasi cha kusahau tarehe zao za kuzaliwa huku wakishuhudia wale waliowachagua wakikata keki ikulu!

Wacha kazi iendelee!
 
Toka ndani ya mioyo yetu tutafakari haya kwa pamoja huku tukimshirikisha Mungu wetu:

1. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu,Je watu wasiojulikana wangekuwa wamepoteza wenzetu wengine wangapi mpaka leo, Wewe unayempinga Rais Samia leo Je umewahi kujiuliza kama ungekuwa hai mpaka leo kama sio huyu Rais Samia unayempinga na kumbeza kila leo?

2. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu tungefanyaje kumaliza upungufu wa madarasa wa miaka mingi yanayofikia elfu 15 sawa na wastani wa madarasa matatu katika kila Shule ya Sekondari ya Serikali nchi nzima na mengine zaidi ya elfu 3 kwa shule za msingi Shikizi najua mnajua kabla tulisema Tanzania hatuna maambukizi ya Covid 19 hivyo tusingeweza kupata mkopo ule usio na riba,

3. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nilini tungekusanya kodi inayofikia Shilingi trilioni 2.51 kwa mwezi mmoja tena bila kunyanyasa wala kukimbiza walipakodi wetu,Kwani simnakumbuka Mzee Jakaya yeye alikusanya wastani wa trilioni 10 kwa mwaka mzima pesa tunayoweza kuikusanya kwa miezi minne tu sasa!!

4. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angeweza kuongeza mzunguko wa fedha kwenye nchi ( M3 ) kwa mara mbili zaidi kutoka asilimia 6.5 hadi asilimia 12.7 tena kwa miezi tisa tu,

5. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angeufikisha Uchumi wetu kwenye ukuaji wa Pato la Taifa wa asilimia 5.4 kutoka mdororo wa asilimia 2.1 wakati wa mtangulizi wake,

6. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu ni lini tungeifikia sera yetu ya 50/50 kwenye nyadhifa mbalimbali za Kivyama, kiserikali na taasisi nyingine mbalimbali kwani kupitia yeye Tanzania na dunia vimejifunza kuwa ni kweli kuwa " A Woman Can Lead anywhere at any Post "

7. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angeinusuru miradi hii mikubwa ya kimkakati ya SGR na SG iliyokuwa ikijengwa kwa mikopo ya masharti ya kibiashara,Je umewahi kuwaza nini ingekuwa hatma ya Tanzania na Watoto wa Watanzani kwa madeni haya hatari ya kibiashara?

8. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angewaachilia huru Mashekhe wetu wa uamsho waliosota gerezani kwa miaka zaidi ya 10 bila kosa au Nani angewaachia Wana-CHADEMA waliokuwa wametapakaa karibu kila gereza hapa Tanzania?

9. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angeifungua Tanzania kimataifa baada ya kuchafuliwa vibaya na kwa muda mrefu na akina Tundu Lissu na wenzake kiasi cha kunyimwa misaada na mikopo ya masharti|riba nafuu kulikotulazimu kama Taifa kuanza kuiingiza nchi yetu kwenye mikopo ya kibiashara wakati nchi haifanyi biashara ila inatoa huduma tu hili lilikuwa ni bomu kwa nchi,

10. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angewaongezea mishahara na madaraja makubwa makubwa watumishi wetu wa Serikali waliosota miaka mitano mfululizo bila kuona senti ya Serikali?

11. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angewaondolea Wasomi wetu VRF ya asilimia 6 toka makato ya asilimia 15 toka HESLB kwani leo wanakatwa asilimia 9 tu tena mpaka upate kazi ndio uanze kukatwa,

12. Kama sio Rais Samia Suluhu Hassan kupewa kibali na Mungu nani angekivusha Chama Changu cha Mapinduzi Salama mwaka wa Uchaguzi 2024|25 ikiwa ni baada ya Rais Samia kurudisha Ushawishi wa Chama kwa jamii|Umma kutokana na matendo mema na mazuri ya Chama Chake na Serikali yake,

#Kama Sio katazo la Katiba kwa kudra za mwenyezi Mungu huyu Mama alitakiwa apewe miaka 20 ila katiba iheshimiwe twende na Mama mpaka 2030 itatufaa sana,Wewe unasemaje?

Mama wala hajui nani anagombea 2025 kum challenge.
1.Bila samia tungekuwa tumeshajua.

2.Miradi ingekuwa imekamilika sasa hivi hatujui bwawa letu lini litawekewa maji ninachoona tu gesi ya wapigaji ndio inapelekwa Ubungo izalishe umeme. Train yetu nayo iko gizani naona wanabinafsisha kwa wachina.

3.Umeme usingekatikakatika

4.Maji yasingekuwa ya mgao

5.Mawaziri wasingekuwa wanakula kwa urefu wa kamba zao

6.Upigaji bandarini usingekuwepo.

7. Makamba na Nauye wangekuwa si mawaziri Kizazi kilcho corrupt

8. Kikwete asinge endesha nchi

9.Magu asingeenda kukopa 178 euro toka Ufaransa etc
 
Huu ni Uchochezi
 
Je,Tanzania ingekuwa wapi kama ingepata kiongozi mzalendo?

1: Uchumi wa Tanzania ungekuwa wa kati daraja la juu tofauti na hali ilivyo sasa ambapo Tanzania imeporomoka kutoka nafasi yake ya 8 kati ya nchi 10 zenye uchumi bora Africa mpaka nje ya top 10 na kuzidiwa na vinchi kama Ghana na Angola

2: Nidhamu na uwajibikaji kazini ungekuwepo.Leo hii tunashuhudia wananchi wakihoji kuhusu hali ya umeme nchini pasipokuwa na majibu au majibu yenye uwalakini. Lakini pamoja na hayo bado viongozi wamebaki wakiwa maofisini pasipo kuwajibika kwa namna yoyote.

3: Kwa miaka kadhaa Tanzania imekuwa ikiifanya juhudi kubwa kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa na ya kimkakati. Licha ya kwamba tangu Rais S.S.H aingie madarakani hakuna mradi wowote wa kimkakati ulioanzishwa bali pia hata ile miradi iliyokuwa ikiendelea imekuwa ikisuasua

4: Umeme usingekuwa wa mgao.Tangu Rais S.S.H aingie madarakani hali ya upatikanaji wa umeme nchini imekuwa mbaya sana.Hali hii imepelekea kurejea kwa mgao wa umeme ambao watanzania wengi walishausahau tangu miaka kadhaa iliyopita.Hali inayopelekea kuwatesa wananchi hususan wale wanaotegemea umeme kujipatia vipato katika shughuli zao za kila siku.

5; Hali ya upatikanaji wa maji imekuwa ya kusuasua.Kwa miezi kadhaa hususan katika jiji la Dar es salaam pamekuwa na mgao wa maji.Hali iliyopelekea kukosekana kwa maji kwa muda mrefu katika maeneo mengi.Hali ambayo hakuwahi kushuhudiwa hapo awali.

6: Tozo zisizokuwa na tija na zilizoua uchumi wa wengi.Serikali ya awamu ya sita imedhulumu na kunyang'anya kwa nguvu fedha za wananchi kwa kigezo cha tozo katika miamala ya simu.Mama mjane anapomtumia mgonjwa wake hospitali kwa ajili ya matibabu anakatwa fedha ambayo kimsingi haikuwa ya biashara. Kwa mujibu wa report kutoka Vodacom hivi karibuni miamala ya simu imepungua kwa asilimia zaidi ya 30!.Hili si jambo la kupuuza hata kidogo kwa uchumi wa nchi.Ni sawa na kutoa fedha mfuko wa kushoto na kuhamishia Kulia.

7: Kupanda kwa bei ya Mbolea.Mara tu baada ya awamu ya sita kuingia madarakani bei ya mbolea ilipanda karibu mara mbili ya bei ya awali.Hii ni imepelekea uchumi wa watanzania wengi ambao ni masikini na wanategemea kilimo kudhoofika.

8; Kupanda kwa bei ya mafuta ya kupikia
9; Kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol
10; Kupanda kwa bei ya bidhaa za ujenzi kama cement,Nondo n.k
11; Teuzi za viongozi wasiokuwa na weledi kwa kigezo cha favour/Undugu/Kujuana (Mf. Riziwani Kikwete,Nape Nauye n.k) Tanzania ina vijana wasomi na wenye upeo mpana wa kifikra. Lakini cha kushangaza teuzi zimekuwa hazina matumaini ta kuipeleka Tanzania kule tunapotarajia.

12: Ukosefu wa uzalendo na ubadhirifu miongoni mwa watumishi wa umma.Siku si nyingi tumeshuhudia kiongozi mkuu wa serikali akiwaasa watumishi wake wale kwa urefu wa kamba zao.Hii inaashiria kwamba hata kiongozi mkuu anashiriki katika ulaji huo.Hali hii ni hatari kwa rasilimali za nchi.

13; Wananchi hususan wa hali ya chini kukosa nafasi katika nchi yao.Siku si nyingi tumeshuhudia wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga wakinyanyaswa kwa kuhamishiwa katika maeneo yasiyokuwa tija kwao.Vuta nikuvute hii imepelekea hali ya unyonge na sintofahamu miongoni mwao na kupelekea kuongezeka kwa umasikini miongoni mwa watanzania

14; Mikopo isiyokuwa na tija kwa taifa.Tangu Tanzania ipate uhuru viongozi wake wote walisisitiza kufanya mambo yetu kwa fedha zetu wenyewe bila kutegemea wahisani. Tanzania imebarikiwa rasilimali za kila aina.Mito,Maziwa,Bahari,Madini kama Tanzanite,Mbuga za wanyama,Gesi n.k Inashangaza Sana kuona kiongozi badala ya kusisitiza au kubuni namna ya kuzitumia rasilimali hizi ziweze kuwa na tija kwa watanzania,Badala yake tumekuwa tukijivunia mikopo!

15 ; Kuongezeka kwa gharama za uunganishaji umeme kutoka 27,000 iliyokuwepo mpaka zaidi ya 300,000 ya hivi sasa.Hali hii imepunguza mno kasi ya usambaaji wa umeme

16 ; Muingiliano baina ya mihimili kwa kigezo cha uchama.Inasikitisha kuona kiongozi wa mhimili mmoja anakosa uwezo wa kuikosoa na kuurekebisha mhimili mwingine kwa kuhofia kibarua chake.hili tumelishuhudia baada ya kuona spika wa bunge la JMT kujiuzulu baada ya kuhoji kuhusu mikopo na tozo.

17 ; Safari zisizokuwa na tija wala umuhimu kwa taifa.Tumeshuhudia safari nyingi mno za nje ya nchi,Safari hizi zimekuwa zikiigharimu nchi fedha nyingi.Safari za vikao visivyokuwa na tija kama mkutano wa kujadili athari za gesi ya ukaa sidhani kama ina tija hususan kwa nchi ambazo bado uchumi wake ni mdogo

18 ; Kukosekana uhuru na ukandamizaji wa demokrasia. Tunaweza kusema kwamba pia hata katika awamu zilizopita hili lilikuwepo, Lakini hili la sasa limekuja kwa namna tofauti.Wakati mwingine baba anaweza kumpa mtoto adhabu ya kulima shamba,Mtoto akalia na kulaumu sana,Lakini shamba hilohilo baadaye likaleta chakula mezani wote wakala na kufurahia. Ila tofauti iliyopo sasa,Hakuna chakula kinachokuja mezani!

19 ; Kushughulikia zaidi mambo yasiyokuwa na tija kwa wananchi kuliko yale yenye umuhimu na tija kwa watanzania. Imekuwa jambo la kawaida kwa awamu hii kujihusisha zaidi na makongamano,Semina elekezi,Birthday Party pamoja na hafla mbali mbali badala ya kujikita katika kufufua na kubuni miradi ya kimaendeleo itakayosaidia kuwapunguzia wananchi mzigo wa umasikini na kuinua uchumi.Hafla ya machifu na watemi si muhimu kama hafla ya utiaji saini mradi wa uchimbaji na usambazaji wa gesi ya Mtwara!

20 ; Kukosekana ajira. Ubunifu na uibuaji wa miradi mipya si tu umekuwa na tija kiuchumi Bali umekuwa ukiajiri vijana wengi.Kukosekana kwa ubunifu na sera mbovu za serikali zimesababisha kukoseka kwa ajira miongoni mwa vijana wengi

21 ; Kuongezeka matukio ya uhalifu.
Mara tu baada ya awamu ya sita kushika hatamu sote tumeshuhudia jinsi wimbi la uhalifu lilivyoongezeka.Sio tu matukio ya wizi na ujambazi bali mpaka uchomaji wa masoko kama Kariakoo, mchikichini n.k wizi mauaji na utekaji nyara vimeongezeka kwa kasi mno. Hii inaonyesha udhaifu katika usimamizi wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama

22 ; Kuongezeka gharama za simu
Kutokana na kodi za miamala Kuongezeka kampuni za simu zimejikuta zikilazimika kupandisha gharama za muda wa maongezi na huduma zinginezo za simu kama vile huduma za vifurushi ili kuweza kubalance gharama za uendeshaji. Hali hii imesababisha mzigo mzito kwa wananchi hasa ukizingatia mawasiliano ni nyenzo muhimu sana katika shughuli zao za kila siku

Hakika ni mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanyika kinyume na matarajio ya watanzania wengi ambao waliwaamini viongozi wao na kuwaweka madarakani huku wakiwa na matumaini makubwa ya kuondokewa na maradhi, ujinga na umasikini ambao ndio maadui wakuu wa taifa kama ilivyobainishwa na Mwl Nyerere badala yake watanzania hao ambao wengi ni masikini na wameteseka kwa umasikini kiasi cha kusahau tarehe zao za kuzaliwa huku wakishuhudia wale waliowachagua wakikata keki ikulu!

Wacha kazi iendelee!
Copy and paste
 
Watanzania wanafiki sana hadi kinyaa!!! tunasifia hata tanganyika kuwa shamba la bibi la zenj
Ila ukweli ni kuwa hakuna serikali isiyokuwa na kibali cha Mungu kwa makusudi yake ya umilele! Hata serikali ya Hitler na Idi Amin ilikuwa na kibali cha Mungu. Serikali kuwa na kibali cha Mungu haina maana kuwa yote yafanywayo na serikali yanampendeza Mungu. Ndiyo maana watawala wote siku moja watasimama mbele za Mungu kutoa hesabu ya namna walivyotumia madaraka yao!!
Waliokuwa wanapiga pambio za sifa enzi za awamu ya tano leo ndio wanaoongoza kuilaani awamu hiyo huku wakijua kuwa tunawajua!!! Hao hao watakuja kuilaani awamu ya sita ikipita japo kwa sasa wanaipigia pambio za sifa! Huu unafiki unatia kinyaa!!!
 
Daaah, Wivu mbaya sana
 
You mean hata wewe ni mnafiki tu
 
Hakika Rais Samia ameletwa Tanzania kuliponya Taifa,

Kitendo cha kukutana na Tundu Lissu Brussels Ubelgiji ni kiwango cha juu kabisa cha Uzalendo kwa Taifa,

Tumuunge mkono Rais wetu kwa haya kwani anastahili sana,
 
Kazi iendelee Tanzania,Tuko salama sana na Mama Samia Suluhu,
 
Back
Top Bottom