Tuondoe aibu hii anayosababisha Spika Ndugai

Tuondoe aibu hii anayosababisha Spika Ndugai

Ibumalo

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2017
Posts
465
Reaction score
501
Nianze kwa kumshukuru Nape Nnauye kwa kutoa hoja iliyomtoa nyoka pangoni. Kwa muda sasa Watanzania wamekuwa wakijiuliza ni lini spika atajitokeza na kutoa kauli juu ya wabunge hao 19 wasio na chama.

Alipojitokeza amekuja na hoja zilizoongeza mkanganyiko ambazo zinahitimisha kwa msimamo kuwa wabunge hao anawatambua na ni wabunge halali.

Hajasema ametumia kipengele gani cha katiba, kanuni au mwongozo unaompa mamlaka hayo. Kwa mtazamo wangu mimi Ndugai amevunja katiba na anatumia ubabe kuendelea kuvunja katiba.

Katiba ni mali ya watanzania wote na kila mmoja wetu ana wajibu wa kuilinda. Kwa muktadha huo mimi ningependekeza mojawapo ya mambo yafuatayo yafanyike;

1) Wabunge wa CCM wapige kura ya kutokuwa na imani na spika. Wabunge wa kutosha wa aina ya Nape wakipatikaba Ndugai anaweza kutolewa na kutuachia katiba yetu.

2) Mwenyekiti wa chama chake cha CCM mama Samia Suluhu Hassan aitishe kikao cha CC cha chama jumjadili na kumshinikiza Ndugai achukue hatua staiki. Aibu anayofanya Ndugai ni kwa chama chake pia

3) Ili kufifisha aibu ya kulazimika kubadili msimamo spika awaombe hao wabunge wake wajiuzulu ili tuanze ukurasa mpya. Utaratibu uanze kwa CHADEMA kufuata taratibu zote zinazohusu uteuzi wa wabunge wa viti maalum.

4) Halima Mdee ni mwanasheria. Nakumbuka katika moja ya mijadala ya bunge lilopita Halima aliwahi kumtambia Prof. Kabudi kuwa yeye Halima ana Cheri cha uwakili. Nashauri aonyeshe umahiri wake wa sheria kwa kuheshimu katiba na kuamua kujiuzuru ili mchakato wa kikatiba na kisheria uchukue mkondo wake.

5) Spika wastaafu mama Anna Makinda na mzee Pius Msekwa mwiteni chemba kijana wenu huyu ambae mwenyewe anajigamba kupata uzoefu toka kwenu mwambieni anayoyatenda anakinajisi kiti cha spika aache na atekeleze matakwa ya kikatiba. Najua mzee Msekwa ukishalitolea ufafanuzi suala hili lakini ingefaa iwe ya mojakwamoja zaidi.

Nihitimishe kwa kutoa msisitizo kwamba mambo anayofanya Ndugai yanatuaibisha sisi sote kama taifa na kuonekana kuishi katika nchi ambamo viongozi wetu tumewaacha watuongoze kifalme bila kufuata taratibu za kikatiba.

Naomba kuwasilisha.
 
wabunge hao anawatambua na ni wabunge halali. Hajasema ametumia kipengele gani cha katiba, kanuni au mwongozo unaompa mamlaka hayo. Kwa mtazamo wangu mimi Ndugai amevunja katiba na anatumia ubabe kuendelea kuvunja katiba.
Hili suala la wabunge 19 wa Chadema, watu mnahamanika bure tuu. Tanzania tunafuata mfumo wa sheria wa Uingereza, common laws, ambao unafuata kanuni za natural justice. Kanuni ya kwanza inasema, everbody is presumed inocent until proven guilt, 2. no one is condemned unheard 3. The burden of proof, lies with the prosecution, the one who alleges, must prove.

Kwanini kina Halima wamehukumiwa bila kusikilizwa?. Kwa vile Spika kapelekewa majina na NEC, Chadema ndio the ones who alleges kuwa hao wabunge wame foji, and must prove, kuwa hawakuwateua, wala hawakuandika barua. Laiti mgejua Spika ana nini mkononi inayompa kiburi hivyo, CC ya Chadema isinge watimua, kwa pupa na kwa papara bila kwanza kujiridhisha majina hayo, yamefikishwa kwa Tume ya Uchaguzi kwa barua gani, iliyosainiwa na nani. Hapo ndipo kwenye mzizi wa fitna. Spika yeye kapelekewa majina tuu. Na sasa kikao cha BUK la Chadema, kitapindua maamuzi ya CC ya Chadema, mchezo utakuwa umekwisha.

Najua wengi humu, watatoa hoja kuwa wabunge hao waliitwa kupewa haki ya kusikilizwa, lakini sii wengi humu, wameisoma katiba ya Chadema na taratibu za kufuta wanachama, kwa faida ya wengi utaratibu ni huu.
  1. Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, ili kumvua mtu uanachama kuna mlolongo wa kanuni na taratibu za kufuatwa na miongoni mwake ni hizi nitakazo ziorodhesha hapa chini, jee zilifuatwa?.
  2. Kuandaa Hati ya Mashtaka kwa maandishi yenye tuhuma zote ambazo mtuhumiwa anakabiliwa nazo. Jee hati hizi za mashitaka kimaandishi ziliandaliwa?. Kina Halima walipewa hati za mashitaka?.
  3. Hati hiyo ya mashitaki kimaandishi inatakiwa ikabidhiwa kwa mtuhumiwa kwa "despatch" ili kuthibitisha imemfikia, jee hili lilifanyika?, nimesikia kuna watu waliitwa kwa simu, jee huu ndio utaratibu kwa jambo zito kama hili?.
  4. Mtuhumiwa atatakiwa kuzijibu tuhuma za mashitaka hayo kimaandishi ndani ya kipindi cha siku 14 tangu tarehe aliyopokea barua ile ili apate muda wa kutosha kutafakari, jee hili lilifanyika?. Mashitaka yanatolewa kwa maandishi na kujibiwa kwa maandishi, ndipo process ya kuitana na kusikilizwa shauri inafuata.
  5. Baada ya majibu ya hati ile ya mashitaka kurejeshwa, ndipo mamlaka ya nidhamu ingepaswa kuitisha kikao rasmi kwa mujibu wa katiba ya Chadema na kuwaalika watuhumiwa kwa barua ili kuwapa nafasi ya haki ya kusikilizwa, kwa kujieleza na kujitetea. Kumsikiliza mtuhumiwa kabla ya kufikia maamuzi ya kumhukumu ni moja ya haki muhimu kabisa!. Jee kwenye huo uamuzi huo wa kuwatimua, kwa nini watimuliwe uanachama bila kusikilizaa. Jee sheria, taratibu na kanuni zilifuatwa?!.
  6. Kwa wabunge wale 18 ni CC ya chadema ndio mamlaka yao ya nidhamu, lakini kwa, Mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee, CC ya Chadema sio mamlaka yake ya nidhamu, mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu, sasa CC ya Chadema, imepata wapi iwezo wa kumsimamisha uanachama Mdee?.
Nawaomba sana Chadema, msishabikie maamuzi ya CC ya Chadema kukaa kama a kangaroo court na kutoa maamuzi ya kuwatimua uanachama wanachama wake shupavu, walio ipigania Chadema kwa machozi, jasho na damu, mkumbuke kuna karma.

Tukisubirie Kikao cha Baraza Kuu, kama kita endorse uamuzi huu wa a kangaroo court ya CC, kitakachofuata ni nyote kushuhudia, jinsi karma, itakavyo washughulikia watu.

Kwa msio jua karma, na inafanya nini kwa Chadema, someni hapa, angalieni chanzo kilichosababisha haya yatokee, nini kilikuja kuwakuta hao visababishi?.

Just wait and see.
P
 
Hili suala la wabunge 19 wa Chadema, watu mnahamanika bure tuu. Tanzania tunafuata mfumo wa sheria wa Uingereza, common laws, ambao unafuata kanuni za natural justice. Kanuni ya kwanza inasema, everbody is presumed inocent until proven guilt, 2. no one is condemned unheard 3. The burden of proof, lies with the prosecution, the one who alleges, must prove.

Kwanini kina Halima wamehukumiwa bila kusikilizwa?. Kwa vile Spika kapelekewa majina na NEC, Chadema ndio the ones who alleges kuwa hao wabunge wame foji, and must prove, kuwa hawakuwateua, wala hawakuandika barua. Laiti mgejua Spika ana nini mkononi inayompa kiburi hivyo, CC ya Chadema isiwatumua, na sasa kikao cha BUK la Chadema, litapindua maamuzi ya CC ya Chadema, mchezo utakuwa umekwisha.

Just wait and see.
P
Mungu anisaidie, nisizeeke vibaya kama Pascal Mayala. Kama moja ya athari ya uzee ni kuwa hivi, hakika uzee unatisha.
 
Hili suala la wabunge 19 wa Chadema, watu mnahamanika bure tuu. Tanzania tunafuata mfumo wa sheria wa Uingereza, common laws, ambao unafuata kanuni za natural justice. Kanuni ya kwanza inasema, everbody is presumed inocent until proven guilt, 2. no one is condemned unheard 3. The burden of proof, lies with the prosecution, the one who alleges, must prove.

Kwanini kina Halima wamehukumiwa bila kusikilizwa?. Kwa vile Spika kapelekewa majina na NEC, Chadema ndio the ones who alleges kuwa hao wabunge wame foji, and must prove, kuwa hawakuwateua, wala hawakuandika barua. Laiti mgejua Spika ana nini mkononi inayompa kiburi hivyo, CC ya Chadema isiwatumua, na sasa kikao cha BUK la Chadema, litapindua maamuzi ya CC ya Chadema, mchezo utakuwa umekwisha.

Just wait and see.
P
Pascal Mayalla
Wewe ni mwandishi nguli na pia ni Mwanasheria, ngoja nikuulize swali jepesi, unasema kuwa hao wabunge wamehukumiwa bila kusikilizwa, hivi wakati CCM ilipoleta taarifa ya kumfukuza uanachama wake Sofia Simba na pale Profesa Lipumba alipowavua uanachama wao wale wabunge wa viti maalum, mbona Spika Ndugai aliwatimua ubunge wao papo kwa papo na hapakuwa na hiyo hoja kuwa hao wabunge hawajasikilizwa??

Hivi hizi sheria zina "double standards" katika utekelezaji wake??
 
Ummemjibu vema mchumia tumbo Pascal,
Pascal anatakiwa awalaumu wajumbe waliomkata kwenye kura za maoni,
Baada ya kuondoka mwenda zake,anafikili anaweza kupata nafasi kwa mwenyekiti mpya,
Lakini Pascal anaahindwa kutambua kuwa Kila zama na kitabu chake.
 
Hili suala la wabunge 19 wa Chadema, watu mnahamanika bure tuu. Tanzania tunafuata mfumo wa sheria wa Uingereza, common laws, ambao unafuata kanuni za natural justice. Kanuni ya kwanza inasema, everbody is presumed inocent until proven guilt, 2. no one is condemned unheard 3. The burden of proof, lies with the prosecution, the one who alleges, must prove.

Kwanini kina Halima wamehukumiwa bila kusikilizwa?. Kwa vile Spika kapelekewa majina na NEC, Chadema ndio the ones who alleges kuwa hao wabunge wame foji, and must prove, kuwa hawakuwateua, wala hawakuandika barua. Laiti mgejua Spika ana nini mkononi inayompa kiburi hivyo, CC ya Chadema isiwatumua, na sasa kikao cha BUK la Chadema, litapindua maamuzi ya CC ya Chadema, mchezo utakuwa umekwisha.

Just wait and see.
P
Nakumbuka hawa watu waliitwA kwenda kujitetea mbele ya kamati kuu dhidi Ya tuhuma zinazowakabili.lakini wao hawakwenda.katika muktadha huohuo uliosema wa sheria shauri linaweza kusikilizwa bila mtuhumiwa kuwepo iwapo tu atakua alipewa wito wakufika .
 
Katika jambo hili la c19,sijajua mpka sasa au labda sijasikia vizuri,Je wabunge hawa walifikaje huko bungeni?na kwa nini mara baada ya kuambiwa CDM haijateua wabunge bado Ndugai aliendelea na utaratibu wa kuwaapisha? Nao hao wabunge hawaoni aibu kwamba waliingia bungeni bila ridhaa ya chama.Tugeuke upande wa pili wa CDM,.mbona hiyo rufani yao waliyoikata haisikilizwi ili waka clear hii dust? naadha kuwahisi vibaya hawa CDM.kuna kitu Ndugai anakijua zaidi kuliko wengine wote.

Ni haki ya Watanzania wote kufuatilia na kupata ukweli juu ya hiyo tuhuma.

Hoja nyepesi ya Ndugai eti kuna unyanyasaji wa kijinsia ni kama koti tuu lililofunika kitu.So yeye ni mwanaharakati wa masuala ya jinsia.

Halafu,kitu kingine ambacho kinaacha maswali mengi,yaani upendo wa Ndugai wa kiasi hicho kwa wapinzani unatoka wapi?
 
Akisema abadilishe msimamo ataaibika yeye amarehemu aliyemtuma. Hapo patamu.
 
Hili suala la wabunge 19 wa Chadema, watu mnahamanika bure tuu. Tanzania tunafuata mfumo wa sheria wa Uingereza, common laws, ambao unafuata kanuni za natural justice. Kanuni ya kwanza inasema, everbody is presumed inocent until proven guilt, 2. no one is condemned unheard 3. The burden of proof, lies with the prosecution, the one who alleges, must prove.

Kwanini kina Halima wamehukumiwa bila kusikilizwa?. Kwa vile Spika kapelekewa majina na NEC, Chadema ndio the ones who alleges kuwa hao wabunge wame foji, and must prove, kuwa hawakuwateua, wala hawakuandika barua. Laiti mgejua Spika ana nini mkononi inayompa kiburi hivyo, CC ya Chadema isiwatumua, na sasa kikao cha BUK la Chadema, litapindua maamuzi ya CC ya Chadema, mchezo utakuwa umekwisha.

Just wait and see.
P

Pana mambo unayaruka mkuu:

1. Chadema hawakuwasilisha majina ya watakaokuwa wabunge wao wa viti maalumu kama utaratibu rasmi unaoafahamika unavyotakikana.
2. Si kuwa wamehukumiwa bila kusikilizwa bali kwa uamuzi wao wenyewe, hawakutokea kusikilizwa pamoja na kuwa walikuwa wamepewa wito rasmi wa kuhudhuria ili kusikilizwa.

Mkuu wangesikilizwa vipi bila wao kutokea kunako uliko wito?

Kama kutotokea kwenye wito ni halali unadhani nini kingewafanya watokee ili kusikilizwa kama kwao hiyo itakuwa ni kinga ya kudumu kuhalalisha kwao kutokusikilizwa?

Wenyewe 19 wanajua kuwa Chadema wametimuliwa isipokuwa Supika, Naibu supika na baadhi ya ma CCM!

Wajameni inaingia akilini kweri?
 
Tupige vita Maradhi Ujinga na Spika Ndugai
 
Back
Top Bottom